Hapa ngoja nikujibu.
TTCL wanatumia aina ya simu ambayo inatumia teknolojia ya CDMA (Code Division Multiple Access) ambayo ina uwezo mkubwa zaidi hasa katika mawasiliano ya "data". Kampuni nyingine inayotumia teknolojia ya CDMA ni Zantel, japokuwa Zantel nao wanatumia teknolojia ya GSM. Kampuni nyinge zote za simu zinatumia GSM, japokuwa kwa upande wa "data", wapo wanaodai kwamba wanatumia teknolojia ya CDMA. Hili sijathibitisha.
Kwa hiyo, ukiwa na simu ya TTCL, ukiweka line nyingine yoyote ile ISIPOKUWA ya CDMA, haitafanya kazi. Uamuzi huu ulifanywa makusudi na TTCL ili kuweza kukuletea huduma BORA ZAIDI, kwa kuwa kiwango cha mawasiliano kwa upande wa CDMA - kwa sauti na data - ni cha juu zaidi, na pia, teknolojia hii ina gharama nafuu zaidi kuliko teknolojia ya GSM ambayo kwa sasa haiwezi kushindana na teknolojia ya CDMA (ambayo inaweza kuongezwa ubora hadi kufikia WiMax na LTE kwa urahisi zaidi).
Hata ukijaribu kutumia IMEI, bila ya kuwa na line ya CDMA (ambayo haiitwi SIMcard bali inaitwa RUIMcard), hutaweza kuitumia simu yako kwenye mitandano mingine, ISIPOKUWA TTCL na Zantel.
Nimesomeka.