KERO Huduma mbovu NHIF Ilala

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mwishoni mwa mwezi Aprili nimeandika hapa malalamiko yangu kuhusu changamoto za utoaji huduma katika ofisi za Bima ya afya ya Taifa (Tawi la Ilala).

Hii changamoto imekwenda mbali zaidi na sababu kubwa ikiwa ni utashi wenye mashaka kwa watoa huduma walionipatia huduma.

Baada ya kulalamika kuhusu kupatiwa control namba kwa ajili ya malipo ya kadi iliyopotea, pasipo kujiridhisha na ukamilifu wa nyaraka zilizotakiwa, baada ya malipo kukamilika kupitia control namba niliyopatiwa, baada ya kurudi tena kwa mara nyingine ili kukamilisha kile kilichohitajika ikagundulika hata control namba niliyopatiwa haikuhusiana na jina la kadi iliyopotea (Wakati wa malipo haikuonesha jina lolote).

Hili liligundulika baada ya kwenda hosp. kutibiwa naambiwa kadi yako pamoja na ya mtegemezi wako mmoja zimezuiliwa kupata huduma. Nikashauriwa kurudi ofisi za Bima ili kujua tatizo ni nini?

Baada ya kufika ofisini wakaniambia kadi zimefungwa. Nikahoji kwanini wafunge kadi ambazo hazijapotea na iliyopotea iachwe active? Kuna mama mtu mzima (mtoa huduma) baada ya kuelekezwa niende kwake ndo akawa ameonesha sura ya kazi na kuhoji nani aliyenipatia huduma mpaka kupelekea makosa yanafanyika kiasi hicho?

Ikaamuliwa zile kadi zifunguliwe na niendelee na zoezi la kurejesha kadi iliyopotea.

Lakini mkwamo ukawa ni kwenye malipo niliyofanya, nimelipa control namba isiyo, nikawaomba pesa yangu wairejeshe ili niweze kulipia control namba mpya watakayonipatia.

Nikaelezwa niandike barua kuiomba hiyo pesa (Na inaweza kuchukua muda mrefu) ama la! Niipotezee mpaka pale itakapotokea nimepoteza kadi yangu mwenyewe (Control namba iliyotolewa ilikuwa ya kadi yangu).

Nilighafilika si kidogo.
Nimeleta malalamiko haya kwa mara ya 2 nijulishwe namna ya kurejeshewa hiyo pesa niliyolipia kwa makosa waliyosababisha wao wenyewe.

2. Ofisi kuwa makini na huduma wanazozitoa, ni kero kubwa kwa wapokea huduma.

NHIFTZ
Wizara ya Afya Tanzania
 
Back
Top Bottom