Huduma CCBRT bomu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huduma CCBRT bomu!

Discussion in 'JF Doctor' started by Mulama, Aug 23, 2011.

 1. Mulama

  Mulama JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Nimefika Hospiitali ya CCBRT tangia asubuhi ili nipime macho, cha kushangaza mpaka muda huu niko kwenye foleni! watu ni wengi ndio lakini wahudumiaji hawaendi na kasi kulingana na idadi ya watu hao, Daktari anaondoka kwenda kunywa chai masaa mawili akirudi anakaa kidogo anaenda lunch, akitoka lunch anakaa kidogo mara kapigiwa simu katoka kuelekea kusikojulikana, ili mradi taabu tu!

  Naona kuna Daktari mzee wa kizungu ana plasta shavuni masikini ndio anachakarika karibu mshine zote za kupimia macho ili kuhudumia wagonjwa, lakini watz wenzetu hawana time!. Hata hivyo manesi wanatumia mwanya huu kupendelea baadhi ya wagonjwa kwa kuweka mafaili yao juu ya waliowahi hapa sijui kuna mbinu gani inatumika ili upendelewe.

  Hivyo ndugu zangu kweli rahisi aghali ukitaka kwenda kupata huduma kwenye hospitali hii hakikisha umejipanga kutumia siku nzima au zaidi msikurupuke kama mimi nilivyofanya leo.
   
 2. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nenda muhimbili bana,au mwananyamala fasta tu unaendelea na mambo yako
   
 3. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #3
  Aug 27, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Pole Mulama kwanini ulikwenda CCBRT na wewe kwani unamatatizo sugu ya macho mpaka uende huko mbona kuna hospitali nyingi tu zinatibu kama ni kupima?? Hiyo Hospital inaviziwa na kila mtu kwa sababu ya bei nafuu.

  Pole hope umepata matibabu..
   
Loading...