Rais Samia katika ufunguzi wa Jengo la Huduma kwa Mama na Mtoto Hospitali ya CCBRT, Julai 5, 2022

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
1,521
9,008


=====
Tayari Rais Samia yupo ndani ya jengo la huduma ya afya ya mama na mtoto akiwasalimia wazazi pamoja na watoto wao (akina mama 88) ambao wapo katika wodi za kupumzikia wakiwa wamejifungua salama kabisa, pia Rais Samia amepata nafasi ya kukagua chumba cha kujifungulia.

Katika wodi hizo kuna wodi za kawaida ambazo wazazi hupana huduma bila malipo na pia kuna wodi za kupia maarufu kama (private ward) ambazo mtu atalipia ili kupata huduma ya hadhi anayotaka, katika wodi hizo mtu ataruhusiwa kuingia na mume au Baba wa mtoto kwenye chumba cha uzazi wakati Mke au akiwa anajifungua, au ndugu yake atakaeridhia awepo iwapo atahitaji kupata mtu wa kumtia moyo wakati wa kujifungua.

Rais amepata nafasi ya kuona vifaa vya kisasa ambavyo vipo katika chumba cha kujifungilia, kama vitanda, alamu kwa ajili ya kutoa mlio ikiwa kuna dharura na choo cha kisasa ambacho watatumia wazazi wakiwa huko ambacho kimejengwa kisasa kabisa kuweza kumsaidia mama kutokana na mazingira yake kwa wakati huo. Rais Samia ametoa zawadi kwa wakina mama ambao walikuwa wodi humo.

Jengo limefunguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan leo tar 5 Julai 2022. Wimbo wa Taifa unaimbwa kuonyesha heshima kwa Taifa letu.

Jengo hilo jipya limepewa jina la Rais wa Tanzania Samia, litajulikana kama Samia Suluhu Hassan matenirty ward.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu

Amesema anapata kigugumizi kusema watu wasivae barakoa, anasema nchi nyingine hawavai kwa kuwa watu wao wamepata chanjo karibu asilimia 70, na bado Tanzania kunapatikana watu wa UVIKO 19 na jana walikuwa na wagonjwa 7 na kati yao 6 walikuwa ni kutoka Dar es Salaam, amesema kama angalau asilimia ya watu 50 wangekuwa wapepata chanjo labda angesema watu wasivae barakoa ila watu wavae na wajitokeze zaidi kuchanja kwa ni hajui kirusi kingine kikija kitakuwa na hali gani.

Hotuba ya Rais Samia, Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tumshukuru Mungu kutujalia kukutana hapa kwa kazi ya ufunguzi wa jengo hili. Pia nawapongeza walioandaa hafla hii, na pamepambwa vizuri, Kwa namna ya pekee, nawapongeza waliochangia kifedha na kwa namna yoyote kuhakikisha jengo na vifaa tiba vinakamilika na hapa namshuru kwa namna ya pekee Rais mstaafu Jakaya Kikwete kwa kutafuta fedha na kuhakikisha hosptali hii inajengwa.

Hospitali imegharimu bilioni 101 na fedha kidogo juu na gharama zote hizo ni kupamtia mwanamke huduma bora ya kujifungua, hosptali hii inaweza kuhudumia wanawake 300 wa nje kwa siku, ina jumla ya vitanda 140 na vyumba 8 vya kujifungulia.

Kabla sijaja hapa nilitembelea hospitali hii mambo niliyoyaona hayana tofauti na kokote ulimwenguni na hivyo tukipimwa katika viwango tupo nafasi za juu katika Afrika na hapa kuna vyumba vya binafsi ambavyo vinaruhusu mama kuwa na mwemza wake wakati wa kujifungua, hii itafanya wanaume wajue kazi wanayokutana nayo wanawake na itawafanya wanaume waweze kutoa huduma na faraja ya kutosha kwa wanawake, hii nimeipenda na serikali tutaiga mfano huo.

Kuwepo kwa hospitali ya CCBRT nI kuendeleza mpango wa Serikali wa kunguza vifo vya mama na mtoto ambavyo vimekuwepo na serikali inaendelea kufanya juhudi kupunguza vifo hivyo ili kufikia lengo la uzazi salama.

Uhaba wa watumishi CCBRT waziri Mwenye dhamana ahahakikishe hospali inapata wafanyakazi kwa wakati na haraka ili iweze kutoa huduma kwa wananchi katika hali iliyo bora zaidi.

Tanzania ni kubwa sana serikali imefanya kazi kubwa kupeleka huduma za afya sehemu mbalimbali na kufikia hatua ya asilimia 81 ya wanawake kujingulia katika vituo vya afya, pia asilimia 10 ya wakina mama hujifungua kwa njia ya upasuaji.

Huduma bora ni njia ya kuzuia kutokea kwa fistula kwa wakina mama wanaojiufungua, na hospitali ya CCBRT inatoa huduma ya kutibu bila gharama wanawake wanaopata fistula, pia wapo watoto wenye umri wa miaka 12 mpaka miaka 4 wanaletwa wakiwa na fistula, na tatizo ni kubakwa.

Rais Samia amesema watu watoe taarifa za wanaume wanaobaka watoto ili wachukuliwe hatua za kisheria kwani wanaharibu watoto na kuwasababishia fistula, akaemia vikali vitendo vya ubakaji.

Vifo vingi vya kina Mama na Watoto wakati wa kujifungua vinatokana na Watoa Huduma kutozingatia weledi, kuwa na dharau au uzembe., watoa huduma wenye dharau ambao huwaonyesha dharau wanawake wanapokwenda kujifungua waache kwani inawafanya kina mama kupata ugumu kwenda kwenye vituo vya afya, pia kuna wahudumu wanaokataa kufungua milango wakifunguzwa nyakati za usiku na wakina mama wanaokwenda kujifungua usiku na hivyo kusababisha kina mama kwenda kwa wakunga wa jadi, huyo inarudisha nyuma juhudi za serikali kuhakikisha uzazi salama, watoa huduma hao waache mara moja na Wizara ya Afya fuatilia huduma katika Vituo vya Afya.

Inakadiriwa Wanawake 12,000 hadi 18,000 wana tatizo la fistula nchini. Watoto wa miaka 4-12 wana tatizo hilo huku sababu mojawapo ya tatizo hilo ikiwa ni Ubakaji, Jamii kutofumbia macho tatizo la Ubakaji, vitendo vya ubakaji, ukatili wa kijinsia, ndoa za utotoni na mambo mengine, mtoto mdogo anapewa mimba anaanza kusukuma mtoto anachana kila kitu mtoto anapata fistula. Hivyo vitendo viovu jamii ipewe elimu ili kuacha vitendo ivyo.
 

kamdudu

JF-Expert Member
Jan 20, 2015
1,546
1,433
Tahadhali kwa wanaume ‼️

Kama utajitia kimbele mbele cha kwenda kuangalia jinsi mkeo anavojifungua na kashudia hio K yake inavokua nakuapia utakaa mwaka mzima bila kuitumia tena

Usijaribu utakuja kunishukuru 🏃🏾‍♂️
 

da gulo

Senior Member
Jul 14, 2020
141
156
Tahadhali kwa wanaume ‼️

Kama utajitia kimbele mbele cha kwenda kuangalia jinsi mkeo anavojifungua na kashudia hio K yake inavokua nakuapia utakaa mwaka mzima bila kuitumia tena

Usijaribu utakuja kunishukuru 🏃🏾‍♂️
Naunga mkono💯💯💯💯 Yaani wanawake tuna MAUMBILE mabaya ndo Mana yamejificha.Yaan hiyo K inavyokuwaga wakati Mtoto anatoka,ewe mwanaume hutasex na mkeo nakwambia Maana utakosa hamu
 

Beberu

JF-Expert Member
Jan 26, 2017
1,271
1,205
Ila mbna mm nazionaga za kawaida tu
Just zinatanuka na kutoka damu na uchafu wa kawaida then zinafutwa zonakuwa normal kabisaaaa
Au niny mnasema K zinakuwa mbaya kwa kigezo kipi

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 

kamdudu

JF-Expert Member
Jan 20, 2015
1,546
1,433
Naunga mkono💯💯💯💯 Yaani wanawake tuna MAUMBILE mabaya ndo Mana yamejificha.Yaan hiyo K inavyokuwaga wakati Mtoto anatoka,ewe mwanaume hutasex na mkeo nakwambia Maana utakosa hamu
kuna wajinga hawanielewi ...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom