Mkuu Inaonekana hatta nilichokiandika hukukielewa.
Nakubali Africa ina uchu wa madaraka ndio maana hatuendelei.
Lakini hao unaowazungumzia wamarekani ni wabaya sannaaaaa.
Wana msemo wao "we don't have permanent friend we don't have permanent enemy".
Na kama hujui fikra zao ni kutaka kurithi rasilimali za Africa na kusema kuwa sisi wengi.
Ndio maana wakatuletea uzazi wa mpango ambao umesababisha kansa ya mlango wa kizazi sannaaaa.
Kutokana na vidonge vyake hvyo walivyotuletea.
Kwann hao hawatumii na wako karibia million 8oo huko?!
Wametuletea Magonjwa lukuki yanatuua ebola na mengineyo we unasema hawa Marekani wanatupenda?!
Yani sisi tungemwombea Gaddafi asife ili alete muonekano mzury wa Africa maana mikopo ya Wb migumu kulipika kwa riba kubwa na ukishindwa ilipa unashurutishwa kutengeneza mikataba ya rasilimali ambayo nyonyezi eti ww umiliki hisa 15% wao 85% si unyonyaji huo.?!
Sisi tunatakiwa tujilaumu wenyewe kiutawala wala sio China sawa mkuu.
Kwasababu hatta huyo America hana nia nzury na sis kila mmoja wao si china wala marekani wote wanaangalia maslahi yao.
Asa kwann nisimlaumu America kwa maafa aliyoyaleta Africa ety mkuu?!
Na bado anaenda kufanya udhalimu huko mataifa ya South America we bado unamchukulia mtu?!
Bora aanguke tyuu kuliko maafa anayotuletea.Bo
Hakuna Mzungu anayekuja na Dawa za uzazi wa mpango na kuwapa Waafrika Moja kwa moja bila kupitia Serikalini.
Ni lazima wakubaliane na Watawala na wataalam wetu ndio wanaotumika kuizitangaza .
Na hakunatu anayelazimishwa kuzitumia.
Kama hutaki achana nazo.
Matangazo mazuri ya kuzipamba yananaruhusiwa na viongozi wa Shit Hole Country wenyewe.
Hakuna Mmarekani anayekuja kuvamia Rasilimali zetu bila mikataba na viongozi wa Shit hole Country. Wakiambiwa wapeleke mikataba Bungeni ijadiliwe kwa uwazi kabla ya kuingia mikataba hiyo wanakua wakali na kuwaua wanaompinga hiyo mikataba.
Marekani inahusika vipi hapo?
Yani kabisa kabisa Afrika inastahili kuitwa rubbish shit hole Countries. Hayo Maovu yote hakuana mtu anayeweza kuyafanya kama kuna Demokrasia ya kusema kwa wazi na kuwakataa viongozi wanaouza rasilimali zetu na vyama vyao.
CCM waliuza sio rasilimali zetu lakini mpaka sasa wanatumia bunduki kuhakikisha wanakaa madarakani .
Marekani inahusika vipi hapo?
Ukifuatilia kwa umakini kila mkataba waliowahi kukaa kwenye madaraka wanahisa zao huko au walihongwa matofali ya dhahabu na wanapeta na kutuchagulia kwa nguvu ya risasi viongozi.
Hapo Marekani inahusika vipi?
Kwa nini leo hii Mahindi kwa kasi kubwa yanabadilishwa na kuletwa yale ya kutengeneza ili ukiyapanda Mara moja tu huwezi tena kutapanda bila kununua mbegu upya. Hata hovyo hakuna aliyejali kuwa wakulima wetu hawana uwezo wa kununua hizo mbegu muda wote mana zinahitaji hela na watakua wanazibadili kila Mara.
Hakuna aliyezileta bila serikali za Afrika kuridhia na hawataki majukwaa ya mikutano ya kisiasa ili watu wayazungumze hayo na kuwashawishi wananchi wawakatae wanaotumika na ikiwezakana kuwafungulia mashtaka na kuwafilisi Mali zao zote ili pasitokee mtu anayeingia mikataba isiyofaa .
Waliouza Madini yaliyoko ardhini ambayo hayakutengeneza na binadamu Bali Mungu kwa Wageni tunaweza kuwasamehe mana watasema hatuwezi kuyachimba ,Je, waliojigawia Nyumba na maeneo yote Mazuri ya serikali na kuyapangishia wageni na pesa zote zinaingia mifukoni Mwao wako Wapi ?
Je,kuna uwanja wa kidemokrasia huru wa kiwaelewesha wananchi ili wananchi waone dhulma waliyotendewa kwa wazi na watu waliowapa Ridhaa ya kutawala na kuongoza wakageuka wakajimilikisha Mali za umma?
Hapo Marekani anahusikaje?
Kwa nini tusianze kuwapiga vita hawa kabla ya Mmarekani aliyeko maelfu ya maili kutoka kwetu?
Hivi Pangekua na Katiba yenye misingi ya Haki sawa kwa kila mtu kuifuata leo hii kuna aliyewahi kutawala angekua uraiani akila bata kwa Mali zisizoelezeka katikati ya nchi maskini? Hapo Marekani inahusikaje?
Katiba kila mtawala Afrika hataki iruhusu Kuwashitaki wao maana wanajua hawapo pale kuwasaidia wananchi Bali kuwapa fursa wao na marafiki zao.
Ndio maana Nchi Maskini lakini watawala ni mabilionea kwenye katiba ya Kijamaa.
Leo hii nani asiyejua kuwa viongozi wa Kiafrika na Watawala wa kila Idara uwiano wao na Watumwa wao wanaoitwa wafanyakazi uwiano wao wa Mishahara ni zaidi ya 1:80 ? Halafu wanawaka hawataki Demokrasia ya kuwaacha wananchi washindane kwa haki ili wapatikane watu wenye Uchungu wa Kweli na Taifa lao.
Kuna watu wapo Tayari hata kuongoza nchi Kwa kulipwa milioni moja na kutembelea Landrover 110 na serikali yao yote kutembelea magari ya bei isiyozidi Milioni 60 mpaka uchumi ufikie ule wa Swiden.
Msafara unapita wa viongozi wa Nchi maskini za Afrika kwenda kuzindua Choo Cha shimo Cha shule ya Nyasi chenye thamani ya sh. Mil.20 feki ,ukipiga hesabu ya Magari yaliyowabeba Mabeberu wa kiafrika humo inafikai Bil. Tatu .
Hapo Marekani analaoumiwa vipi ?
Shit hole Country ni pale unapoona watu wanatumia mabilioni na kuchangisha fedha nyingi za mafuta na za kuwalipa watu wanaokimbiza Moto barabarani kuzunguka nchi nzima.
Bajeti yake hairuhusiwi kamwe kujadiliwa wala kuhojiwa.
Hakuna uwanja wa kidemokrasia was kukaa na kupinga huo mfumo ili kama Waafrika tuweke utaratibu mzuri utakaowapata viongozi watakaopiga marufuku huo upotevu wa kodi za wanyonge.
Mtu akipinga anakamatwa na hata kuuawa kuwa anapinga Moto unaokimbizwa.
Kweli moto usio na akili unaweza kuokoa rasilimali zetu badala ya kuwaacha watu wenye akili wapatikane kidemokrasia na tuwapate kihalali na kuwakabidhi Katiba inayobainisha wazi kuwa wakishindwa wataishia Gerezani au hata kunyongwa na familia zao kubaki maskini wa kutupwa kwa uzembe wao.
Hapo Marekani wanahusikaje?
Pakiwa na Demokrasia Afrika ya namna bora ya kuwapata watawala waadilifu kwa wazi ndipo Afrika itakapojitegemea mana Kama mtu kwa miaka Mitano na serikali yake hata kama ameshindwa kupaisha uchumi lakini mambo yote yamefanyika kwa wazi na kufuata sheria tulizojiwekea ,hakuna wizi ndani ya serikali yake,hakuna matumizi yasiyoeleweka kwenye idara zote bila kujali kuwa ni nyeti au sio nyeti uadilifu kwanza. Hata akishindwa kwenye uchaguzi lakini anajua ameshindwa kwa hoja na wananchi wamechagua kwa haki na kwa wazi kuanzia chini mpaka juu. Hakuna mtu atakayeleta fujo wala kumfunga hata akiwa nje ya madaraka atakua ameshindwa bila kutumia nguvu. Wananchi ndio wawe last say ya Nchi yao kwenye kura kwa haki na wawe na nafasi ya kuwasikiliza watu wote kwa usawa wakati wa kupiga kampeni.
Hapo Marekani wanahusikaje?
Watu wanatawala na kuwatisha watu wakati wa kampeni kuwa Fulani akishinda tunafanya mapinzuzi Daima halafu unailaumu Marekani?
Watu wanasema ushindi lazima hata kwa Goli la mkono halafu unailaumu Marekani?
Watu hao hao waliotumiwa na Marekani kufanya mapinzuzi ndio wanaokuambia kuwa Marekani anatusbabishia maskini!!
Hatuwezi kukwepa Kauli ya Trump. Mana ana nia njema na Afrika kuwakomboa watu wasitawaliwe na watu wale wale waliowaibia kwa miaka nenda rudi wakishirikiana na Mataifa makubwa.
Ni viongozi yupi Afrika aliyeweka Mali zake wazi na kueleza alivyozipata ?
Kuanzia Majumba ,maviwanda ,Mabasi ,malori, mahoteli, Ardhi ,biashara haramu, Ajira zenye maslahi mazuri ; vyote hivyo vina mikono ya watawala Afrika na wamevipata kwa kupitia kodi za wananchi na mikataba ya hovyo wanayoifanyia gizani!
Hapo Marekani inahusikaje.
Eti Ugonjwa wa Ukimwi umeletwa na Wamarekani. Wakati hata mbwa wana Kisonono kutokana na umalaya wao usio na kiasi.
Kila kitu Afrika kinafanyika bila utaratibu. Hivi nani analazimishwa asizae watoto kumi kama anaweza.
Mimi sijakatazwa popote kuzaa watoto wengi ni uwezo tu unanilimit na kukimbizana na malezi bora mana hata Ardhi ni ya serikali sasa watoto watarithi nini?
Zamani ningeenda porini nikajitangazia kjiji changu na kuzaa kijiji kizima na kufuga na kilimo . Leo Watakuja na Msururu wa magari na Wale Wanyapara wa wilaya na mabunduki na kutoa amri ya kukamata kijiji kizima na kukiweka gerezani eti nimevamia ardhi na sina hati ya kukitambua kijiji na siruhusiwa kuwapa watoto elimu ninayoona inawafaa ya kuwinda ,kufuga na kupambana na fisi wasivamie mifugo yao.
Wataitwa maskini kwa tafsiri ya wakoloni weusi na weupe?
Marekani analaumiwa vipi?
Adui wa Afrika ni Watawala wao.
Rafiki wa Afrika ni Adui wa Watawala wao.
Trump ni Rafiki mwema wa Afrika . Wangemwelewa wangeachana kabisa na Misaada na Kitu chochote kinachoitwa Mzungu au mkoloni mpya Mchina. Wakajiwekea mifumo yao wenyewe bila kutegemea Mtu yeyote zaidi ya wananchi wao.
Wakaweka Tafsiri yao ya maana ya maendeleo.
Kama Tunaweza Kutoa trilion Nane au kumi kujenga mradi mmoja kwa nini tunashindwa kujenga barabara mpya ya speed 140 kwa saa kutoka DSM mpaka Mwanza.
Kwa akili ya magari yenye dharura na yanayipia hiyo barabara hasa mabasi na mabasi ya kukodi na watu binafsi.
Kwa nini tunashindwa kujenga barabara mpya nyingine ya kutoka Dsm kwenda Musoma kupitia Arusha ya Kiwango cha lami na yenye upana na eneo la Mwendo kasi zaidi ya speed 100 mpaka 140 kwa saa.
Pesa za mradi mmoja tu zinazotosha kujenga barabara mpya kwenda mikoa yote na hata za vijijini ni jambo lilostahili kujadiliwa kwa wazi na wananchi wakapewa nafsi ya kuchambua faida ya mradi mmoja au ya kutumia fedha hizo kujenga barabara mpya na zisizo na kuna za ajabu ajabu na zenya upana wa kutosha nchi nzima mpaka vijijini.
Lakini bado tunamlaumu Trump.
Afrika tuweke Demokrasia ili tuwashindanishe wanaotaka kutuongoza kuelekea kwenye Maendeleo halisi na sio kutumia hisia za mtu mmoja bila kukosolewa.
Tuweke Mipango ya kitaifa na Sera za kitaifa ili tusikilize wachambuzi wa namna bora ya kuzitekeleza.
Zito Kabwe asimame achambue kuwa yeye angefanyaje ,Lisu achambue,Na mkubwa wetu achambue , Wapambe wao wachambue, Mbowe achambue ,Mbatia achambue kwa wazi kabisa bila kutishwa wala hofu bila kujali vyama , Asasi za kiraia wachambue , na wataalama wa uchumi wachambue bila kujali maslahi na ahadi za kuteuliwa.
Mana kinachotuumiza ni watu kulenga uteuzi hivyo kuweka unafiki Mbele huku watu kama akina Bashe na Serukamba wakionekana watukutu wakati wanayosema ni mawazo yao toka kichwani mwao na wanachoamini kama watanzania sio wasaka Vyeo wanaotumia kanuni za Kibeberu kupanga maendeleo bila kutumia Uhuru wa mawazo kama hao mabeneru waliowapa elimu hiyo ya uchumi.