Huawei Y 300-Unfortunately Stopped

mojave

JF-Expert Member
Apr 30, 2016
5,567
6,409
Habari za leo wanaJF..?

Naomba msaada wa kitaalamu juu ya simu tajwa hapo juu..
Hii simu nimeitumia tangu 2014 May lakini siku chache zilizopita ilianza kuleta maandishi juu ya kioo ambayo yanajirudia kila mara bila kuisha (kila application inakuwa inaandika UNFORTUNATELY STOPPED) na kunifanya nishindwe kuitumia.

Niliipeleka kwa fundi (Tanga ) akanambia simu hii haifai tena sasa nimeshindwa kuamini naomba msaada kabla sijaipeleka k/koo kwa mafundi ninaohisi wanamzidi huyu wa hapa Tanga...

Naomba kuwasilisha wakuu ...natumai ntapata msaada wa kitaalamu..
 
Muamini huyo fundi.Hilo ni tatzo linalohitaji flashing.Lakn hizo huawei zikishakuwa ivo huwa hazikubali kupokea file jingine.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Nnaamini hizi simu za siku hizi huwa designed kutumika si zaidi ya miaka miwili.

Kubali matokeo.
Hata mimi naamini hivyo.

Na ndo maana karibu kila mwaka huwa wanatoa matoleo mapya ambayo hata hayana tofauti kubwa sana na matoleo yalopita.
 
Nilikua na Y300 iliharibika ghafla hivyohivyo toka mwaka juzi kwenye mwezi wa 9 hivi, niliitumia toka 2013, mpaka leo ipo ndani inawaka ila ndio hivyo apps zote zinacrash na huwezi kabisa kuitumia, nina utaalamu kidogo na hivi vitu, kilichokufa hapo ni chip inaitwa eMMC, kwa tatizo hilo ndugu fanya kama nilivyofanya mimi, toss it inside and go buy a new one. wala usipoteze pesa kuitengeneza you'll be dissapointed.
 
mmmh nafwaa
 
Imesharudisha hela hiyo jipange kununua nyigine ukimiliki simu moja miaka yote hiyo mbona maduka yatafungwa
 
Niliwahi kumpelekea fundi akaniambia Huawei Ikishaleta huo ujumbe basi ujue imekufa
 
Simu za android sio rahisi kutumia zaidi ya miaka mitatu kwasababu zinashambuliwa sana na virus na sio imara.
 
habari za leo wanaJF..?

naomba msaada wa kitaalamu juu ya simu tajwa hapo juu..
hii simu nimeitumia tangu 2014 May lakini siku chache zilizopita ilianza kuleta maandishi juu ya kioo ambayo yanajirudia kila mara bila kuisha (kila application inakuwa inaandika UNFORTUNATELY STOPPED) na kunifanya nishindwe kuitumia.

Niliipeleka kwa fundi (Tanga ) akanambia simu hii haifai tena sasa nimeshindwa kuamini naomba msaada kabla sijaipeleka k/koo kwa mafundi ninaohisi wanamzidi huyu wa hapa Tanga...

Naomba kuwasilisha wakuu ...natumai ntapata msaada wa kitaalamu..
Fuata maelekezo yafuataya ikikwambia emmc read only haifai kutengeza: toa betri baada ya km sekunde 10 liweke muda huo unatosha isijiwashe yenyewe halafu bonyeza volume+&volume- kwa pamoja halafu power button utatokea mwanga wa pink km juu yake kuna maandisha haya emmc read only haitengenezeki
 
Fanya kama ifuatavyo zima simu yako kisha kwa pamoja bonyeza button mbili za kuongezea sauti na bila kuachia bonyeza power button.
Ikiwa itatokea rangi ya pink katika simu yako basi waweza kuiflash na ikapona
Ikiwa itatokea rangi ya pink kisha kwa haraka ikaondoka na kuleta maneno emmc readbonly basinujue simu yako imeua internal memory (emmc) yaweza kupona kwa kubadilisha hiyo emmc lakini mara nyingi inakuwa ndo mwisho wa safari yake
 
mkuu unaweza kutoiflash kabisa na tatizo lako lisirudie ,,in rahisi sana kwa kufanya hivi, ijue application inayokuwa stopped ,kwa mfano unfortunatelly instagram has stopped! maana hapo instagram ndo inahusika, sasa fatilia maelezo haya hapa chini.
1.nenda sehemu ya setting
2.tafuta sehemu palipo andikwa applications
3.moja kwa moja nenda kwenye hiyo app inayo stopped
4.ibonyeze italeta tabs "force stop" "unstall" "clear data"
5.bonyeza clear data hakiksha umemaliza process ya kuclear.
HAPO HAITARUDIA KULETA NENO HILO NA HUNA HAJA YA KUNUNUA SIMU NYINGINE KAMA UNAIPENDA
 
Fanya kama ifuatavyo zima simu yako kisha kwa pamoja bonyeza button mbili za kuongezea sauti na bila kuachia bonyeza power button.
Ikiwa itatokea rangi ya pink katika simu yako basi waweza kuiflash na ikapona
Ikiwa itatokea rangi ya pink kisha kwa haraka ikaondoka na kuleta maneno emmc readbonly basinujue simu yako imeua internal memory (emmc) yaweza kupona kwa kubadilisha hiyo emmc lakini mara nyingi inakuwa ndo mwisho wa safari yake
asante mkuu..ila imegoma
 
Kwanini hizi huawei zinatatizo hilo la kufa (emmc) kulko simu nyingine?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom