Nipeni jibu wana Jamii wenzangu! Ni nini kinachowatembelea wana ndoa siku hizi hatuzithamini tena ndoa zetu? Kuna kituko kimetokea ofisini kwangu leo asubuhi! Mama 1 wa makamo (above 50 I think), amevalia nadhifu kweli kweli na inavyoonekana hana shida ya hela, katinga kwa ofisi mapema anamtafuta bosi wa ofisi, bahati bosi alikuwepo ofisini akatoka, inavyoonekana wanafahamiana na bosi alishampa majibu ya kuwa hataki uhusiano naye lakini mwanamama anafanya kulazimisha. Big boss wetu ni kijana tu, alipata harisa na kufoka bila kutambua wafanyakazi baadhi tulikuwepo kwa kushuhudia hiyo scene, NENO KUBWA NA LA SAUTI, " MAMANGU NIMESHAKWAMBIA SIKUTAKI" nina mke wangu na watoto wangu SIHITAJI SHUGA MUMY. Naomba utoke ofisini kwangu. After 2 hrs yule mama katuma bundle ya Roses. Sasa sijaelewa amechanganyikiwa huyu mama au hakuelewa neno SIKUTAKI? Nilimcheki mama ana pete ya ndoa kidoleni sijui ni ya kweli au ni geresha?