How South Korea Developed! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

How South Korea Developed!

Discussion in 'International Forum' started by WA-UKENYENGE, Jul 22, 2012.

 1. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Katika pita pita yangu, nimekutana na hii wanaJF, inatia hamasa kwa nchi kama yetu yenye kila aina ya resources kuendeleza nchi na watu wako.
  Bofya hapa chini ni dakika 10 tu, SOUTH KOREA DEVELOPMENT HISTORIA
   
 2. Dotworld

  Dotworld JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 3,929
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
 4. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
 5. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
 6. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Halafu blueprint ya maendeleo haya ilifanyika wakati nchi ikiwa chini ya military dictatorship. Hili ni jibu tosha kwa wale wanaosema kuwa nchi haiwezi kupiga hatua za maendeleo pasipokuwepo utawala wa kidemocrasia.
   
 8. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Jana nilikuwa ninaangalia documentry fulani kuhusu mada hii hii. Moja ya sababu kubwa za maajabu hayo ya maendeleo ya S.Korea ni kuwa wamewekeza katika elimu. Kwa sasa S.Korea ni moja ya nchi zinazoshikilia kiwango cha juu cha elimu bora. Lakini "on the dark side of this education", idadi ya watu wanaojiua/kujinyonga ni ya juu zaidi kuliko nchi yoyote inayoendelea. Shinikizo la kutaka katokeo mazurio na aibu ya kushindwa kufanya vyema kweye masomo inawafanya vijana wa S.Korea wawe wanatumia muda wote kusoma.

  Shule rasmi inaanza asubuhi hadi saa 11 jioni, wakitoka hapo moja kwa moja wanakwenda kwenye tuitions hadi saa saba, nane usiku; wengi wao wanalala si zaidi ya masaa manne.

  Kutokana na kiwango cha suicides miongoni mwa wanafunzi, serikali imeamua kubadili mfumo wake wa elimu. Sasa watazawadia wale wanaojifurahisha zaidi bila ya kuharibu maendeleo yao ya elimu. serikali imeanxa na kupiga marufuku muda wa tuition mwisho saa nne usiku.
   
 9. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Siyo wanafunzi tu mkuu hadi maprofessor, akishindwa kitu au kufikia lengo au akiona there is no way atafanya kitu alichotarajia anajiachia. Achilia mbalia wanamziki wanajinyonga kila wakati, kuna high rate ya watu wengi sana kujinyonga kutokana na kwamba hakuna loophole za kuiba au kupata pesa haraka haraka bila kuisotea. Mfumo/system ulivyo ni kuwa mtu anayepiga kazi au kufanya kitu kinacholiingizia taifa faida au sifa ya kipekee ndiye mwenye kuweza kuzipata.
   
 10. Nyamgluu

  Nyamgluu JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 3,147
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  There is always a price to pay.
   
 11. zinginary

  zinginary JF-Expert Member

  #11
  Sep 22, 2016
  Joined: Dec 18, 2015
  Messages: 1,795
  Likes Received: 1,085
  Trophy Points: 280
  Daah
   
 12. mkorinto

  mkorinto JF-Expert Member

  #12
  Sep 22, 2016
  Joined: Jun 11, 2014
  Messages: 7,117
  Likes Received: 3,793
  Trophy Points: 280
  sasa bongo mtu kasogeza nyuzi moja tu, watu kamasi mpaka kitovuni.
   
 13. Ciprofloxacin.

  Ciprofloxacin. JF-Expert Member

  #13
  Sep 22, 2016
  Joined: Apr 15, 2015
  Messages: 1,099
  Likes Received: 1,400
  Trophy Points: 280
  isiwe chini ya ccm, hakuna maendeleo duniani bila Elimu bora.
   
 14. Ciprofloxacin.

  Ciprofloxacin. JF-Expert Member

  #14
  Sep 22, 2016
  Joined: Apr 15, 2015
  Messages: 1,099
  Likes Received: 1,400
  Trophy Points: 280
  isiwe chini ya ccm, hakuna maendeleo duniani bila Elimu bora.
   
 15. salazar

  salazar JF-Expert Member

  #15
  Sep 22, 2016
  Joined: Aug 13, 2016
  Messages: 688
  Likes Received: 372
  Trophy Points: 80
  Elimu elimu elimu
   
 16. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #16
  Sep 22, 2016
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Elimu ndio msingi wa maendeleo.
   
 17. Malcom Lumumba

  Malcom Lumumba JF-Expert Member

  #17
  Sep 22, 2016
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 4,826
  Likes Received: 8,155
  Trophy Points: 280
  Nimependa mwishoni tu " Despite many criticism about his style of rule, there is no doubt that South Korea would be a very different nation without him"

  Watanzania hawataki haya wanataka Democrasia ya Marekani na mijadala ya CNN,
  Hiyo ikifanyika wao ndiyo wanaridhika. Wanadhani Marekani na mataifa ya Ulaya yaliendelea tu kwa kupiga soga bungeni na kisiasa.
  Watanzania sijui nani katuroga sisi.

  Hebu tuanze na nchi ambazo zimepiga maendeleo makubwa ambapo kuna nyakati udikteta ilibidi uingie:

  1. China- tokea mwaka 1949 hadi leo ni nchi ya chama kimoja lakini tumona hali yao ya kiuchumi. Huku kulikuwa na ubabe kweli kweli lakini leo ni matajiri kuliko nchi ambazo wanasema wanafuata demokrasia.

  2. South Korea- Utawala wa kijeshi toka 1961 hadi 79 lakini ona hali yao ya uchumi leo. Hawa walimfunga hadi raisi wao waliyempindua na hata kupeleka majeshi Vietnam ulitumika ubabe, wengi walipinga.

  3. Malaysia- Mahathir Mohamad alitawala kwa zaidi ya miaka 22 tokea mwaka 1981 hadi 2003, tofauti kabisa na demokrasia ya wazungu. Leo Malaysia ni nchi kubwa ya viwanda na uchumi wao unazidi kukua.

  4. Urusi- Utawala wa kikomunisti tokea mwaka 1925 hadi 1991 ndiyo umeifanya urusi kuwa na viwanda vikubwa hadi leo. Jehuri yote ya Putin imejengwa na vizazi vilivyopita ambavyo walikuwa madikteta.

  5. Ujerumani- Tangu mwaka 1871 hadi 1945 utawala wa Kijerumani umekuwa wa kijeshi na kifalme. Lakini hata wakina Willy Brandit walikuta teknolojia kubwa sana imeachwa na dikteta Hitler pamoja na wanazi wenzake.

  6. U.S.A- Baada ya kupata mtikisiko wa kiuchumi wa mwaka 1929-1933 Roosevelt alipewa madaraka makubwa ambayo hata George Washington hajawahi kupewa tangu nchi iundwe. Republicans wakaanza kumuita raisi mfalme (Imperial President) na makakama kuu ya Marekani ilipinga sheria nyingi sana za NEW DEAL hasa mwaka 1936.
  Huyu huyu mwandemokrasia akapitisha sheria mwaka 1937 iliyompa nguvu kuchagua majaji kumi na tano wa Supreme Court of America. Hawa ndiyo waliomsaidia kupitisha sheria nyingi za kibabe hata kama mahakama za chini zitapinga, hii inaitwa COURT PACKING. Huyu jamaa alitawala awamu tatu kinyume kabisa na katiba ya Marekani na sidhani kama kuna raisi ataweza tena kufanya hivyo.
  Huyu dikteta Roosevelt ndiye amelifanya taifa la Marekani kuwa kubwa hapa duniani, na liwakataze wengine wasijaribu kuiga wao walivyofanya.
   
 18. Malcom Lumumba

  Malcom Lumumba JF-Expert Member

  #18
  Sep 22, 2016
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 4,826
  Likes Received: 8,155
  Trophy Points: 280
  Mkuu ukitaka cha uvunguni sharti uiname,
  Uchumi siyo sukari ambayo unaweka kwenye chai inakolea hapo hapo; unahitaji kujitoa; nguvu; uvumilivu na uzalendo wa hali ya juu ili kujengeka.
   
 19. mkorinto

  mkorinto JF-Expert Member

  #19
  Sep 22, 2016
  Joined: Jun 11, 2014
  Messages: 7,117
  Likes Received: 3,793
  Trophy Points: 280
  Mkuu tunaofahamu haya mambo ndio maana tunalia tunapoona watu wanapotosha mambo kwa makusudi kwa maslahi wanayoyafahamu wao wenyewe ni ya nani.

  Wimbo wa demokrasia unalazimishwa kuonekana ni mtamu kwenye masikio ya watu, wakati kuna nyimbo nyingine watu hawajazisikiliza.

  Uhuru wenyewe tumeupata kizembe zembe tu,tumekuwa wazembe hatujui hata maana kutafuta vizuri kwa gharama, tumeishia kudhani kwamba tunaweza kupiga hatua pasipo kuvuja jasho la damu kwa namna yoyote ile.

  Tena huu haujapasi kuitwa udikteta,anatakiwa aongeze drip tukae sawa.
   
 20. Malcom Lumumba

  Malcom Lumumba JF-Expert Member

  #20
  Sep 22, 2016
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 4,826
  Likes Received: 8,155
  Trophy Points: 280
  Dhana nzima ya kuwa na demokrasia kwenye nchi ni kumfanya kila raia apata kinda dhidi ya Seriakli pindi pale inapovuka mipaka. Na kwa upande mwingine ni kuikumbusha serikali kwamba hata kama ina dola lakini na wao ni raia kama wengine hivyo kuna uwezo wa kutoka pindi hamfanyi yanoyopaswa kufanywa na viongozi waliochaguliwa. Ndiyo maana tunaweka ukomo wa kutawala na kufanya chaguzi. Ule siyo mchezo ambapo umeamka tu asubuhi unaanza kulia na kupinga tu kila kitu; tukosoea panapohitaji kukoselewa na tusifie panapohitaji kusifiwa.

  Demokrasia ya leo duniani siyo ile ambayo Wagiriki wa Athens waliitunga.
  Kwanza kabla ya yote demokrasia ni lazima iendane na muktadha wa jamii husika.
  Ni lazima izingatie miiko ya kijamii, tamaduni husika, utu wa mtu na haki zote za raia.
  Leo wengi wetu tumeaminishwa kwamba chochote tutakacho kitaka basi tukiamua kupiga kula tutakipata, hii siyo kweli hata kidogo.

  Kamwe, demokrasia haimjengi mtu wala taifa.
  Bali watu hujenga demokrasia na taifa lao. Popote palipo na maendeleo ya kielimu na kiuchumi demokrasia huleta maendeleo chanya pasi kuvunja mshikamano na muunganiko wa watu. Lakini demokrasia hiyo hiyo kwenye jamii ambazo zipo nyuma kimaendeleo haswa kwenye nyanja ya kielimu na kiuchumi huleta mmonyoko mkubwa sana wa mshikamano wa kisiasa na kitamaduni.

  Mathalani, mpaka leo hii Uchina inajenga demokrasia japo ni ya chama kimoja. Naamini ipo siku itakuwa ni nchi ya kidemokrasia kwasababu watu wake wameendelea kielimu, kitamaduni na kiuchumi; maamuzi yao yatakuwa sahihi sana kwa maslahi ya taifa lao. Mwaka 2007 Marekani alipigwa vita sana na mataifa ya Ulaya kwa kufanya biashara kubwa sana na taifa la Uchina ambalo wao wanasema linjavunja haki za binadamu bila hata soni. Jibu la Marekani lilikuwa ni moja tu kwamba " Uchina ikiendelea kibiashara lazima lazima uchumi ukue na huo uchumi utawaletea watu maendeleo ya kielimu kuwawezesha waweze kufanya mapinduzi ya kifikra" Kwa hiyo msomi atabaki kuwa msomi tu, hata umuweke chini ya shimo. Binafsi naamini Tanzania tuna safari ndefu sana, tunahitaji mabadiliko makubwa sana ya kimtizamo na kifikra.
   
Loading...