HorsePower
JF-Expert Member
- Aug 22, 2008
- 3,612
- 2,569
Mara nyingi hawa watu huwa tunawa-mistreat, lakini ukweli ni kuwa wana msaada mkubwa sana na pengine bila ya uwepo wao, shughuli nyingi za nyumbani na malezi ya watoto wetu yangekuwa magumu sana! Kwa kifupi ni kama wanatulea.
Lakini pia wanaponyanyaswa na kufikia hatua ya kuchoka au ya 'liwalo na liwe' hugeuka kuwa wakatili kuliko simba! Nilishawahi kusikia habari za HG aliyemuweka mtoto kwenye friza na kisha kutoroka baada ya kunyanyaswa na mama mwenye nyumba kwa muda mrefu. Yupo mmoja aliyemuweka mtoto kweny oven kwa kutendwa mabaya. Na mwingine aliwahi kumdumbukiza mtoto wa bosi wake chooni na kutoroka kwa kile kilichoitwa manyanyaso ya mama mwenye nyumba. Wapo pia ambao hujirahisi kwa wababa wenye nyumba kwa nia ya kumkomoa mama mkorofi!
Kwa ushauri wa bure, ma hasa kwa ndg zangu wadada, hawa watu wanaweza kukudhuru na kuidhuru familia yako ndani ya masaa machache sana. Wanaweza hata kukuwekea sumu au kukufanyia kituko kibaya. Ni vyema tukawaheshimu hawa watu na kuishi nao kama ndugu wa damu. Kwa kufanya hivyo, watatusaidia kututunzia familia zetu na kulinda heshima ya ndoa zenu na waume zenu.