House girls wanapofanywa binadamu nusu!

House girls wanapofanywa binadamu nusu!

Nyie wanaume sababu hamshindi nyumbani pia vituko wanavyofanya hao mabek 3 pia ni vikubwa wengine wachawi, wezi wanawafundisha watoto tabia za ajabu
But tatzo ni kua beki 3 hakikosea mother house huna pa kusemea ngoja ww ukosee kila mtu atasema
They are good but sio kama wao ni malaika pia!
Wasichana wa kazi wengine ni headache jamani unakuta unaishi naye vizuri km mdogo wako, kazi zingine unasaidia km una muda, mfano nguo zangu na za Mzee housemaid hafui, niko nyumbani housemaid hanipikii Mimi, lakini sasa dah
 
Wanao wadharau hil kundi ni wale ambao wanawapata ukubwani, sisi tuliowakuta majumbani kwetu na wametulea, hadi tunakuwa na sisi kuanza kuwaajiri tunawaheshimu sana, ukija kwangu sio rahisi kumtofautisha na wengine, na wakiondoka huomba kurudi hata Kama nimemfukuza sio kwa Shida bali kusema kweli inamuia ngumu kufanya kazi kwingine, na huwa namrudisha ila akiondoka mara ya pili simpokei tena.
 
Hata kwa Mungu hatuwezi kuwa sawa ,mwenye dhambi na asiye na dhambi...Mwisho Wa siku ujumbe wako umefika tuwaheshimu hawa wenzetu nao ni binadamu tusiwachukulie kama punda
 
Wakati huo nilikuwaga humble sana house girls walininyanyasa sana. Nawalipa na wananipa mawazo daily. Sasa hivi tunaenda kwa mujibu wa sheria na mkataba na hivi serikali inataka wapewe 60 tu. Namheshimu kama mfanyakazi na haki zake za kikazi anapata ila atimize majukumu tuliyoandikishana otherwise natumbua.
Wewe Ndiyo yule yule unaye nyanyasa watoto wa wenzako, usijifiche kwenye kichaka cha kusema serikal, stupid subir muda wako utafika hata kwa kwa wanao
 
uzii huu ungehusu makalio ungepata likes nyingi sana pamoja na comments

Nimekuelewa sana Minded Tips! Watanzania wengi wako interested na mijadala isiyojenga. We need to address the issue of house girls. Akina mama wengi wanawatesa. With impunity!!!
 
Nasisitiza chanzo kikubwa cha tatizo hili ni kwamba jamii inawaona house girls kama watu daraja la mwisho!! Hili ni kosa kubwa. Serikali haijafanya la maana ku address hii issue. Zaidi ya blabla.
Hata baadhi ya familia za mawaziri zinanyanyasa wadada wa kazi! Don't they?
 
Nyie wanaume sababu hamshindi nyumbani pia vituko wanavyofanya hao mabek 3 pia ni vikubwa wengine wachawi, wezi wanawafundisha watoto tabia za ajabu
But tatzo ni kua beki 3 hakikosea mother house huna pa kusemea ngoja ww ukosee kila mtu atasema
They are good but sio kama wao ni malaika pia!

Then mrudishe kwao. End of story. Kwani lazima kuwa na house girl.
 
Ni rahisi sana. Kama una msaidizi wa kazi za nyumbani hajameet vigezo vyako katisha mkataba aende akatafute kwingine. Inefficincies zake hazihalalishi boss umnyanyase.
Mara nyingine huwa wana historia ngumu, wengine uelewa wa mambo ni mdogo, fanya bidii kumwelekeza vile ungependa afanye au awe.
Usimlaumu tu wakati baadhi ya vitu tunavyowatuma hata sisi hatuwezi kuvifanya.
Fanya bidii kubwa kumwelewa ili ujue utakavyoishi naye. Ukiona inakuwa ngumu mpe nafasi aende
 
Katika dunia tunayoishi kuna watu wamejaliwa kuwa matajiri na wengine ni masikini. Wapo mameneja wengine wahudumu. Huku mfyagizi kule CEO. nk nk.

Kuna wakurugenzi na walinzi. Huku makarani kule maafisa. Hapa makamanda kule makuruta. Huku wachungaji kule wanakwaya. Ilimradi watu wapo katika madaraja tofauti.

Ndio hadithi ya maisha ilivyo. Wengine wapewa maisha mazuri wakati wengine ni walalahoi.

Bill Gates anasema life is not fair. Get used to it. Tofauti za maisha zitakuwapo siku zote lakini zisitufanye tunyanyasane. Ingawa tunasema binadamu wote ni sawa lakini ukweli ni kwamba tuko sawa lakini 'sio sawasawa'

Familia nyingi kuanzia tabaka la juu, kati na hata la chini huajiri house girls ili kusaidia kazi za nyumbani.

Sehemu kadhaa wasichana hawa wamekumbana na mateso na manyanyaso kutoka kwa akina mama tena wengine wenye heshima katika jamii wakiwemo wachungaji nk.

Wasichana hawa huishia kutukanwa na kusimangwa kila mara. Kunyimwa chakula au kupewa makombo. Sehemu zingine hawaruhusiwi kukaa kwenye makochi!

Familia nyingi dada wa kazi huwa wa kwanza kuamka na wa mwisho kulala. Hutengwa wakati familia inakula na ni mara chache sana wanaruhusiwa kutoka.

Hulazimika kufanya kazi nyingi sana ingawa mshahara ni mdogo sana na kulipwa kwake kwa manati. Inashangaza kuona baadhi ya akina mama wanaonyanyasa house girls ni Wakristo au Waislamu. Wanafiki!

Tatizo kubwa ni kwamba kisaikolojia, jamii inawaona house girls kama ni watu daraja la pili. Hili ni kosa kubwa. Kuwa house girl au house boy hakumfanyi mtu kuwa binadamu nusu.

Ni fate tu imewafanya dada hawa kufanya kazi hizi. Wasinyanyaswe. Mama muone dada wa kazi kama binti yako.

Ni ujinga kumnyanyasa mtu anayekupikia chakula na au kukutunzia watoto wako. Unajiweka katika mazingira ya hatari. Usijenge uadui na house girl. She can be your doom.

House girl sio punching bag. Sio mtu wa kumalizia hasira zako za kazini au kero za mume. Wewe si binadamu bora zaidi kuliko huyo msichana.

Wewe pia ungeweza kuwa house girl shukuru tu fate imeamua vinginevyo. Aliyekupa wewe ndio aliyewanyima wasichana wa kaazi.

Anaitwa msichana wa kazi sio mtumwa. Alipwe ujira wake na heshima ya utu wake ithaminiwe kama watoto wako.
Ingawa nimesema kidunia binadamu sio sawasawa, mbele ya Mungu watu wote ni sawa. Tunaunganishwa na kifo. Uwe mkurugenzi uwe nani utakufa kama huyo msichana unayemnyanyasa.
Acheni kuwafanya house girls watu daraja la pili. Acha visingizio. Kama umeshindwa kuishi nae kwa upendo na staha mrudishe kwao. Period.
Nakuunga mkono 100%. Pamoja na kwamba nina maisha ya kawaida sana ila huwa najitahidi kumuhimiza mke wangu suala hili.
Ikiambatana na malipo ya posho kwa wakati.
Binafsi nawaona kama wanangu.
 
Akina dada na akina mama mkome kuwatesa house girls kwa sababu yeyote ile. Hao ni watoto wa akina mama wenzenu. Wewe utajisikiaje ukisikia mtoto wako ananyanyaswa?
Kumbuka hata wewe mtoto wako anaweza kuwa house girl au house boy.... Nani anajua ya kesho?! Take care
 
Back
Top Bottom