House girls wanapofanywa binadamu nusu!

House girls wanapofanywa binadamu nusu!

Nsimbi

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2014
Posts
1,091
Reaction score
1,208
Katika dunia tunayoishi kuna watu wamejaliwa kuwa matajiri na wengine ni masikini. Wapo mameneja wengine wahudumu. Huku mfyagizi kule CEO. nk nk.

Kuna wakurugenzi na walinzi. Huku makarani kule maafisa. Hapa makamanda kule makuruta. Huku wachungaji kule wanakwaya. Ilimradi watu wapo katika madaraja tofauti.

Ndio hadithi ya maisha ilivyo. Wengine wapewa maisha mazuri wakati wengine ni walalahoi.

Bill Gates anasema life is not fair. Get used to it. Tofauti za maisha zitakuwapo siku zote lakini zisitufanye tunyanyasane. Ingawa tunasema binadamu wote ni sawa lakini ukweli ni kwamba tuko sawa lakini 'sio sawasawa'

Familia nyingi kuanzia tabaka la juu, kati na hata la chini huajiri house girls ili kusaidia kazi za nyumbani.

Sehemu kadhaa wasichana hawa wamekumbana na mateso na manyanyaso kutoka kwa akina mama tena wengine wenye heshima katika jamii wakiwemo wachungaji nk.

Wasichana hawa huishia kutukanwa na kusimangwa kila mara. Kunyimwa chakula au kupewa makombo. Sehemu zingine hawaruhusiwi kukaa kwenye makochi!

Familia nyingi dada wa kazi huwa wa kwanza kuamka na wa mwisho kulala. Hutengwa wakati familia inakula na ni mara chache sana wanaruhusiwa kutoka.

Hulazimika kufanya kazi nyingi sana ingawa mshahara ni mdogo sana na kulipwa kwake kwa manati. Inashangaza kuona baadhi ya akina mama wanaonyanyasa house girls ni Wakristo au Waislamu. Wanafiki!

Tatizo kubwa ni kwamba kisaikolojia, jamii inawaona house girls kama ni watu daraja la pili. Hili ni kosa kubwa. Kuwa house girl au house boy hakumfanyi mtu kuwa binadamu nusu.

Ni fate tu imewafanya dada hawa kufanya kazi hizi. Wasinyanyaswe. Mama muone dada wa kazi kama binti yako.

Ni ujinga kumnyanyasa mtu anayekupikia chakula na au kukutunzia watoto wako. Unajiweka katika mazingira ya hatari. Usijenge uadui na house girl. She can be your doom.

House girl sio punching bag. Sio mtu wa kumalizia hasira zako za kazini au kero za mume. Wewe si binadamu bora zaidi kuliko huyo msichana.

Wewe pia ungeweza kuwa house girl shukuru tu fate imeamua vinginevyo. Aliyekupa wewe ndio aliyewanyima wasichana wa kaazi.

Anaitwa msichana wa kazi sio mtumwa. Alipwe ujira wake na heshima ya utu wake ithaminiwe kama watoto wako.
Ingawa nimesema kidunia binadamu sio sawasawa, mbele ya Mungu watu wote ni sawa. Tunaunganishwa na kifo. Uwe mkurugenzi uwe nani utakufa kama huyo msichana unayemnyanyasa.
Acheni kuwafanya house girls watu daraja la pili. Acha visingizio. Kama umeshindwa kuishi nae kwa upendo na staha mrudishe kwao. Period.
 
YOUR MESSAGE IS GOOD...

UKIKUTA VIDADA OFISINI STORIES ZAO KUHUSU WADADA WA KAZI ZA NYUMBANI... unaweza wazaba vibao... Unaziona kbs roho zao zilivyo mbaya...

NACHUKIA SANA ANAYEMNYANYA MDADA WA KAZI... NA KUMCHUKULIA AS IF SIO BINADAM UNAMGOMBEZA SOMETIMES KWA UPUMBAVU WAKO MWENYEWE AU WA MITOTO YAKO...
 
Jamani wadada wanateseka sana, unakuta mtoto amefika drs la sita eti anasubiri Dada wa kazi aje amsaidie kufuta na kubrashi viatu vya shule, amshushie net nk.
Hapo Huyo wa sita ana wadogo zake watatu wanamtegemea Dada wa kazi, hapo mama nyumba nae nguo zake na za baba zinasubiria Dada afue, hajapika, hajadeki, hajaosha vyombo.

MARUFUKU KUMTUMA MOTOTO HATA DUKANI.. AMETOKA SHULE AMECHOKA!!!
 
Wakati huo nilikuwaga humble sana house girls walininyanyasa sana. Nawalipa na wananipa mawazo daily. Sasa hivi tunaenda kwa mujibu wa sheria na mkataba na hivi serikali inataka wapewe 60 tu. Namheshimu kama mfanyakazi na haki zake za kikazi anapata ila atimize majukumu tuliyoandikishana otherwise natumbua.
 
Yaan hapa hii jinsia nyingine ndio hawalifikri wala kuwaza. Wao ni kejeli na kusahau kama nao ni watoto kama wake
Kiukweli sisi kina Dada ndio haswa tunawatesa hawa wanawake wenzetu.

Ila tusisahau pia kuishi na MTU baki ni kazi mwingine hata umfanyie nini ataona unamtesa tu!

Hata hivyo mama ukipata Dada mzuri mpende, mpende kweli, mpende haswaaa!!!
 
Nyie wanaume sababu hamshindi nyumbani pia vituko wanavyofanya hao mabek 3 pia ni vikubwa wengine wachawi, wezi wanawafundisha watoto tabia za ajabu
But tatzo ni kua beki 3 hakikosea mother house huna pa kusemea ngoja ww ukosee kila mtu atasema
They are good but sio kama wao ni malaika pia!
 
Back
Top Bottom