House girl na mume wa boss wake

House girl na mume wa boss wake

jangala

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2014
Posts
1,583
Reaction score
2,383
MUME: darl ninakikao mkoani kesho naomba niandalie vitu pls
MKE: dada zile nguo za baba pmj na soksi ulifua?
DADA: ndio nimepanga kabatini.

Mama anarudi chumbani na kumuomba hubby wakacheki TV sebulen, lakn baada ya muda mama anamuita dada akapange suruali kadhaa na mashati kwa ajili ya safari ya kesho, dada anapanga kila kitu anatoka.

MKE: kama tayari hakikisha unarekebisha yale mashuka pale kitandan weka na maji bafuni.

Dada anafanya na kwenda zake kulala, asubuhi dada anaamka mapema na kuandaa kila kitu ikiwamo na chai, baba anakunywa chai na kutaka kuondoka.

MKE: dada msindikize baba ili ufunge geti sbb bado ni giza
DADA: sawa mama.

Dada anatoka na begi la baba hadi nje kwavile mkewe yupo ndani, baba anamtaka dada abaki vizuri na watoto, dada anaitika na kusema nawao wanamuombea safari njema. Baada ya muda baba anarudi toka safari.

MKE: huku akitabasam, dada si umemuona baba amerudi vipi chakula tayari?
DADA: ndio.
MKE: haya kapange meza vizuri mimi nandaa juice.

Baada ya muda wanakula na baba anagundua juice sio nzuri anaamua kuiacha na kusema leo wamesahau kuweka baadhi ya vitu hivyo hataweza kuinywa. Baadae baba anakumbuka kuwa aliacha boxer zake kwenye ndoo ya maji chumban na kufunika mfuniko, anamuuliza mama vipi zile nguo zangu kwenye ndoo zilifuliwa? Maana nilisahau kusema kama zina maji.

MKe: dada njoo hapa hivi zile nguo za baba chumbani ulifua?
DADA: ndio mama (lkn hasemi kama alianua na kuweka chumbani kwake akidhan atakunja baada ya kazi kupungua)
MKE: darling zilifuliwa.
MUME: na watoto vipi wameshalala?
MKE: anajibu wamelala darl.
MUME: vipi dereva wao alifika kuchukua pesa yake?
MKE: dada eti uncle Hassan amechukua pesa yake?
DADA: hapana wamembadilishia gari uncle Hassan amesafiri kwa muda.

MKE: tutampatia darl siku akirudi acha dada aendelee kuitunza
MUME: basi vizuri, ehee vipi na tution walienda leo
MKE: ndio walienda (anamgeukia dada, si eti ee walienda si eti)
DADA: hapana Kelvin anaumwa leo siku ya pili nilinunua dawa dukan nimempa lkn hajambo.
MKE: (anashangaa) heeE! mtoto mgumu huyu kumbe jana alikua mgonjwa halafu wala!!! alikua anacheza tu jamani watoto!! Asante dada umefanya vizuri
MUME: haya mimi niwaache nataka nikapumzike lkn darl nitaomba zile boxer nichome kabla ya kulala sababu zimeanza kuchoka
MKE: anaingia chumbani anafungua kabati na kuzikosa lkn kabla hajajieleza anamuona dada analeta mzigo wa boxer zikiwemo chupi za mama na mataulo
MUME: basi dada zirudishe tutachambua kesho nenda kafanye kazi zako.

mume anainuka na kuelekea kulala, lkn anagundua mke wake alimwaga nguo kitandan wkt anatafuta boxer hivyo anaamua kurudi sebuleni ili aombe kuandaliwa kitanda, kwavile chumba cha dada kipo jiran na chao anagundua dada ameacha mlango wazi, anaamua kuufunga ili mbu wasiingie lkn anaona baadhi ya mashati na suruali zake zikiwa zimenyooshwa na kuwekwa pemben huku kitanda kikiwa kimetandikwa kwa ustadi anaamua kufunga mlango na kutoka, anafika sebuleni anakuta mama anatazama tamthilia anamwambia akatandike kitanda.

MKE: dada njoo, (kwa sauti ya kunong'ona) naomba ukatandike kitanda haraka
DADA: tayari nilipeleka viatu vya baba nikaamua kutoa na zile nguo
MKE: anaamka na kwenda kuhakikisha anarudi na kumwambia mumewe tayari aende akalale
MUME: anaenda kulala lkn huku akijuiliza sana ni nini amfanyie huyu dada kwa ukarimu anaowafanyia hapo nyumban, kwanza anajua ni vitu gani baba anabeba akiwa safarini, ndio pekee anaemtakia safari njema na kumuombea, ndio anaefua boxer zake na kutunza vizuri, ndio anaepika chakula kitamu, ndio anaetandika kitanda chake, ndio anaejua juice gani baba anapenda, ndio anaejua kama watoto wamerudi vipi kutoka shule, vilevile ndio anaejua kama watoto wake wanaumwa ama vipi.

Sasa mnafikiri baba atamzawadia nini huyu binti ambae amebakiza kujua style anazopenda baba tu, si atamfundisha ili kesho asimsumbue tena mke wake ambae kila kitu lzm amuulize dada. Akina baba hawaridhiki lkn wamama jitahidini hata kama mnamajukumu kiasi gani...
 
Kwa uzembe wa baadhi ya akina mama kila kitu kumuachia mfanyakazi ndoa nyingi zimepinduliwa 'dada wa kazi ana mipaka yke c kila kitu dada wa kaz unakuta mume anasahau hadi radha ya pishi la mkewe kwa mchezo huu dada wa kazi lzma awe first lady
 
Kuna heka heka niliisikia more than 6 years ago clouds fm dada akizungumzia jinsi alivyompindua mama mwenye nyumba sababu zilikuwa hizo hapo juu
 
Shida ni kwamba dada akishampindua Mama... Dada nae anakua mama.. Halafu na yeye anatafuta dada wa kumsaidia.. mzunguko unarudi palepale
 
Uyo ana haki ya kuchukuliwa mume mm najimudu na kazi zangu ndo mana sitaki house girl unajilemaza hivi hivi unajiona
 
That is life, hayo majaribu bana kote kote aiseeee dah!
 
Basi ngoja mumeo anyakuliwe nyakuuuuu kama mwewe anavyonyakua kifaranga cha kuku..
Najielewa mkuu..
Kazi ninayosaidiwa kufanya ni kuosha viatu tu.

Mume nitanyang'anywa na makahaba lkn cyo hg.
 
MUME: darl ninakikao mkoani kesho naomba niandalie vitu pls
MKE: dada zile nguo za baba pmj na soksi ulifua?
DADA: ndio nimepanga kabatini.

Mama anarudi chumbani na kumuomba hubby wakacheki TV sebulen, lakn baada ya muda mama anamuita dada akapange suruali kadhaa na mashati kwa ajili ya safari ya kesho, dada anapanga kila kitu anatoka.

MKE: kama tayari hakikisha unarekebisha yale mashuka pale kitandan weka na maji bafuni.

Dada anafanya na kwenda zake kulala, asubuhi dada anaamka mapema na kuandaa kila kitu ikiwamo na chai, baba anakunywa chai na kutaka kuondoka.

MKE: dada msindikize baba ili ufunge geti sbb bado ni giza
DADA: sawa mama.

Dada anatoka na begi la baba hadi nje kwavile mkewe yupo ndani, baba anamtaka dada abaki vizuri na watoto, dada anaitika na kusema nawao wanamuombea safari njema. Baada ya muda baba anarudi toka safari.

MKE: huku akitabasam, dada si umemuona baba amerudi vipi chakula tayari?
DADA: ndio.
MKE: haya kapange meza vizuri mimi nandaa juice.

Baada ya muda wanakula na baba anagundua juice sio nzuri anaamua kuiacha na kusema leo wamesahau kuweka baadhi ya vitu hivyo hataweza kuinywa. Baadae baba anakumbuka kuwa aliacha boxer zake kwenye ndoo ya maji chumban na kufunika mfuniko, anamuuliza mama vipi zile nguo zangu kwenye ndoo zilifuliwa? Maana nilisahau kusema kama zina maji.

MKe: dada njoo hapa hivi zile nguo za baba chumbani ulifua?
DADA: ndio mama (lkn hasemi kama alianua na kuweka chumbani kwake akidhan atakunja baada ya kazi kupungua)
MKE: darling zilifuliwa.
MUME: na watoto vipi wameshalala?
MKE: anajibu wamelala darl.
MUME: vipi dereva wao alifika kuchukua pesa yake?
MKE: dada eti uncle Hassan amechukua pesa yake?
DADA: hapana wamembadilishia gari uncle Hassan amesafiri kwa muda.

MKE: tutampatia darl siku akirudi acha dada aendelee kuitunza
MUME: basi vizuri, ehee vipi na tution walienda leo
MKE: ndio walienda (anamgeukia dada, si eti ee walienda si eti)
DADA: hapana Kelvin anaumwa leo siku ya pili nilinunua dawa dukan nimempa lkn hajambo.
MKE: (anashangaa) heeE! mtoto mgumu huyu kumbe jana alikua mgonjwa halafu wala!!! alikua anacheza tu jamani watoto!! Asante dada umefanya vizuri
MUME: haya mimi niwaache nataka nikapumzike lkn darl nitaomba zile boxer nichome kabla ya kulala sababu zimeanza kuchoka
MKE: anaingia chumbani anafungua kabati na kuzikosa lkn kabla hajajieleza anamuona dada analeta mzigo wa boxer zikiwemo chupi za mama na mataulo
MUME: basi dada zirudishe tutachambua kesho nenda kafanye kazi zako.

mume anainuka na kuelekea kulala, lkn anagundua mke wake alimwaga nguo kitandan wkt anatafuta boxer hivyo anaamua kurudi sebuleni ili aombe kuandaliwa kitanda, kwavile chumba cha dada kipo jiran na chao anagundua dada ameacha mlango wazi, anaamua kuufunga ili mbu wasiingie lkn anaona baadhi ya mashati na suruali zake zikiwa zimenyooshwa na kuwekwa pemben huku kitanda kikiwa kimetandikwa kwa ustadi anaamua kufunga mlango na kutoka, anafika sebuleni anakuta mama anatazama tamthilia anamwambia akatandike kitanda.

MKE: dada njoo, (kwa sauti ya kunong'ona) naomba ukatandike kitanda haraka
DADA: tayari nilipeleka viatu vya baba nikaamua kutoa na zile nguo
MKE: anaamka na kwenda kuhakikisha anarudi na kumwambia mumewe tayari aende akalale
MUME: anaenda kulala lkn huku akijuiliza sana ni nini amfanyie huyu dada kwa ukarimu anaowafanyia hapo nyumban, kwanza anajua ni vitu gani baba anabeba akiwa safarini, ndio pekee anaemtakia safari njema na kumuombea, ndio anaefua boxer zake na kutunza vizuri, ndio anaepika chakula kitamu, ndio anaetandika kitanda chake, ndio anaejua juice gani baba anapenda, ndio anaejua kama watoto wamerudi vipi kutoka shule, vilevile ndio anaejua kama watoto wake wanaumwa ama vipi.

Sasa mnafikiri baba atamzawadia nini huyu binti ambae amebakiza kujua style anazopenda baba tu, si atamfundisha ili kesho asimsumbue tena mke wake ambae kila kitu lzm amuulize dada. Akina baba hawaridhiki lkn wamama jitahidini hata kama mnamajukumu kiasi gani...
Kazi kwao nina miaka zaidi ya 20 sijui dada ni mtaa gani. Pamoja na majukumu lakini mume kwanza. Hivi unafikiri na hizi kucha za bandia ambazo hata kudonoa simu ni shida zitaweza hata kufua face towel achilia mbali kuosha vyombo. Mmmmmh
 
Back
Top Bottom