House girl ana mimba yangu

House girl ana mimba yangu

Mbembeleze akatoe,huu si ndio ushauri ulio utakua?

Sent from my iPhone 8 using JamiiForums mobile app
 
Hongera kwa kupata mtoto wa ujanani!

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Kijana wa form six hiki siyo kitu cha kuja kuanzishia uzi. Kwa umri wako ulitakiwa ujue ukisex kuna matunda na kama upo tayari nayo au la....

Sasa matunda yanakuja unakuja kuanzisha uzi!!?

Taratibu ni hizi
Pima naye
Kama ipo muulize ana mpango gani, kisha fanya atakachosema
kwa ushauri huo nahisi harufu ya damu changa isiyo na hatia. msithubutu kukatisha uhai japo huyo kiumbe hana mtetezi ila kumbukeni jicho kali la Mungu liko nanyi na itawaandama. huwezi kujua leo ukatae mtoto au vinginevyo kisha uje kuoa asiyejaaliwa uzazi. utalia kilio cha rohoni hadi unazama kaburini na majuto juu.
kiume na ubinadamu ni kuwaambia wazazi wako. huyo sio mtoto wa shule useme utashitakiwa kumharibia masomo, aibu ya wewe kudhan jamii itakuangalia kwa jicho ka kukuzomea (hadhi tofauti kati yako na bi. mkubwa) usiijali. madhari 'mlipeana kwa hiari yenu, tena nawe ukafunguka tena na tena hadi ukarutubisha; kiumbe ni matokeo + ya zile ' mechi za kirafiki' na USITHUBUTU kuikana 'damu' ya ujana wako kuitukuza fahari ya dunia.
 
Nimemaliza form six may mwaka huu nikarudi home, nyumban tupo 5 tu yaani baba, mama, wadogo zangu wawili na msichana wa kazi ambao asbh wakiamuka wanaenda shule na wazazi kazin, wanapoondoka kazin ninabakia na msichana wa kazi, mwanzo nilichukulia kawaida kukaa nae ila baadae nikabadili utaratb, wazazi wakiondoka naenda chumbani kwa dada( house girl) tunafanya yetu mpaka saa 2 anaendelea na kazi zake, Jana matokeo yametoka nimefaulu, leo kasikia baba yangu ananipongeza kwa kufaulu, kaingia chumbani kwake kanitumia msg ananiambia ana mimba yangu!!! Nifanyeje?
hakikisha kama ni yako,anaweza kukupakazia kisa umefaulu na anajua unaenda cho kikuu hivyo uhakika wa maisha upo,chunguza sana kama yako usikatae ndo jawabu la kubadili utaratibu

mi nilikua kama wewe na tukawa na housegal mkali mtoto wa kinyaturu esther,nimemaliza form 6 wakat huo,lakini sikushawishika ingawa yule dada alikua mzuri ajabu lakin nilimchukulia kama ndugu yangu tu.
 
Dogo nakufundisha kitu:

Jiwekee misimamo kuhusu wanawake..unanisikia?

Fanya hivi:- siku zote azimia kuwa mwanamke yeyote utakayelala nae kuwa utaweza kumfanya mke wa ndoto yako hivyo acha kuchovyachovya hovyo.

Pointi yangu ni kuwa msichana utakayelala naye ni lazima akidhi vigezo ulivyojipangia mfano awe na mvuto uupendao n.k

Sasa ona unabebeshwa mzigo ambao haukuwa kwenye mke wako wa future.
Wachache sana hapa duniani wana msimamo kama wako. Hongera sana. Wangepatikana 50% kama wewe dunia ingekuwa mahali safe kuishi.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Usiitupe damu yako, kuna kijana ninamfahamu alipata sijui niite bahati au janga kama la kwako. Yule kijana alimwambia housegirl aoundoke wala asimtafute yeye hawezi kuoa mtu wa hadhi ya house girl.

Kijana alimaliza shule na kuoa dream wife, miezi michache baada ya harusi alipata ajali na kuparalise spinal cord. Ilikuwa ni wazi hawezi Tena kupata mtoto maishani mwake.

Aliwaomba wazazi waulizie kijiji alichotokayule house girl anakuja kuletewa mtoto angekuwa chokoraa. KARMA
 
ae52b557272abe23adeb1ace323900b3.jpg


Post sent using JamiiForums mobile app
 
~~~>>Hili jukwaa tupo na wenetu na wengine wajukuu kabisa ....

Hongera kwa kufaulu kama kweli umefaulu.....

Mengine ya mimba utajua mwenyewe!

Sent using Nokia toch......
 
Back
Top Bottom