Hotuba za Rais kila mwezi

Je unaridhika na hotuba za Rais Kikwete?

  • Ndio

    Votes: 13 15.5%
  • Hapana

    Votes: 71 84.5%
  • SIJUI

    Votes: 0 0.0%
  • Sina jinsi

    Votes: 1 1.2%

  • Total voters
    84
  • Poll closed .
Hivi kwa nini hawafanyanyi " proof reading" kabla ya hizi hotuba kusomwa na Rais , ili ni jambo la aibu sana na kuhuzunisha ....whoever is writing these speeches should be fired.

JK si mtu makini, hii si mara ya kwanza, umesahau ile "cheque" aliyokabidhiwa mbele ya waandishi wa habari!! Tarakimu ilikuwa tofauti na maneno!
 
mmmmhhhh... I think you can predict what mzee mwanakijiji atasema hata kabla Rais hajaongea.
 
Nawaomba tuwe watulivu kwani utulivu wetu ni sehemu ya jawabu.

Busara ya huu msemo ni kama kiini macho tu.

Ukiwa, kwa mfano, safarini halafu chombo cha kusafiria kama meli au ndege kikaanza kupigwa na dhoruba mnaambiwa mtulie. Mkianza kuhamaki ovyo na kuruka ruka mnaweza kuzidisha matatizo kama kuyumbisha chombo, mkawa mnausaidia upepo kupepesua chombo. Lakini ukiendelea kuufikiria zaidi kidogo utagundua huu msemo ni mchanga wa macho. Mkitulia, ule utulivu wenu utakachofanya ni kutoongeza tatizo, lakini haufanyi lolote kupunguza lile dhoruba.

Rubani ndie yuko sehemu mahsusi ya kukabiliana na lile dhoruba. Tutulie, tusitulie dhoruba la hali ya hewa liko pale pale. Tena inawezekana tukitulia ndio rubani atadhani tunaona ni sawa tu, hususan rubani ambae hajali jali chombo kikiangamia kwa maana anateua makondakta ambao wanachochea dhoruba la ufisadi. Rubani na makondakta wake wao wana maparashuti ya kujiokoa na dhoruba la ufisadi kwa sababu wenzetu wana maakaunti nje ya nchi, na makampuni yao binafsi, na kinga za kisheria. Yani dhoruba la ufisadi wao haliwaangamizi, mambo yao yako "mswano," hivyo wanadhani na sisi tunaweza kutulia kama wao.

Kutulia sio sehemu ya jawabu.

Kikwete, do something. Your paid job, that is.
 
Sasa kweli tutegemee aongee nini? yeye binafsi keshakili kwamba hajakuwapo kama miezi mitatu. Kweli atazungumzia mambo yoyote ya ndani ya nchi?
Kwa sababu hiyo kaona ni vema aweke hapa usanii wake kwa kutuambia stori za majuu ambazo katu hazina msaada wowoteeeeeeeeeeeeee na nchi hii.
Hata visenti hivyo walivyoahidi amashapanga jinsi ya kuvifisadi tu. Hapa tumeliwa tena. Tusubiri 2010 tuone kama tutajifunga bomu au tuta save!
 
Mama weeee. Hivi hii ni "Travel briefing" au hotuba kwa Taifa? Nimesikitika sana, mkuu wa kaya, licha ya kuwa kimya kwa muda wote huo, ni hiki tu ndicho anachotuambia watanzania?

Hii ni ripoti ya kutoa UA (Umoja wa Afrika) au AU, sio kwa Watanzania. Nchi kiwa imekabwa na mambo lukuki, halafu tunaletewa "cheap talk"?.

Siamini...
 
Nilikuwa nina wasiwasi kwanini hapakuwa na hotuba lakini ukweli wa itinerary yake unaonyesha tarehe za mwisho za April, May na June ndizo alizokuwa safarini mh. Rais wetu... Na kwa kuwa anasema amesita kutoa recorded hotuba akiwa nje ya nchi... basi mimi mwananchi wa kuangalia mambo kwa upana zaidi nimemuelewa rais wetu.
 
!!!!!!!!!!!!!!!??????!!!!😱😱😱
 
Watanzania mlilikoroga lazima mlinywe. Mmezidi ujinga na ushabiki wa kijinga. CCM CCM! Halafu bado mnataka hotuba nzuri.Azungumzie Chenge na vijisenti vyake? Au RA na Richmond yake, au mnataka kusikia EPA, no mlitaka kusikia hatua zinazochukuliwa dhidi ya wezi wa pesa za msaada toka Japan?Nilitaka sahau, mlitaka awaambie anachukua hatua gani kwa Mzee wa mishavu BK na maafisadi wengine? Watanzania wananitia hasira kiasi nashindwa namna gani niwafutilie katika ramani ya Dunia. Ni wajinga, wanalalamika kupita kiasi na tatizo wanalijua lakini hawataki kuchukua hatua. JK anajua watanzania ni wajinga kiasi gani na ndo maana anawaletea hotuba hiyo. Mngekuwa mnajua mnastahili vilivyo bora, msingemchagua JK na CCM yake.Nasikitika sana nchi nzuri na tajiri ya asilimali tulipewa sisi waafrika-watanzania wajinga.
 
That man will never say anything kwenye issue zinazoyumbisha taifa sasa, hasa swala la muungano, wakati anajua kabisa kuwa linasubiliwa tamko lake rasmi la kusema kama zanzibar sio nchi na sehemu ya muungano anakuja na mambo ya AU, hivi kwa mtanzania wa kawaida value added ya hii hutuba hakuna kabisa.
 
nimejitolea kurefreshen his hotuba unpaid, anonymously, and in total and absolute confidence. Labda nimuandikie barua ya wazi ya kuomba kibarua cha bure.
 
Ama kweli hii siyo hotuba, ni hadithi.
Mhh! Zanzibar conflict hajagusa 2) epa hamna kitu 3) mkakati wa nchi kukabiliana na njaa hamna 4) jinsi ya kupambana na bei ya mafuta locally hakuna 5)taarifa ya madini kakaa kimya.
Hotuba umejaa "tumewaomba watusaidie", tumewaomba hiki" tumeomba kile".
Mbona hasemi jinsi alivyojizatiti kukabiliana na wahujumu wa nchi.
Ombaomba si suruhisho, suruhisho ni wewe Jk kusimamia utendaji na kuadhibu wahalifu wote wa uchumi wote.
Natamani tumlete kagame
 
ama Kweli Hii Siyo Hotuba, Ni Hadithi.

...huyu Msanii Angefaa Kuajiriwa Redioni Kama Mtangazaji Wa Kipindi Cha ...mama Na Mwana......

Siku Hizi Magazeti Mengi Serious Habari Zake Huwa Utazikuta Ukurasa Wa Tano...wamegundua Hazina Impact..
 



MegaPyne umetudanganya,

Hii haiwezi kuwa hotuba ya mtukufu rais kwa Taifa. Rais hawezi kulihutubia taifa kwa kupiga projo tu kuhusu za safari zake za nje na kumalizia na porojo nyingine za kutoa rambirambi kwa mara nyingine tena baada ya alizokwisha toa oafficially kuhusu msiba huo huo.

Rais huwa anatumia muda huu kutoa summary ya hali ya nchi (State of the Nation) na utendaji wa ya serikali yake.
 
Tanzania tunayokazi Kama huyu ndio rais,na inaonekana haambiliki hii si hotuba Kama alivyosema wajumbe waliyotangulia ilikuwa vema hii kuongelea ktk vikao vya AU.

Na kweli hii ni tusi kwa Watanzania kwa kuwa anajua kabisa anatuzuka na katupima kwamba kaona tunazukika,angejua kuwa majority ni watu makini asinge fanya hivi alichofanya.Maana matatizo ya taifa kwa sasa yako wazi kuwaambia watu watulie bila kuwaleza kipi kimefanyika na kipi kitafanyika au kinaendelea kufanyika ni failure kubwa kiuongozi.Alidhani lelemama ............ila mkwere hana aibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…