Informer
JF-Expert Member
- Jul 29, 2006
- 1,582
- 6,627
HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI WIZARA YA FEDHA MHE.KABWE ZUBERI ZITTO (MB) KUHUSU MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA 2011/2012
UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika, Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa afya njema na kuweza kusimama hapa mbele ya Bunge hili, kuwasilisha Maoni na Mapendekezo ya Kambi ya Upinzani kuhusu hali ya uchumi ya nchi yetu na bajeti kwa mwaka 2011/2012 kwa mujibu wa kanuni za Bunge, kanuni ya 96(6).
Mheshimiwa Spika, Naomba kwa niaba ya waheshimwa wabunge wote wa Kambi ya Upinzani ambao hawakupata nafasi ya kushiriki au kutoa rambirambi zao kwako kwa msiba mkubwa uliokupata wa kuondokewa na Mama yako mpenzi, nifanye hivyo kwa niaba yao.
Mheshimiwa Spika, Kabla ya kuanza kutoa mtazamo wetu naomba nikishukuru chama changu cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, viongozi wangu wakuu wote, kwa juhudi kubwa tunazozifanya ili kuhakikisha Watanzania wanaelewa maana halisi ya wananchi kuwa na mamlaka kwa Serikali waliyoiweka madarakani kwa njia ya kura. Vile vile na kwa umuhimu wa kipekee namshukuru Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Aikael Mbowe (Mb) kwa kuniteua kuwa Waziri Kivuli wa Wizara hii nyeti katika uchumi na maendeleo ya nchi. Kama ilivyo ada yangu, nitaifanya kazi hii kwa uaminifu, uadilifu na umakini mkubwa sana.
Endelea kusoma katika attachment hii chini