Hotuba ya Zitto Kabwe Bungeni Juni 15, 2011 - Bajeti Mbadala

Zitto mdogo wangu mungu akupe maisha marefu sana..Kuna siku utakuja kuvikwa nishani kwa umakini na uzalendo wako wewe!!! asante sana
 
naomba ufafanuzi tafadhali hapo kwenye red, wanasema budget iko supported na donors kwa 40%. Sasa ukichukua jumla ya budget ambayo ni Trilion 13.5 (?) ukatoa 40% ya wafadhili si tunabakiwa karibia na Trilion 8 hivi! Sasa kama deni linazidi kile tunachozalisha (kusanya) na increment ya deni ni 38% maana yake ni nini??? NCHI SI IMEFILISIKA!!!!????? Msaada wenu tafadhali wana jf

ndo manake yaani nchi imefilisika ..rais baada ya kuweka mikakati kutwa kuchekacheka na kusafiri kwenda ulaya kuomba neti za mbu kwake hayo ndo maendeleo
 
Nimependa sana ule mpango wa maendeleo vijijini, umenigusa kwani serikali itajikita kwenye ujenzi wa miundombinu hasa barabara na ukijumlisha na mradi mwingine wa kilimo na masoko ya uhakika- nasema maisha bora baada ya miaka 5 yataonekana.

Pia tatizo la usimamizi wa fedha za umma ni sugu, bila kujirekebisha kwa hili tutaendelea kubakia tulipo, hongera kambi ya upinzani kuliona hilo

Jingine hili na magari ya serikali kukopeswa kwa wanaostahiri na mengine kuwekwa kwenye pool, haya ndiyo yanafanyika katika nchi nyingi kubana natumizi yasiyo ya lazima kwa serikali - hongera kambi ya upinzani

Kuhusu Elimu, kuna uelekeo baadaye ikawa bure kabisa kwa dalili hizi walizokuja nazo, kwani kwa sasa wamejaribu kupunguza ada kwa vijana wetu na kipaombele kizuri ni masichana kusoma bure. wamefikia hapo baada ya kuainisha vyanzo vipya vya mapato na usimamizi mzuri wa fedha za umma.

Huwezi kuendelea kwa kutegemea misaada toka nje, bajeti imeanisha vyanzo vipya vya mapato, usimamizi bora wa raslimali zetu na kuwekeza taratibu kwenye elimu ya waalamu wa migodi yetu hasa kwenye makaa ya mawe, gasi asilia, umeme na uchimbaji wa madini.

Kifupi jamaa wamegusa maisha ya mtanzania wa vijijini moja kwa moja, na wale wa mjini ambao hawana kipato cha uhakika pia wamepatiwa njia mbadala ya kuendeleza maisha yao badala ya kukimbizana na maaskari wa jiji kila kukicha.

Thanks Zitto na crew nzima ya upinzani -- Tupo pamoja.


 
Hivi ilikuwa lazima u-quote hilo habari zima na mwisho uweke maneno 6 tu? Daaaa.......
kweli mkuu wakati mwingine hakuna haja ya ku-quote hasa kwenye maelezo marefu mengi, shida kubwa kwa wanao tumia simu....
 
Ni kweli Chadema wanakwenda na sayansi na teknologia yakizazi kimpya namuona muheshimiwa Zito Kabwe anavyoFlow kuhusiana na mapendekezo ya bajeti kutoka kambi ya upinzani kwakutumia IPOD na sio karatasi! anashusha mistari yenye vina hata Mustafa Mkulo anaikubali babaake!

Mkuu naona umekosea kidogo. Kifaa kinaitwa iPad na sio iPod kama ulivyoonesha hapo juu kwenye RED. Nmeona nirekebishe kwa ajili ya kutunza kumbukumbu vizuri. iPod ni mahsusi kwa kula muziki wakati iPad ni kwa kusomea.

ipad-ibooks.jpg

new-apple-ipad.jpg
 

Attachments

  • ipad-vs-iphone-2-1264623446.jpg
    ipad-vs-iphone-2-1264623446.jpg
    29.6 KB · Views: 30
Wanajamii

Nimebahatika kumsilikiza vizuri Mh. Zitto wakati akiwasilisha Budget mbadala ya Kambi ya Upinzani, hakika ni budget yenye mshiko na mwelekeo wa ujenzi wa taifa bora. CCM na serikali yake wasiipuuze hata kidogo!

Ninasema hivi, yeyote atakaeiponda budget ya upinzani atakuwa na lake na kwa vyovyote ni mchawi!

Hongera Mh. Zitto Kabwe na CDM kwa ujumla:israel:
 
Hii hotuba nadhani ni miongoni mwa mambo ya muhimu yaliyozungumuzwa bungeni kwenye mkutano huu, pamoja na ile ya Mh Natse MB (CHADEMA)
 
hata mimi nishamjua mchawi mwingine wa nchi baada ya yule wa kwanza ambaye kwa sasa ni marehemu..
 
katibu uenezi wa magamba kaiponda... so nimepata jibu.


nape ni mchawi tu............yeye katumwa na mabwana zake awe anapinga kila kitu kitakacholetwa na cdm........ na atajuta sana mwaka huu kwa kukubali kutumiwa kwa maslah ya watu wachache
 
Where is Zitto tunaomba kopi ya Bajeti tafadhali sana if possible tupate zote na ile ya Serikali wengine hatuja zisoma vyema mstari kwa mstari
 
Back
Top Bottom