Mtaka Haki
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 492
- 149
Pamoja na kwamba CDM ni wazuri sana katika kujenga hoja na katika hotuba zao lakini natamani wana JF mjaribu kuweka maoni yenu hapa juu ya mamno ambayo ni muhimu wananchi wakayasikia siku ya Alhamisi. Haya hapa chini ni maoni yangu juu ya yale ambayo natamani yasikosekane.
1. Sababu ya kutokumtambua meya haikuwa ni kwa kukosa vyeo. Ilikuwa ni ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi na kutokuwapo kwa haki.
2. Pale ambapo waliokuwa wanapigania haki kufuatwa na ghafla wanageuka na kubadilisha agenda toka kwenye ukiukwaji wa haki na kutokufuatwa kwa taratibu na sheria na kuishia kuwa agenda ya kugawana madaraka, basi mtu unaweza kuamini kuwa kuna nguvu nyuma ya jambo hilo. Na endapo chama kikausaidia kujenga msingi wa kusimamia haki bado wewe ukageukwa basi ni rahisi watu kuamini kuwa kuna nguvu nyingine nyuma yako.
3.Chama makini hakiwezi kuruhusu wanachama wake wachukue hatua ambazo ni kinyume na misingi ya haki inayoainishwa na chama chao kwa maslahi binafsi ya vyeo.
a)Hatuwezi kuwa kama wengine wanaosema watavua magamba na kila siku wanaendelea kuahirisha kwa hofu ya kuogopa matokeo yanayoweza kuletwa na maamuzi magumu.
b) Pale ambapo kwa sababu zisizoeleweka na kwa ghafla wanachama wanabadilisha msimamo basi kunakuwepo na mmomonyoko wa maadili
na hapo inabidi kuchukua hatua hata kama hatua hizo zitakigharimu chama kukosa nafasi ya udiwani lakini tutakuwa tumejenga na kutetea haki hata kama ni kwa hasara yetu.
4. Endapo tutashindwa kuchukua hatua basi hatukuwa na haki ya kupiga kelele na kuwashangaa wale wanaoshindwa kuwachukulia hatua watuhumiwa wa ufisadi huku wakiahirisha kila siku. Hatuwezi kuruhusu Gamba kuota kwani tunajua magamba yakiota inakuwa vigumu kuja kuyavua kwani mengine yanaleta hofu ya kutoa damu yakishaachwa kwa muda mrefu.
5. Ujumbe tunaotaka uende kwa kila mtanzania ni kuwa CDM ni chama kinachosimamia na kutekeleza kwa vitendo misingi ya utawala bora na ufutwaji wa haki , taratibu na sheria.
6. Mambo yanayofanywa kihuni na kwa ubabe hayapaswi kukubaliwa hata kama matokeo yake yana maslahi binafsi kwangu. Ni lazima tuangalie mbali na kusimamisha utaratibu wa kisheria na kutimizwa matakwa ya demokrasia.
7. Hatuwezi kuwa kama watu wengine ambao uongozi umewashinda, huku wakitoa matangazo ya kufukuza watu na bado wakipatwa na hofu kila wanapokutana na kuishia kuahirisha. Ni lazima chama makini kichukue maamuzi magumu kwa maslahi ya taifa na maslahi ya taifa kwa hili ni kuzuia ukiukwaji wa haki taratibu na misingi ya kidemokrasia katika chaguzi mbalimbali.
NAOMBA KUWASILISHA ONGEZENI HAPA CHINI
Hii ni ajabu kabisa.
yaani unafundishwa namna ya kuwapooza wananchi wa Arusha.
Hotba safi ni ile inayoangalia yaliojiri na maamuzi yenu je yanasaidia nini katika maendeleo ya jamii ile, na je yamejenga amani na utulivu?
lakini kikubwa na kukonga nyoyo za wananchi wengi waliowachagua.
Je mnaona kama uchaguzi utafanyika katika kata husika, mna nafasi hata ya kupata kiti kimoja.
Siku zote kiongozi hatungiwi hotba bali anazungumza kutokana na matokio.
kazi ipo kwa Chadema kuleta hotba za kuleta amani na kujenga mshikamano husisan pale mlopoharibu.
Mkuu hii hotuba inayobeba ujumbe wa Arusha hasa hongera sana na ninawashauri viongozi wa Chadema kuichukua na kuifanyia baadhi ya marekebisho ambayo wao watayaona yanawafaa lakini hii siyo ya kuiacha imejaa ujumbe unaoeleweka
Mimi naona Godbless Lema ni mnafiki namba one ambapo kama kamati kuu ya Chadema ingekuwa makini walitakiwa wamfukuze Chama kabisa.
Kwani yeye ndio chanzo kikuu cha mgogoro huo kwani yeye pamoja na kuwa ni Mbunge lakini ni Sehemu ya baraza la madiwani waliofikia muafaka ule ambao chadema wameukana.
Na kama anasema yeye hajui lolote ila baraza la madiwani wa walifanya siri BASI HASTAHILI KUWA KIONGOZI WA WATU SABABU ILI MBUNGE AFANYA KAZI ZAKE VIZURI ANAHITAJI KUSHIRIKIANA NA MADIWANI WAKE. Kwa sababu hizo mbili alilazimika kufukuzwa kabisa ndani ya Chama. Kwani viongozi wanafiki ni khatari sana katika jamii.
Lakini maamuzi ya kamati kuu hayawezi hata siku moja kuweza kukidhi haja ya wakaazi wa Arusha kwani siku zote wananchi wanahitaji maendeleo na sio malumbano.
naamini wazi madiwani hao wakifikisha suala lao mahakamani kupinga kuenguliwa kwao ndani ya Chama na sababu zilizotumika kuwaondoa basi wana nafasi kubwa sana kushinda na kurejeshwa katika nafasi zao kama madiwani kwa Amri ya mahakama.
Na naamini kuwa kama uchaguzi utafanyika kuziba nafasi za madiwani hao. CCM watashinda viti vyote na hakuna kuwa na muafaka.
Nimewapenda sana msimamo ulioonyeshwa na madiwani hao katika kusimamia kile walichokusudia.
Chadema walishindwa kusoma alama za nyakati.
kama ana akili timamu atakuwa amekuelewa.Ndugu Baru baru,siri BASI HASTAHILI KUWA KIONGOZI WA WATU SABABU ILI MBUNGE AFANYA KAZI ZAKE VIZURI ANAHITAJI KUSHIRIKIANA NA MADIWANI WAKE

Hii si kweli,

Hivi, kama madiwani wote hawakushirikiana na Mbunge au wakitofautiana na Mbunge na kama ktk tofauti hiyo madiwani wamevunja kanuni na katiba ya Chadema na kama Mbunge Lema yuko sahihi pmoja na kuwa yuko peke yake nani anapaswa kuitwa mnafiki?

Je, wingi (Madiwani wote) Vs Mbunge Moja huwa unabaidilisha ukweli? Kwamba madiwani wote wako upande moja lazima wawe sahihi? Hapa naomba nikuhakikishie tu kwamba Godbless Lema yuko sahihi kwa mujibu wa taratibu za chama.

Pili, madiwani watano kati ya 11 ndo waliotimuliwa kwa hiyo. Lema yuko pamoja na zaidi ya Nusu ya madiwani waliotii amri ya kamati kuu ambayo G. Lema ni mjumbe. period

wananchi wanahitaji maendeleo na sio malumbano.

Hapa nani analeta malumbano.

Mosi, Nani aliyevunja kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa wakati wa uchaguzi wa mmea wa Arusha ambayo ndo imeleta yote haya?

pili, Ni nani aliyekwenda kudanganya wabunge kuhusu uchaguzi wa mmea wa Arusha na Maandamano ya Arusha kati ya Chadema ( Lema ) na CCM (Pinda )wakati akija swali la Mbowe?

Tatu, Nani sasa aibu yake imewekwa kapuni na Speaker Anna Makinda kati ya Chadema na CCM?

kurejeshwa katika nafasi zao kama madiwani kwa Amri ya mahakama.

Mosi, according to our current weak constitution hilo haliwezekani. Hili lilitokana na woga wa CCM kuogopa mgombea binafsi. wamejinasa wenyewe ktk mtego waliotega wenyewe.

Pili, Kama CCM itafanya chochote wawezalo makamani na kuwarudisha hawa madiwani madarakani that has nothing to do with uamuzi wa KAMATI KUU YA CHADEMA. WanaArusha na watanzania watakuwa wameshajua Chadema inasimamia nini na madiwani hao wamesimamia nini ktk sakata la Arusha? That is enough. But I doubt if the court can judge that way.

CCM watashinda viti vyote na hakuna kuwa na muafaka

Sasa ndugu yangu hili la imani yako kuwa CCM itashinda hatuwezi kulijadili sana. Imani haijadiliki ila nina maswali mawili.

Mosi, kwanini hawa wana ccm haikuchaguliwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010?

Pili, umeshaongea na wapiga kura wangapi ktk kata hizo nne mpaka ukawa na imani kwamba mtashinda kata zote?

Nimewapenda sana msimamo ulioonyeshwa na madiwani hao katika kusimamia kile walichokusudia.

Chadema walishindwa kusoma alama za nyakati.

Ni kweli wamesimama kidete kutetea hicho walichokusudia yaani ( Vyeo vya unaibu mmea na wenyeviti wa kamati) Bahati mbaya msimamo wao umekwenda kinyume na katiba na kanuni za Chadema. Hawakupaswa kufanya hivyo ( kuomba vyeo kupitia mwafaka) bila ridhaa ya viongozi wa Arusha wa Chadema na kamati kuu.

Huo ndio ukweli mkuu.
ninaamini watayazingatia maoni yako mkuu kwani ni muhimu watu kuwa na kimuhemuhe na chama chake
Hotba safi ni ile inayoangalia yaliojiri na maamuzi yenu je yanasaidia nini katika maendeleo ya jamii ile, na je yamejenga amani na utulivu?
lakini kikubwa na kukonga nyoyo za wananchi wengi waliowachagua.]
Nadhani haya ni maoni yanayounga mkono kwa nini viongozi wa CDM wamechukua hatua walizochukua. Na kwa haponimeonyesha yaliyojiri na maamuzi haya yanasaidia sana jamii kuzingatia taratibu, haki, demokrasia na sheria zilizowekwa.
ThanksHongera sana Mtaka Haki, pointi ulizoeleza ni za msingi sana, watu wa Arusha walikuwa tayari kufa kwa ajili ya haki si viongozi wachache kugawana madaraka. Chadema imechukua hatua nzuri na ngumu sana, ifike wakati chama (Taasisi) kiwe/ iwe na nguvu kuliko watu bibafsi na maslahi yao. Hongera sana kwa uzalendo wako, Mungu akuzidishie.
'By overcoming your fear you prove your worth'.To make clear i mean 'making decisions'