Hotuba ya viongozi wa CHADEMA huko Arusha

@Barubaru. Umejaribu kujenga hoja lakini imekaa kinafiki.

Wakazi wa Arusha ndio wana maamuzi wamchague nani sio wewe.

Madiwani hao 5 walionunuliwa na magamba ndo wako mtaani na hawana nyimbo.

Kwa taarifa chama makini kinataka viongozi quality na sio QUANTITY!

Pole! Naona CDM imewashika pabaya

Haijalishi nani atashinda au laa! Chadema hata kama watapoteza kata zote 4 wamefanikiwa kwa kufanya maamuzi magumu, wametoa fundisho juu ya makali yake. Alhamis mambo yote hadharani! Umejenga hoja vyema mkubwa!

Cdm wanaona mbali na sio kukumbatia maovu kwa maslahi binafsi heko kwa uongozi mzima wa cdm

Hii ni ajabu kabisa.

yaani unafundishwa namna ya kuwapooza wananchi wa Arusha.

Hotba safi ni ile inayoangalia yaliojiri na maamuzi yenu je yanasaidia nini katika maendeleo ya jamii ile, na je yamejenga amani na utulivu?

lakini kikubwa na kukonga nyoyo za wananchi wengi waliowachagua.

Je mnaona kama uchaguzi utafanyika katika kata husika, mna nafasi hata ya kupata kiti kimoja.

Siku zote kiongozi hatungiwi hotba bali anazungumza kutokana na matokio.

kazi ipo kwa Chadema kuleta hotba za kuleta amani na kujenga mshikamano husisan pale mlopoharibu.

we Batilda tulia weka makalio kwenye mkeka waache watu wafanye kazi. Umeshindwa kwenye uchaguzi kazi yako ni kulala na waume zako tu sasa

Haijalishi nani atashinda au laa! Chadema hata kama watapoteza kata zote 4 wamefanikiwa kwa kufanya maamuzi magumu, wametoa fundisho juu ya makali yake. Alhamis mambo yote hadharani! Umejenga hoja vyema mkubwa!

Nakubaliana na wewe mkuu kuwa kwa hili la maamuzi magumu ndio kushinda kwenyewe.

Mimi naona Godbless Lema ni mnafiki namba one ambapo kama kamati kuu ya Chadema ingekuwa makini walitakiwa wamfukuze Chama kabisa.

Kwani yeye ndio chanzo kikuu cha mgogoro huo kwani yeye pamoja na kuwa ni Mbunge lakini ni Sehemu ya baraza la madiwani waliofikia muafaka ule ambao chadema wameukana.
Na kama anasema yeye hajui lolote ila baraza la madiwani wa walifanya siri BASI HASTAHILI KUWA KIONGOZI WA WATU SABABU ILI MBUNGE AFANYA KAZI ZAKE VIZURI ANAHITAJI KUSHIRIKIANA NA MADIWANI WAKE. Kwa sababu hizo mbili alilazimika kufukuzwa kabisa ndani ya Chama. Kwani viongozi wanafiki ni khatari sana katika jamii.

Lakini maamuzi ya kamati kuu hayawezi hata siku moja kuweza kukidhi haja ya wakaazi wa Arusha kwani siku zote wananchi wanahitaji maendeleo na sio malumbano.

naamini wazi madiwani hao wakifikisha suala lao mahakamani kupinga kuenguliwa kwao ndani ya Chama na sababu zilizotumika kuwaondoa basi wana nafasi kubwa sana kushinda na kurejeshwa katika nafasi zao kama madiwani kwa Amri ya mahakama.

Na naamini kuwa kama uchaguzi utafanyika kuziba nafasi za madiwani hao. CCM watashinda viti vyote na hakuna kuwa na muafaka.

Nimewapenda sana msimamo ulioonyeshwa na madiwani hao katika kusimamia kile walichokusudia.

Chadema walishindwa kusoma alama za nyakati.

nadhani mkuuu hapo khs uchaguzi utakaokuja tuwachie waakazi wa Arusha wafanye maamuzi yao. wacha jamaa waende mahakamani kama watahisi hawakutendewa haki. inatubidi tufike mahali UOGA NA HOFU usitunyime usingizi, CDM watakuwa tayari kupokea matokeo...., hilo linafahamika. mabadiliko ni ya lazima hapa nchini mwetu kipindi hiki!

Kwa kweli hii imekaa vizuri hongera. Ninaona watu wa magamba wanavyojikanyaga hapa, wanahangaika kuitafutia hoja ya kuipinga lakini wameshindwa. Wananchi walikuwa na hamu ya kusikia huu mfano wa madiwani ili kujua ya kuwa hata mbunge akienda kinyume na sheria inabidi awajibike. Chadema wapewe nchi hata kesho tutawaona waliouza na waliokula mashirika yetu mpaka watanzania tumekuwa kama mayatima.

Asante Mkuu. Penye Ukweli uongo hujitenga. Kwa kuwa kila mtu anaelewa jinsi ambavyo wengine wanapata kigugumizi katika kuwachukulia hatua wanaovunja utaratibu basi ni vigumu wawe na hoja ya nguvu kwa hili.

Pamoja na kwamba CHADEMA ni wazuri sana katika kujenga hoja na katika hotuba zao lakini natamani wana JF mjaribu kuweka maoni yenu hapa juu ya mambo ambayo ni muhimu wananchi wakayasikia siku ya Alhamisi. Lengo ni kujaribu kutafakari kwa pamoja kama kuna faida kwa maamuzi yaliyochukuliwa au la. Haya hapa chini ni maoni yangu kwani naamini hatua zilizochukuliwa ni sahihi kabisa.

1. Sababu ya kutokumtambua meya haikuwa ni kwa kukosa vyeo. Ilikuwa ni ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi na kutokuwapo kwa haki.

2. Pale ambapo madiwani waliokuwa wanapigania haki wanafuatwa na mtu au kikundi cha watu na baada ya hapo ghafla wanageuka na kubadilisha agenda toka kwenye ukiukwaji wa haki na kutokufuatwa kwa taratibu na sheria, na kuishia kuigeuza agenda hiyo kuwa agenda ya kugawana madaraka, basi mtu unaweza kuamini kuwa kuna nguvu nyuma ya jambo hilo. Na endapo chama bado kilijaribu kuwasaidia kujenga msingi wa kusimamia haki, bado chama kikageukwa basi ni rahisi watu kuamini kuwa kuna nguvu nyingine nyuma yao.

3.Chama makini hakiwezi kuruhusu wanachama wake wachukue hatua ambazo ni kinyume na misingi ya haki, demokrasia na ustawi wa utaratibu na sheria kama ilivyo imani ya chama chao, kisha wao wafuate maslahi binafsi au vyeo.

a)Hatuwezi kuwa kama wengine wanaosema watavua magamba na kila siku wanaendelea kuahirisha kwa hofu ya kuogopa matokeo yanayoweza kuletwa na maamuzi magumu.

b) Pale ambapo kwa sababu zisizoeleweka na kwa ghafla wanachama wanabadilisha msimamo basi kunakuwepo na mmomonyoko wa maadili

na hapo inabidi kuchukua hatua hata kama hatua hizo zitakigharimu chama kukosa nafasi ya udiwani, lakini tutakuwa tumejenga na kutetea haki hata kama ni kwa hasara yetu.

4. Endapo tutashindwa kuchukua hatua basi hatukuwa na haki ya kupiga kelele na kuwashangaa wale wanaoshindwa kuwachukulia hatua watuhumiwa wa ufisadi huku wakiahirisha kila siku. Hatuwezi kuruhusu Gamba kuota kwani tunajua magamba yakiota inakuwa vigumu kuja kuyavua kwani mengine yanaleta hofu ya kutoa damu yakishaachwa kwa muda mrefu.

5. Ujumbe tunaotaka uende kwa kila mtanzania ni kuwa CDM ni chama kinachosimamia na kutekeleza kwa vitendo misingi ya utawala bora na ufuatwaji wa haki , taratibu na sheria na maadili.

6. Mambo yanayofanywa kihuni na kwa ubabe hayapaswi kukubaliwa hata kama matokeo yake yana maslahi binafsi kwangu. Ni lazima tuangalie mbali na kusimamisha, kuenzi na kuheshimu utaratibu wa kisheria na kutimizwa kwa matakwa ya demokrasia.

7. Hatuwezi kuwa kama watu wengine ambao uongozi umewashinda, huku wakitoa matangazo ya kufukuza watu na bado wakipatwa na hofu kila wanapokutana wanaishia kuahirisha maamuzi magumu. Ni lazima chama makini kichukue maamuzi magumu kwa maslahi ya taifa na maslahi ya taifa kwa hili ni kuzuia ukiukwaji wa haki taratibu na misingi ya kidemokrasia katika chaguzi mbalimbali. Ni kuonyesha bayana kuwa heshima sio cheo cha kibinafsi au umaarufu bali ni heshima ni kutimizwa kwa matakwa ya demokrasia.

TUNAAMINI KUWA WANANCHI WALIOWACHAGUA WALIWACHAGUA ILI WAKADUMISHE DEMOKRASIA HAKI NA UTARATIBU WA SHERIA. WANANCHI WA ARUSHA WAKIWEMO VIONGOZI WA DINI WALIONA UHUNI NA UBABE ULIOFANYWA WAKATI WA UCHAGUZI WA MEYA NA UKIUKWAJI WA HAKI. WANANCHI WALIWACHAGUA VIONGOZI KWA KUKIAMINI CHAMA MAKINI KILICHOWATEUA, NI KWA MISINGI HIYO HIYO WANANCHI HUPOTEZA IMANI KWA CHAMA CHAO PALE AMBAPO WANAGUNDUA KUWA WALIOTUMWA WANAFANYA VIBAYA AU TOFAUTI NA MATAKWA YAO, NA KAMA NI KUWAONDOA NI HADI PALE WANAPOSUBIRI UCHAGUZI MWINGINE. HIVYO CHAMA KINAPOCHUKUA HATUA WANANCHI WAKITUMIA BUSARA YAO WATAONA WAMEPUNGUZIWA MZIGO WA KUNGOJA HADI UCHAGUZI MWINGINE WAKATI WALIOWATUMA WAMEGEUKA NA KUUNGA MKONO UKIUKWAJI WA TARATIBU, HAKI, DEMOKRASIA NA MISINGI YA SHERIA

NAOMBA KUWASILISHA ONGEZENI HAPA CHINI

Respect Mkuu. Thanks

nadhani mkuuu hapo khs uchaguzi utakaokuja tuwachie waakazi wa Arusha wafanye maamuzi yao. wacha jamaa waende mahakamani kama watahisi hawakutendewa haki. inatubidi tufike mahali UOGA NA HOFU usitunyime usingizi, CDM watakuwa tayari kupokea matokeo...., hilo linafahamika. mabadiliko ni ya lazima hapa nchini mwetu kipindi hiki!
Busara ya kawaida inakataa wazo la kwenda mahakamani kwa jambo kama hili na kwa namna mchakato mzima ulivyoenda kwa kuzingatia katiba ya chama chao. Ndio maana hata yule ambaye hakufika hukumu yake haikutolewa.

Mimi naona Godbless Lema ni mnafiki namba one ambapo kama kamati kuu ya Chadema ingekuwa makini walitakiwa wamfukuze Chama kabisa.

Kwani yeye ndio chanzo kikuu cha mgogoro huo kwani yeye pamoja na kuwa ni Mbunge lakini ni Sehemu ya baraza la madiwani waliofikia muafaka ule ambao chadema wameukana.
Na kama anasema yeye hajui lolote ila baraza la madiwani wa walifanya siri BASI HASTAHILI KUWA KIONGOZI WA WATU SABABU ILI MBUNGE AFANYA KAZI ZAKE VIZURI ANAHITAJI KUSHIRIKIANA NA MADIWANI WAKE. Kwa sababu hizo mbili alilazimika kufukuzwa kabisa ndani ya Chama. Kwani viongozi wanafiki ni khatari sana katika jamii.

Lakini maamuzi ya kamati kuu hayawezi hata siku moja kuweza kukidhi haja ya wakaazi wa Arusha kwani siku zote wananchi wanahitaji maendeleo na sio malumbano.

naamini wazi madiwani hao wakifikisha suala lao mahakamani kupinga kuenguliwa kwao ndani ya Chama na sababu zilizotumika kuwaondoa basi wana nafasi kubwa sana kushinda na kurejeshwa katika nafasi zao kama madiwani kwa Amri ya mahakama.

Na naamini kuwa kama uchaguzi utafanyika kuziba nafasi za madiwani hao. CCM watashinda viti vyote na hakuna kuwa na muafaka.

Nimewapenda sana msimamo ulioonyeshwa na madiwani hao katika kusimamia kile walichokusudia.

Chadema walishindwa kusoma alama za nyakati.

Kafungue kituo chako cha mfuta utuuzie, siasa hujui

Mtoa mada hana jipya. CHADEMA ni chama makini. Kinaamua bila kusubiri kupoteza muda. Wanatembea na Katiba, msingi wa maadili yao

Naona Gabachori umeamua Kudandia Mambo ya A Town,najua ni hofu tu pale watu kama akina Lema watapokuwa wanadhamana ya Kuongoza Jeshi La Polisi na Magereza, Unajua nini kitawapata Nyie Magabachori

Mimi naona Godbless Lema ni mnafiki namba one ambapo kama kamati kuu ya Chadema ingekuwa makini walitakiwa wamfukuze Chama kabisa.

Kwani yeye ndio chanzo kikuu cha mgogoro huo kwani yeye pamoja na kuwa ni Mbunge lakini ni Sehemu ya baraza la madiwani waliofikia muafaka ule ambao chadema wameukana.
Na kama anasema yeye hajui lolote ila baraza la madiwani wa walifanya siri BASI HASTAHILI KUWA KIONGOZI WA WATU SABABU ILI MBUNGE AFANYA KAZI ZAKE VIZURI ANAHITAJI KUSHIRIKIANA NA MADIWANI WAKE. Kwa sababu hizo mbili alilazimika kufukuzwa kabisa ndani ya Chama. Kwani viongozi wanafiki ni khatari sana katika jamii.

Lakini maamuzi ya kamati kuu hayawezi hata siku moja kuweza kukidhi haja ya wakaazi wa Arusha kwani siku zote wananchi wanahitaji maendeleo na sio malumbano.

naamini wazi madiwani hao wakifikisha suala lao mahakamani kupinga kuenguliwa kwao ndani ya Chama na sababu zilizotumika kuwaondoa basi wana nafasi kubwa sana kushinda na kurejeshwa katika nafasi zao kama madiwani kwa Amri ya mahakama.

Na naamini kuwa kama uchaguzi utafanyika kuziba nafasi za madiwani hao. CCM watashinda viti vyote na hakuna kuwa na muafaka.

Nimewapenda sana msimamo ulioonyeshwa na madiwani hao katika kusimamia kile walichokusudia.

Chadema walishindwa kusoma alama za nyakati.

Wameshindwa kusoma alama za nyakati zipi kwani maamuzi yaliyofanywa na CDM kuwafukuza wasaliti ndio kusoma kwenyewe alama za nyakati. Mikutano iliyofanywa jana haswa ule uliofanyika Tindigani jana umedhihirisha wazi kuwa wananchi wako tayari kumchagua mgombea mwingine wa udiwani baada ya Estomihi Mallah kufukuzwa. CCM isijaribu kujipa matumaini kwamba itanyakua badhi ya viti vya CDM huko ni kujidanganya kwani CDM bado inawanachama wengi mno na haijapoteza mvuto hapa Arusha.

Mtoa mada hana jipya. CHADEMA ni chama makini. Kinaamua bila kusubiri kupoteza muda. Wanatembea na Katiba, msingi wa maadili yao

Ni kweli ili chama chochote kilinde heshima yake kwa jamii lazima kiheshimu katiba yake na maadili yao. Ukikiuka maadili ya chama na kisha usijali ukiukwaji huo basi heshima yako haiwezi kubaki.

8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom