Hotuba ya viongozi wa CHADEMA huko Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hotuba ya viongozi wa CHADEMA huko Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtaka Haki, Aug 9, 2011.

 1. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pamoja na kwamba CHADEMA ni wazuri sana katika kujenga hoja na katika hotuba zao lakini natamani wana JF mjaribu kuweka maoni yenu hapa juu ya mambo ambayo ni muhimu wananchi wakayasikia siku ya Alhamisi. Lengo ni kujaribu kutafakari kwa pamoja kama kuna faida kwa maamuzi yaliyochukuliwa au la. Haya hapa chini ni maoni yangu kwani naamini hatua zilizochukuliwa ni sahihi kabisa.

  1. Sababu ya kutokumtambua meya haikuwa ni kwa kukosa vyeo. Ilikuwa ni ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi na kutokuwapo kwa haki.

  2. Pale ambapo madiwani waliokuwa wanapigania haki wanafuatwa na mtu au kikundi cha watu na baada ya hapo ghafla wanageuka na kubadilisha agenda toka kwenye ukiukwaji wa haki na kutokufuatwa kwa taratibu na sheria, na kuishia kuigeuza agenda hiyo kuwa agenda ya kugawana madaraka, basi mtu unaweza kuamini kuwa kuna nguvu nyuma ya jambo hilo. Na endapo chama bado kilijaribu kuwasaidia kujenga msingi wa kusimamia haki, bado chama kikageukwa basi ni rahisi watu kuamini kuwa kuna nguvu nyingine nyuma yao.

  3.Chama makini hakiwezi kuruhusu wanachama wake wachukue hatua ambazo ni kinyume na misingi ya haki, demokrasia na ustawi wa utaratibu na sheria kama ilivyo imani ya chama chao, kisha wao wafuate maslahi binafsi au vyeo.

  a)Hatuwezi kuwa kama wengine wanaosema watavua magamba na kila siku wanaendelea kuahirisha kwa hofu ya kuogopa matokeo yanayoweza kuletwa na maamuzi magumu.

  b) Pale ambapo kwa sababu zisizoeleweka na kwa ghafla wanachama wanabadilisha msimamo basi kunakuwepo na mmomonyoko wa maadili
  na hapo inabidi kuchukua hatua hata kama hatua hizo zitakigharimu chama kukosa nafasi ya udiwani, lakini tutakuwa tumejenga na kutetea haki hata kama ni kwa hasara yetu.

  4. Endapo tutashindwa kuchukua hatua basi hatukuwa na haki ya kupiga kelele na kuwashangaa wale wanaoshindwa kuwachukulia hatua watuhumiwa wa ufisadi huku wakiahirisha kila siku. Hatuwezi kuruhusu Gamba kuota kwani tunajua magamba yakiota inakuwa vigumu kuja kuyavua kwani mengine yanaleta hofu ya kutoa damu yakishaachwa kwa muda mrefu.

  5. Ujumbe tunaotaka uende kwa kila mtanzania ni kuwa CDM ni chama kinachosimamia na kutekeleza kwa vitendo misingi ya utawala bora na ufuatwaji wa haki , taratibu na sheria na maadili.

  6. Mambo yanayofanywa kihuni na kwa ubabe hayapaswi kukubaliwa hata kama matokeo yake yana maslahi binafsi kwangu. Ni lazima tuangalie mbali na kusimamisha, kuenzi na kuheshimu utaratibu wa kisheria na kutimizwa kwa matakwa ya demokrasia.

  7. Hatuwezi kuwa kama watu wengine ambao uongozi umewashinda, huku wakitoa matangazo ya kufukuza watu na bado wakipatwa na hofu kila wanapokutana wanaishia kuahirisha maamuzi magumu. Ni lazima chama makini kichukue maamuzi magumu kwa maslahi ya taifa na maslahi ya taifa kwa hili ni kuzuia ukiukwaji wa haki taratibu na misingi ya kidemokrasia katika chaguzi mbalimbali. Ni kuonyesha bayana kuwa heshima sio cheo cha kibinafsi au umaarufu bali ni heshima ni kutimizwa kwa matakwa ya demokrasia.

  TUNAAMINI KUWA WANANCHI WALIOWACHAGUA WALIWACHAGUA ILI WAKADUMISHE DEMOKRASIA HAKI NA UTARATIBU WA SHERIA. WANANCHI WA ARUSHA WAKIWEMO VIONGOZI WA DINI WALIONA UHUNI NA UBABE ULIOFANYWA WAKATI WA UCHAGUZI WA MEYA NA UKIUKWAJI WA HAKI. WANANCHI WALIWACHAGUA VIONGOZI KWA KUKIAMINI CHAMA MAKINI KILICHOWATEUA, NI KWA MISINGI HIYO HIYO WANANCHI HUPOTEZA IMANI KWA CHAMA CHAO PALE AMBAPO WANAGUNDUA KUWA WALIOTUMWA WANAFANYA VIBAYA AU TOFAUTI NA MATAKWA YAO, NA KAMA NI KUWAONDOA NI HADI PALE WANAPOSUBIRI UCHAGUZI MWINGINE. HIVYO CHAMA KINAPOCHUKUA HATUA WANANCHI WAKITUMIA BUSARA YAO WATAONA WAMEPUNGUZIWA MZIGO WA KUNGOJA HADI UCHAGUZI MWINGINE WAKATI WALIOWATUMA WAMEGEUKA NA KUUNGA MKONO UKIUKWAJI WA TARATIBU, HAKI, DEMOKRASIA NA MISINGI YA SHERIA

  NAOMBA KUWASILISHA ONGEZENI HAPA CHINI
   
 2. m

  miradibubu JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 313
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  ninaamini watayazingatia maoni yako mkuu kwani ni muhimu watu kuwa na kimuhemuhe na chama chake
   
 3. D

  Derimto JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu hii hotuba inayobeba ujumbe wa Arusha hasa hongera sana na ninawashauri viongozi wa Chadema kuichukua na kuifanyia baadhi ya marekebisho ambayo wao watayaona yanawafaa lakini hii siyo ya kuiacha imejaa ujumbe unaoeleweka
   
 4. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #4
  Aug 9, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,203
  Likes Received: 3,765
  Trophy Points: 280
  Nimeipenda naamini viongozi wangu wataitumia!
   
 5. b

  bashiru issa New Member

  #5
  Aug 9, 2011
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu Hii ndio Tz tunataka ierekee NA kikubwa NA kibaya ni pale gamba likiota kipind cha kulitoa hutoka NA damu
   
 6. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mimi naona Godbless Lema ni mnafiki namba one ambapo kama kamati kuu ya Chadema ingekuwa makini walitakiwa wamfukuze Chama kabisa.

  Kwani yeye ndio chanzo kikuu cha mgogoro huo kwani yeye pamoja na kuwa ni Mbunge lakini ni Sehemu ya baraza la madiwani waliofikia muafaka ule ambao chadema wameukana.
  Na kama anasema yeye hajui lolote ila baraza la madiwani wa walifanya siri BASI HASTAHILI KUWA KIONGOZI WA WATU SABABU ILI MBUNGE AFANYA KAZI ZAKE VIZURI ANAHITAJI KUSHIRIKIANA NA MADIWANI WAKE. Kwa sababu hizo mbili alilazimika kufukuzwa kabisa ndani ya Chama. Kwani viongozi wanafiki ni khatari sana katika jamii.

  Lakini maamuzi ya kamati kuu hayawezi hata siku moja kuweza kukidhi haja ya wakaazi wa Arusha kwani siku zote wananchi wanahitaji maendeleo na sio malumbano.

  naamini wazi madiwani hao wakifikisha suala lao mahakamani kupinga kuenguliwa kwao ndani ya Chama na sababu zilizotumika kuwaondoa basi wana nafasi kubwa sana kushinda na kurejeshwa katika nafasi zao kama madiwani kwa Amri ya mahakama.

  Na naamini kuwa kama uchaguzi utafanyika kuziba nafasi za madiwani hao. CCM watashinda viti vyote na hakuna kuwa na muafaka.

  Nimewapenda sana msimamo ulioonyeshwa na madiwani hao katika kusimamia kile walichokusudia.

  Chadema walishindwa kusoma alama za nyakati.
   
 7. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Hii ni ajabu kabisa.

  yaani unafundishwa namna ya kuwapooza wananchi wa Arusha.

  Hotba safi ni ile inayoangalia yaliojiri na maamuzi yenu je yanasaidia nini katika maendeleo ya jamii ile, na je yamejenga amani na utulivu?
  lakini kikubwa na kukonga nyoyo za wananchi wengi waliowachagua.

  Je mnaona kama uchaguzi utafanyika katika kata husika, mna nafasi hata ya kupata kiti kimoja.

  Siku zote kiongozi hatungiwi hotba bali anazungumza kutokana na matokio.

  kazi ipo kwa Chadema kuleta hotba za kuleta amani na kujenga mshikamano husisan pale mlopoharibu.
   
 8. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Ungekuwa unatimiza nguzo ya kislamu ya kufunga usingekuwa na mawazo haya, mwislam swafi hana mawazo kama ya kwako, jitazame upya na ujirekebishe, yaani wewe unashabikia amani wakati watu wanamiliki trilion 3 nje ya nchi na ilhali hospitali zetu zipo hai, mashule balaa na nk, wewe bado unaona tunaamani, umeyaona mambo ya UDa, Jairo na mengine mengi tu wewe bado unahubiri amani!? kweli wewe kijana wewe mrudie mola wako akupe hekma.
   
 9. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Haina kitu zaidi ya porojo !
   
 10. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #10
  Aug 9, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0  Ndugu Baru baru,siri BASI HASTAHILI KUWA KIONGOZI WA WATU SABABU ILI MBUNGE AFANYA KAZI ZAKE VIZURI ANAHITAJI KUSHIRIKIANA NA MADIWANI WAKE
  Hii si kweli,
  Hivi, kama madiwani wote hawakushirikiana na Mbunge au wakitofautiana na Mbunge na kama ktk tofauti hiyo madiwani wamevunja kanuni na katiba ya Chadema na kama Mbunge Lema yuko sahihi pmoja na kuwa yuko peke yake nani anapaswa kuitwa mnafiki?

  Je, wingi (Madiwani wote) Vs Mbunge Moja huwa unabaidilisha ukweli? Kwamba madiwani wote wako upande moja lazima wawe sahihi? Hapa naomba nikuhakikishie tu kwamba Godbless Lema yuko sahihi kwa mujibu wa taratibu za chama.
  Pili, madiwani watano kati ya 11 ndo waliotimuliwa kwa hiyo. Lema yuko pamoja na zaidi ya Nusu ya madiwani waliotii amri ya kamati kuu ambayo G. Lema ni mjumbe. period

  wananchi wanahitaji maendeleo na sio malumbano.

  Hapa nani analeta malumbano.
  Mosi, Nani aliyevunja kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa wakati wa uchaguzi wa mmea wa Arusha ambayo ndo imeleta yote haya?
  pili, Ni nani aliyekwenda kudanganya wabunge kuhusu uchaguzi wa mmea wa Arusha na Maandamano ya Arusha kati ya Chadema ( Lema ) na CCM (Pinda )wakati akija swali la Mbowe?
  Tatu, Nani sasa aibu yake imewekwa kapuni na Speaker Anna Makinda kati ya Chadema na CCM?

  kurejeshwa katika nafasi zao kama madiwani kwa Amri ya mahakama.

  Mosi, according to our current weak constitution hilo haliwezekani. Hili lilitokana na woga wa CCM kuogopa mgombea binafsi. wamejinasa wenyewe ktk mtego waliotega wenyewe.
  Pili, Kama CCM itafanya chochote wawezalo makamani na kuwarudisha hawa madiwani madarakani that has nothing to do with uamuzi wa KAMATI KUU YA CHADEMA. WanaArusha na watanzania watakuwa wameshajua Chadema inasimamia nini na madiwani hao wamesimamia nini ktk sakata la Arusha? That is enough. But I doubt if the court can judge that way.

  CCM watashinda viti vyote na hakuna kuwa na muafaka

  Sasa ndugu yangu hili la imani yako kuwa CCM itashinda hatuwezi kulijadili sana. Imani haijadiliki ila nina maswali mawili.
  Mosi, kwanini hawa wana ccm haikuchaguliwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010?
  Pili, umeshaongea na wapiga kura wangapi ktk kata hizo nne mpaka ukawa na imani kwamba mtashinda kata zote?

  Nimewapenda sana msimamo ulioonyeshwa na madiwani hao katika kusimamia kile walichokusudia.
  Chadema walishindwa kusoma alama za nyakati
  .

  Ni kweli wamesimama kidete kutetea hicho walichokusudia yaani ( Vyeo vya unaibu mmea na wenyeviti wa kamati) Bahati mbaya msimamo wao umekwenda kinyume na katiba na kanuni za Chadema. Hawakupaswa kufanya hivyo ( kuomba vyeo kupitia mwafaka) bila ridhaa ya viongozi wa Arusha wa Chadema na kamati kuu.
  Huo ndio ukweli mkuu.
   
 11. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  kama ana akili timamu atakuwa amekuelewa.
   
 12. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapa sio mtu anafundishwa hotuba bali tunajaribu kuona ukweli ulioko katika hatua mahsusi zilizochukuliwa na viongozi wa CDM. Je huoni ujumbe unaeleweka kwa wale wanaotakiwa kuvuliwa magamba kwamba wangechukuliwa hatua mapema hali isingefikia hapa iolipo leo. Ndio maana watu wanathubutu kutoa masaa 24 kwa serikali isalimu amri yao.
   
 13. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #13
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nashukuru mkuu sijaelewa "kimuhemuhe" labda kiswahili kinanipiga chenga
   
 14. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #14
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
   
 15. T

  Think Tank JF-Expert Member

  #15
  Aug 9, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 234
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  'By overcoming your fear you prove your worth'.To make clear i mean 'making decisions'
   
 16. Izack Mwanahapa

  Izack Mwanahapa JF-Expert Member

  #16
  Aug 9, 2011
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 497
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Hongera sana Mtaka Haki, pointi ulizoeleza ni za msingi sana, watu wa Arusha walikuwa tayari kufa kwa ajili ya haki si viongozi wachache kugawana madaraka. Chadema imechukua hatua nzuri na ngumu sana, ifike wakati chama (Taasisi) kiwe/ iwe na nguvu kuliko watu bibafsi na maslahi yao. Hongera sana kwa uzalendo wako, Mungu akuzidishie.
   
 17. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #17
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yes Actually FEAR means False/fake Evidence Appearing Real that means you think that you are sure that something will happen but its actually fake.
   
 18. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #18
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Thanks
   
 19. Izack Mwanahapa

  Izack Mwanahapa JF-Expert Member

  #19
  Aug 9, 2011
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 497
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  123456
   
 20. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #20
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Actually FEAR means: False/fake Evidence Appearing Real that means you think that you are sure that something will happen but its actually fake.
   
Loading...