Hotuba ya Rais Kikwete kuuaga mwaka 2011

Hotuba ya Rais Kikwete kuuaga mwaka 2011

Tatizo ninaloliona ni kwamba Rais anatumia muda mwingi kutoa review ya mambo ya nyuma ambayo yanafaamika na kuacha kutueleza tutajikwamuaje kwenye huu umaskini unaotokana na ufisadi na maamuzi na matumizi mabaya ya rasilimali zetu. Haina logic kuelezea hatua za kulima hata mtoto wa miaka sita anajua ya nini sasa itumie muda wa rais kuelezea?Ni wazi tutapata katiba mbovu kutokana na rais kusisitiza ile adhabu ya miaka5& mil5. Inasikitisha kwa kweli, MUNGU tusaidie waja wako.
 
Yes tatizo ni Priority . Katika Dunia tuliyopo na matukiyo yaliyotokea alitakiwa kutaja
  • TEKNOHAMA
  • UUZAJI WA WANYAPORI NJE
  • POSHO ZA WABUNGE
Kwangu haya ni muhimu kuliko hata habari za maharamia wa Kisomali

Well kwangu mimi hayo uliyoyasema siyo muhimu sana zaidi ya kutoa maelekezo ya ki-ofisi

mimi nipenda alipoongelea kwamba
a. Nchi itapata katiba mpya natamani wafanye kweli maana kuna watu wengi sana hawataki katiba hasa wanaccm
b. Alipoongelea uwekezaji wa ndani ili wananchi wachangamkie fursa zilizopo serikalini kupata mitaji ya miradi ya maendeleo etc..

Lakini pengine alichosahau ni kwamba:

a. Public services ni mbaya sana hasa kutokana na urasimu unaowekwa na maofisa wa serikalini,
b. Umoja wa kitaifa unaochokonolewa kila mara na matamko/ waraka wa viongozi wa kiislam na kikristo
 
Uhalisia upi? mkuu

Mimi nina ndugu zangu kibao wamepata division two; shule za kata to be specific kutoka Dodoma (kondoa); wanaenda chuo mimi nazipenda sana hizi shule za kata; japo sipingi kwamba zinatakiwa kuboreshwa zaidi lol

Never loose hope; kujipanga ni kila siku katika maisha
kwahiyo ndugu zako wakifaulu huku 82% ya watahiniwa wamefeli wewe inakupendeza haya ???????????
Nijuavyo kila project inaplan yake ya kuanza mradi na kuona matunda yake sas hii plan gani unaanza vyote kwa pamoja ilihali event moja huitegemea nyingine ikamilike ili nayo ifikiwe.
Huna maabara maktaba nyumba za walimu unadarasa moja then unachukua wanafunzi mikondo minne!!!!! Haingii akilini
what a planner!!!!!!!?
 
Very subjective mkuu, taarifa ambazo wewe unaona ni muhimu au siyo muhimu watu wengi wanaona ni muhimu au siyo muhimu..ndio maana uko huru kufikiri kipi ulitegemea kiwe taarifa kwako kwasababu wewe unashida employment isssues

Kuhusu statistics nafikiri ni kazi ya mtafiti kutafuta taarifa siyo kwenye website tu hadi kwenye source kwenyewe ..

Ni kweli taifa halijaweza ku-computurize kila kitu..ni gharama vilevile; je ni priority kwa sasa
Hivi unajuwa maana ya statistics mkuu?

Kwanini website iwe National Bureau of statistics halafu uniambie niende wizarani?

Halafu unageuka sasa na kusema ni gharama, really?

Na posho mnawang'an'anizia wabunge kila kukicha?

Only in banana republic!
 
Where is "Kilimo kwanza"?. Naona haijaongelewa kabisa. Au utekelezaji wake ndo ushamalizika?.

What about our International relations?. Mbona hatuna kitu cha kusimamia kama taifa?.
Nilitegemea kusikia mengi katika eneo hili!!!!!!!!!
 
kwahiyo ndugu zako wakifaulu huku 82% ya watahiniwa wamefeli wewe inakupendeza haya ???????????
Nijuavyo kila project inaplan yake ya kuanza mradi na kuona matunda yake sas hii plan gani unaanza vyote kwa pamoja ilihali event moja huitegemea nyingine ikamilike ili nayo ifikiwe.
Huna maabara maktaba nyumba za walimu unadarasa moja then unachukua wanafunzi mikondo minne!!!!! Haingii akilini
what a planner!!!!!!!?

Hata yule mgunduzi wa trekta alipoisha mara ya kwanza ilikuwa inaenda nyuma (reverse) aka-improve kukawa na trekta unayoiona sasa..

Hata kama angefaulu mtu moja tu Tanzania nzima; ningeona wamefanya jambo la maana; ispokuwa ningewashauri waongeze bidii kuweka walimu, maabara, etc..

Changamoto zipo tupambane nazo kama taifa..period; shule za kata ni muhimu sana kwa wananchi wasio na uwezo vijijini tuendelee kuziboresha au siyo??
 
Hivi unajuwa maana ya statistics mkuu?

Kwanini website iwe National Bureau of statistics halafu uniambie niende wizarani?

Halafu unageuka sasa na kusema ni gharama, really?

Na posho mnawang'an'anizia wabunge kila kukicha?

Only in banana republic!

haya wewe ni mtafiti wa aina gani?? unategemea website pekee..pole sana

Tuma (research assistants wakusaidie mkuu) acha ubakhili kaka
 
Where is "Kilimo kwanza"?. Naona haijaongelewa kabisa. Au utekelezaji wake ndo ushamalizika?. What about our International relations?. Mbona hatuna kitu cha kusimamia kama taifa?. Nilitegemea kusikia mengi katika eneo hili!!!!!!!!!
Unafikiri hotuba inaweza kugusa kila pande unayoifikiri. Swala la msingi ni kwamba hotuba imegusa eneo kbwa.
 
Where is "Kilimo kwanza"?. Naona haijaongelewa kabisa. Au utekelezaji wake ndo ushamalizika?.

What about our International relations?. Mbona hatuna kitu cha kusimamia kama taifa?.
Nilitegemea kusikia mengi katika eneo hili!!!!!!!!!

Niliandika mimi hapa jukwaani mara baada ya kutangazwa kilimo kwanza kwamba Kilimo kwanza ni usanii mwingine wa Kikwete na Magamba katika kubadilisha somo ambalo lilikuwa limeshamiri wakati ule la kushindwa kupambana na mafisadi, sasa niliyoyaandika yamekuwa kweli. Hakuna kilimo kwanza wala kilimo pili ni usanii tu wa hali ya juu unaoendelea.
 
haya wewe ni mtafiti wa aina gani?? unategemea website pekee..pole sana

Tuma (research assistants wakusaidie mkuu) acha ubakhili kaka
Si kwamba naitegemea, nitegemee kitu gani toka serikali yenye ukiritimba? Issue nyeti si mnapeana wenyewe kwa wenyewe? Weka hayo makampuni yaliyopewa hizo billions kama ni pesa za wananchi, hivyo vyama vya ushirika, kuna data za kuonyesha ni kweli hayo yanayotoka kinywani mwa rais ama ni kumwamini tu kama yeye ni Mungu? Unaleta porojo ukiulizwa unasema nifwatilie?

Issue ni kudai eti hii ni "National Bureau of Statistics" na huku hakuna statics ndani zaidi ya statemement za porojo zenye maana ya ku analyze statistics za mwaka 2006 na 2011.

Really?Acheni bana!
 
Unafikiri hotuba inaweza kugusa kila pande unayoifikiri. Swala la msingi ni kwamba hotuba imegusa eneo kbwa.

Swala sio kugusa eneo kubwa. swala ni kugusa maeneo yenye tija na yenye kuonyesha mikakati ya kumkomboa mtanzania aondokane na haya maisha magumu!!!
 
Niliandika mimi hapa jukwaani mara baada ya kutangazwa kilimo kwanza kwamba Kilimo kwanza ni usanii mwingine wa Kikwete na Magamba katika kubadilisha somo ambalo lilikuwa limeshamiri wakati ule la kushindwa kupambana na mafisadi, sasa niliyoyaandika yamekuwa kweli. Hakuna kilimo kwanza wala kilimo pili ni usanii tu wa hali ya juu unaoendelea.

Salute kwako mkuu,
Mimi pia sikuamini kama ulikuwa mkakati wa dhati wa kuinua kilimo ndio maana nimekuwa nikiufuatilia sana. And now it turns out that my hypothesis is proved right. No more Kilimo first, a way to forget it is purposely being created!!!
 
Niliandika mimi hapa jukwaani mara baada ya kutangazwa kilimo kwanza kwamba Kilimo kwanza ni usanii mwingine wa Kikwete na Magamba katika kubadilisha somo ambalo lilikuwa limeshamiri wakati ule la kushindwa kupambana na mafisadi, sasa niliyoyaandika yamekuwa kweli. Hakuna kilimo kwanza wala kilimo pili ni usanii tu wa hali ya juu unaoendelea.
Mimi quntititive figure kama hizi za Politician huwa siziamini , wakifanya 5 vizuri wakaharibu 95 kati ya yaliyohalibika 90 ni uzembe na 5 yalikuwa nje ya uwezo wao . Wataripoti wamefanikiwa 5 wameshindwa 5 na yalikuwa nje ya uwezo wao . Yale 90 hayatazungumzwa kamwe labda yasemwe na na wapinzani wao

Mfano
Kikwazo kikubwa cha maendeleo yetu ni RUshwa ktk mikataba mikubwa ya umma , JK hawezi lisema ipasavyo.

Mfumuko wa bei , kila siku wanasema ni < 9% lakini kwa kipindi cha miaka 5 iliyopita vitu karibu vyote vimepanda 3 times
 
Topical said:
Well kwangu mimi hayo uliyoyasema siyo muhimu sana zaidi ya kutoa maelekezo ya ki-ofisi

Lakini pengine alichosahau ni kwamba:

a. Public services ni mbaya sana hasa kutokana na urasimu unaowekwa na maofisa wa serikalini-
Nilposema Kasahau TEKNOHAMA kama ungenielewa basi ungegundua Ni jambo hili hili la Public service nililolenga. tatizo watu wengi waikiwemo na washauri wa RAis na a taasisi wao teknohama ni kuanzisha tovuti tu. Ndio maana kuna haja ya kuwa na viongozi kuelewa hasa Concept ya TEKNHOMA pamoja fusra na michango unaotolewa na TEKNOHAMA kwenye kuboresha hudma za jamii..

So wewe unaona hajaongelea Public service amabyo kwako Ni muhimu. Mimi naona hajaongelea TEKNOHAMA amabyo ni inatakiwa kutumika kuboresha Public service

Kwa hiyo kumbe kuna mambo tunakubalina ila kwa lugha tofauti. Ningeweza kukupa mifano kivipi teknohama inaweza kusaidia kuondoa kero za huduma za jamii zinazolega lega kwenye tasisi mbali mbali mbali kuanaizia kwenye ELIMU, POLISI, UTALII, AFYA etc lakini tuache.

BTN
Heri ya 2012
 
Si kwamba naitegemea, nitegemee kitu gani toka serikali yenye ukiritimba? Issue nyeti si mnapeana wenyewe kwa wenyewe? Weka hayo makampuni yaliyopewa hizo billions kama ni pesa za wananchi, hivyo vyama vya ushirika, kuna data za kuonyesha ni kweli hayo yanayotoka kinywani mwa rais ama ni kumwamini tu kama yeye ni Mungu? Unaleta porojo ukiulizwa unasema nifwatilie?

Issue ni kudai eti hii ni "National Bureau of Statistics" na huku hakuna statics ndani zaidi ya statemement za porojo zenye maana ya ku analyze statistics za mwaka 2006 na 2011.

Really?Acheni bana!

Sasa naona unataka kufanya research ndani ya JF nikupe na makampuni yaliyopewa mabilions ha ha kweli wewe mtafiti..

Nitakusaidia ili kujua wapi waweza kupata makampuni yaliyopta hizo pesa nenda NMB, CRDB na EXIM ndipo fedha zilipopita na projects zilizofund through vikundi na saccos mbalimbali..
 
Si unaona unapopata shida hata kuelezea kidogo tu?

Hivi unadhani kwenye nchi ya wananchi waelewa unaweza kutumia pesa ya umma bila maelezo yenye details za kutosha?

Kwenda huko ulikosema ni kwenda kuangalia kama ni kweli ama sivyo, lakini kampuni ama shirika linalopewa pesa za umma kuna shida gani kutoa majina yake? Mbona tunajuwa Obama aliwapa GM pesa za umma na ni kiasi gani bila ya kwenda benki?

Makampuni si yalikuwa machache tu? Ama una confuse na saccos ambayo iko chini ya "wajasiriamali wadogo"? Unakumbuka swali nililokuuliza mkuu?

Ok na hayo mashirika yaliwekeza kwenye nini? ni kiasi gani cha export kiko associated na project hiyo? Ama hata projection?

Ndo maana hotuba imekaa hivyo, hakuna cha kuelezea in reality.
 
Back
Top Bottom