Hotuba ya Rais Kikwete kuuaga mwaka 2011

Mwenye shamba aliingia mikataba mibovu na wazungu. Harafu alishawamilikisha hilo shamba kwa miaka 99 (Kakola...). Mwenye shamba alidhani waliomtuma ni wajinga hawatakuja kugundua, wengine aliwaua ili kuficha ushahidi, ila mpaka sasa waliomtuma wameshachoka na wanadai shamba liuzwe upya tena. Kwa pamoja tunaweza kuudha shamba letu upya tena!!!
 
Inawezekana wewe ni intellectual..unayeona mfano uliotolewa haufai.....lakini mwananchi wa kawaida wa Mpanda, Kishapu, Geita,Iramba, Itigi n.k atauelewa......audience ya hotuba hii ni watanzania wote milioni 40....wasomi, wasio wasomi, waliopo mjini, na vijijini pamoja na wale wanaokula bata ughaibuni......hivyo yawezekana yapo baadhi ya mambo haya appeal kwako, yana appeal kwa mwingine....balancing act aliyofanya Mhe tumpe credit tu badala ya kulaumu.

Wewe toa real analysis ni kitu gani amechemsha kuliko kutoa sweeping statments za kulaani bila hoja. Kwani ni uwongo uwekezaji hauhitaji resources? anachozungumzia pale ni manpower(labour),capital, infrastructure etc

Wewe ndo hewa kabsa! Resources hakuna? Mbona zimejaa,watu,madini,mbuga za wanyama n.k.Kinachokosekana hapa ni UONGOZI BORA NA SIASA SAFI! Acha kuandika upupu!
 
Je, umejiandaa kupata katiba mpya! Tafakari kwa makini.

Mchakato wa Katiba

Ndugu Wananchi;

Tukio lingine la kihistoria lililotokea mwaka huu tunaoumaliza leo ni kuanza kwa mchakato wa kupata Katiba mpya ya nchi yetu. Kama mnavyokumbuka, katika hotuba yangu ya kuuaga mwaka 2010 na kuukaribisha mwaka 2011, niliahidi kwamba tutaanzisha mchakato wa kuitazama upya Katiba ya nchi yetu kwa lengo la kuihuisha, ili hatimaye tuwe na Katiba inayoendana na taifa lenye umri wa nusu karne. Azma yetu ni kuwa tusherehekee miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tukiwa na Katiba mpya itakayotumika kwenye Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2015.
Soma na hapa, hadithi imeandaliwa barabara kabisa kwa chakula cha masikio.
Naye Dk. Benson Bana, Mwenyekiti Mwenza wa REDET alisema; "Ni lazima Katiba Mpya ichukue karibia asilimia 80 ya Katiba ya sasa. Kwa maana hiyo, si kuandika Katiba Mpya bali ni kufanya marekebisho ya Katiba iliyopo sasa."

source: Raia Mwema | Tanzania tuko njia panda au tumechanganyikiwa?
 
negative mind always suspecious

Naaw mkuu, mimi nakubaliana na ile falsafa ya "trust but verify"


Mkuu ulitegemea rais aje nyumbani kukupa taarifa za fursa mbalimbali kwa wawekezaji na uwekezaji nchini?

Kama wewe unafanya politics or poli-tricks kwenye kila jambo huwezi kutafuta hizo fursa utaishia kulaumu serikali kama wafanyavyo upinzani; forgeting that hao jamaa wanaishi kwa kuikosoa serikali

If you are interested with investments in different areas in Tanzania; facilities or schemes are in place

Walio na interest wanazitumia na wame invest tayari..(wametumia rasilima za nchi)
Kama tunapata taarifa nyinginezo ambazo hata hazina msingi kwanini tusipate taarifa kama hizo?

Hayo ya statistics yenyewe umeniambia hadi niende wizarani.
 
NINGEPENDA KUSIKIA NA KUONA JK ANAGUSIA MAMBO HAYA

UUZAJI WA WANYAMAPORI NA MALIASILI NJE YA NCHI

  • Kustopisha kabisa kuuza wanyama pori hai nje ya nchi.....
  • Kupeleka muswada kwa nchi za afrka mashariki na hata umoja wa afrika nao kuachana na jambo hilo
  • Kama kuna ulazima badala ya Kuuza wanyama basi tuwakodishe Maana sasa hivi ni kama tunahujuu utalii wetu wenyewe na hata hiyo bei yenyewe ni ndogo mno.
TEKNHOHAMA KATIKA MAENDELEO,UWAJIBIKAJI NA UPASHANAJI HABARI
  • Shule hazina maabara na vifaa lakini teknohaam inawezesha kila shule hasa zile za mjini ziwe na VISUAL LAB.
  • Tasisis kama Polisi,Takukuru hazijatumia fursa ya ICT kuwa karibu na UMMA. Wengi wanaimbilia kuazisha Tovuti tu lakini tovuti za ahzitumi kupokea taarifa au kutoa taarifa zile zinazotakiwa kwa jamii . Mfano hii ni Twiiter ya Police ya UK. . Tanzania tasisi nyingi mamboya ICT ni siasa tu hata tovuti ya shirikakama TBC ni aibu
  • etc

NAFASI NA MCHANGO WA MICHEZO NA MATARIJIO YA LONDON 2012
grrrrrrrr

Kuna wizara zina husika na hayo mambo unaweza kupata mwelekeo wao kwa miaka ijayo; rais anaongelea issues zinazogusa, zilizogusa au zitakazogusa jamii nzima
 
Je, umejiandaa kupata katiba mpya! Tafakari kwa makini.

Mchakato wa Katiba

Ndugu Wananchi;

Tukio lingine la kihistoria lililotokea mwaka huu tunaoumaliza leo ni kuanza kwa mchakato wa kupata Katiba mpya ya nchi yetu. Kama mnavyokumbuka, katika hotuba yangu ya kuuaga mwaka 2010 na kuukaribisha mwaka 2011, niliahidi kwamba tutaanzisha mchakato wa kuitazama upya Katiba ya nchi yetu kwa lengo la kuihuisha, ili hatimaye tuwe na Katiba inayoendana na taifa lenye umri wa nusu karne. Azma yetu ni kuwa tusherehekee miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tukiwa na Katiba mpya itakayotumika kwenye Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2015.


Soma na hapa, hadithi imeandaliwa barabara kabisa kwa chakula cha masikio.


Naye Dk. Benson Bana, Mwenyekiti Mwenza wa REDET alisema; "Ni lazima Katiba Mpya ichukue karibia asilimia 80 ya Katiba ya sasa. Kwa maana hiyo, si kuandika Katiba Mpya bali ni kufanya marekebisho ya Katiba iliyopo sasa." => source: bofya hapa: Raia Mwema | Tanzania tuko njia panda au tumechanganyikiwa?

Eti katiba ita "Huishwa" kwani ilikuwa mfu?

Watu wanataka katiba mpya yeye anatuletea kiswahili sijui ya wapi?
 
Naaw mkuu, mimi nakubaliana na ile falsafa ya "trust but verify"



Kama tunapata taarifa nyinginezo ambazo hata hazina msingi kwanini tusipate taarifa kama hizo?

Hayo ya statistics yenyewe umeniambia hadi niende wizarani.

Very subjective mkuu, taarifa ambazo wewe unaona ni muhimu au siyo muhimu watu wengi wanaona ni muhimu au siyo muhimu..ndio maana uko huru kufikiri kipi ulitegemea kiwe taarifa kwako kwasababu wewe unashida employment isssues

Kuhusu statistics nafikiri ni kazi ya mtafiti kutafuta taarifa siyo kwenye website tu hadi kwenye source kwenyewe ..

Ni kweli taifa halijaweza ku-computurize kila kitu..ni gharama vilevile; je ni priority kwa sasa
 
Hakika tumepata mafanikio makubwa sana katika miaka 50 hii ya Uhuru wetu kuliko yale yaliyopatikana katika miaka 77 ya ukoloni wa Wajerumani (miaka 34) na Waingereza (miaka 43). Pamoja na mafanikio hayo tuliyoyapata bado nchi yetu ni miongoni mwa nchi maskini sana duniani hivyo bado tunayo kazi kubwa sana ya kufanya mbele yetu.
Tumepata mafanikio makubwa sana lakini bado ni miongoni mwa nchi masikini sana duniani. Sielewi kabisa hapa wataalamu nielewesheni kwenye hili
 
Eti katiba ita "Huishwa" kwani ilikuwa mfu?

Watu wanataka katiba mpya yeye anatuletea kiswahili sijui ya wapi?

Hata lugha sasa ni source of criticism?

Kweli nyie hakuna hoja; ngoja nisubiri hoja nijibu vinginevyo niwe msomaji
 
Luhanjo kastaafu, vipi hawajibishwi??

Tehe tehe, yeye si wa kwanza ktk serikali hii kustaafu kabla ya kuwajibishwa! Wimbo umepata waibaji kwa nini usiimbwe! Kama angelisubiriwa awajibishwe kabla ya kustaafu, hasingelipwa posho zake! tihi tihiiii
 
Tumepata mafanikio makubwa sana lakini bado ni miongoni mwa nchi masikini sana duniani. Sielewi kabisa hapa wataalamu nielewesheni kwenye hili

Ukilinganisha na miaka 70 ya ukoloni na miaka 50 ya uhuru; tumefanikiwa sana..je siyo kweli?
 
Daah! hivi ndugu hii makitu (Hotuba ya kila mwezi ya raisi) ina faida gani kwa nchi yetu?,kuletewa tathmini na takwimu za kupikwa kila mwisho wa mwezi wakati kunywa chai Tanzania imeshakuwa jambo la anasa,kwa nini tusiwe na National Dialogue on selected issues hata kama ni mara moja kwa mwaka then yeye apate kitu cha kuaddress watu ambacho kitakuwa ni genuine!...kwa hali hii kufika huko kwenye nchi ya Ahadi kwa Sisi Wadanyika acha tuendelee kuota!
 
Kuna wizara zina husika na hayo mambo unaweza kupata mwelekeo wao kwa miaka ijayo; rais anaongelea issues zinazogusa, zilizogusa au zitakazogusa jamii nzima

Tatizo nadhani mkuu wewe hutetei hotuba ila unatetea Mleta hotuba.
  • Kwa hiyo unataka kusema mambo aliyoongelea hayana wizara?.
  • Na ukisema Issue zinazogusa, Zilizogusa, ZITAKAZOGUSA jamii ndio mimi nakueleza sasa hivi Dunia hi tuliyopo sasa inaendeshwa na TEKNOHAMA. Hivi Unajua Role ya TEKNOHAa katika biashara, elimu, Utalii, etc Kidunia ? Hayo mambo ya kitambulisho cha Taifa ilitakiuw kuwa ndani na sehemu ya ya mada Kuu ya TEKNOHAMA. Kama ulivyosema yanahusika na wizaraya mambo ya ndani .
Kwenye hotuba Rais kataja suala la mafuriko limeleta hasara. Lkini issue za mafuriko si zina wizara yake. Je unajua hasara ya kuuza Swala na twiga kwa $ 200. Je unajua kuwa China wao wanakodisha panda wao.

Topical hakuna tutakachobadilisha kwenye hotuba ya Mh Rais lakini hapa tunatoa mtazamo mbadala pia jaribu kuangalia na kutathmini. Mimi kama mdau wa teknohama natarajia Rais kila anapopata fursa azungumzie na kukumbusha sekta mbali mbali nafasi , fursa na changamoto za TEKNOHAMA zilizopo Tanzania.
 
Umasikini wa watanzania haushii kwenye uwekezaji tu,kwani kwenye madini hakuna wawekezaji?je ni nini tumefaidka na uwekezaji huo,Tulikuwa na kiwanda cha zana za kilimo Mbeya hakikupata mwekezaji?Viwanda vya nguo ili pamba inayolimwa kanda ya ziwa ifanyiwe kazi hapa hapa,hivyo viwanda havikupata wawekezaji?
Na je kuna tofauti gani ya hotuba zake ama salamu za mwaka mpya ambazo JEY KEY amekuwa akizitoaambazo zimefanyiwa kazi na impact ikadhihirika?matokeo yake Rais anawauliza tena wananchi malimbikizo yatakoma lini,mwalimu analalamika Rais analalamika hapo kuna kitu?
Hivi ni kwanini asizungumzie UFISADI ambao ndio unalimaliza Taifa hili pia,ufisadi ndio unaleta umasikini kama sio kuchangia kwa asilimia kubwa,kumbuka ukizungumza kilimo kwanza utazungumzia pembejeo pia hamjui kama zilifanyiwa ufisadi kila inapofika muda wa usambazaji?angalia miradi hewa,mfano ni kule Tanga ambako mwisho wa siku wabunge wa CCM-magamba wakapokea rushwa ili kuzima sakata la ufisadi uliofanyika au hamkumbuki Kafulila aliwataja kwa majina,sasa haya ni mambo makubwa ambayo alitakiwa kuyazungumzia pia kwani ni kikwazo katika maendeleo ya taifa hili,leo ameleta hadithi ama historia yenye lugha ili watu waone anajali anajali kitu gani walimu tu bado hajatimiza,ngoja nisali kwanza maana ni hasira tupu binafsi sijaona hotuba wala salamu
 
Tatizo nadhani mkuu wewe hutetei hotuba ila unatetea Mleta hotuba.
  • Kwa hiyo unataka kusema mambo aliyoongelea hayana wizara?.
  • Na ukisema Issue zinazogusa, Zilizogusa, ZITAKAZOGUSA jamii ndio mimi nakueleza sasa hivi Dunia hi tuliyopo sasa inaendeshwa na TEKNOHAMA. Hivi Unajua Role ya TEKNOHAa katika biashara, elimu, Utalii, etc Kiunia ? Hayo mambo ya kitambulisho cha Taifa ilitakiuw kuwa ndani na sehemu ya ya mada Kuu ya TEKNOHAMA. Kama ulivyosema yanahusika na wizaraya mambo ya ndani .

Angalia umeshaanza uwoga/hisia kama kawaida yenu eti mimi namtetea mleta hotuba na siyo hotuba what if mimi nikisema wewe unamshambulia mtoa hotuba na siyo hotuba..lol

Back to the topic; umuhimu wa teknohama unajulikana na inatakiwa kuhuishwa kwenye kila taasisi hilo halina taabu; sioni kwanini rais alizungumze hilo wakati kila taasisi inajitahidi kujiingiza kwenye teknolijia hiyo??

Sijaona tatizo kwenye hotuba yake; sijaona aliyekuja na criticism za maana kwa faida ya nchi ili nimuunge mkono zaidi ya stereotype za kila siku
 
.... Nimearifiwa kuwa shilingi 817,740,849 zimelipwa kwa ajili ya kugharamia ukarabati wa nyumba zao zilizoharibiwa. Bahati mbaya kwa wale ambao nyumba zao ziliharibiwa sana na kulazimika kujengwa upya kazi hiyo imechelewa sana kuanza kwa sababu za urasimu wa kupata viwanja.
Kauli za JK bwana, lazima aweke mtu wa tatu ambaye kama mambo yariharibika/ yakiharibika lawama zimwendee yeye!... anapenda kweli kusikia "Watendaji wa raisi ndio wanamuangusha". Yaani hapa hana uhakika na kile "alichoarifiwa" kama ni kweli au la.
 
Ukilinganisha na miaka 70 ya ukoloni na miaka 50 ya uhuru; tumefanikiwa sana..je siyo kweli?

kama tumefanikiwa kwa nini shule zetu zinatoa wanafunzi butu, kwa nini tunashindwa kusomesha watoto chuo kikuu, kwa nini zahanati hazina dawa, kwa nini hata TRC yetu imekufa hivi hivi tunaona, ATC yetu imepaa tumebakia kwenda kigoma na Tabora, wakati wa mkoloni EAA ilienda sehemu nyingi tu.

Maendeleo ya namba kwamba chuo kilikuwa kimoja sasa hivi vipo 40 haya sioni kama ni maendeleo.
 
Hali ya Usalama Nchini

Uharamia Baharini


Ndugu Wananchi
;
Hali ya usalama wa nchi yetu katika mwaka 2011 ilikuwa ya kuridhisha na Tanzania iliendelea kuwa nchi yenye amani na utulivu. Kwa jumla, mipaka yetu yote ilikuwa salama isipokuwa ule wa majini kwa upande wa Bahari Kuu ya Hindi ambako kumekuwepo na matukio ya uharamia. Katika mwaka huu tunaoumaliza leo, kumekuwepo na majaribio tisa ya kuteka meli ndani ya mipaka yetu katika Bahari Kuu hiyo. Bahati nzuri hakuna hata moja lililofanikiwa kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na Jeshi letu la Wanamaji. Maharamia saba wamekamatwa na kufikishwa Mahakamani ambako kesi zao zinaendelea.

Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi maalum kwa Jeshi letu la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa kazi nzuri waliyoifanya na wanayoendelea kuifanya ya kupambana na maharamia katika Bahari Kuu ya Hindi. Kutokana na juhudi zao hizo matukio ya kujaribu utekaji meli yamepungua mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana ambapo kulikuwa na matukio 30.
Haya ni maneno ya kutumwa na rafiki yake kipenzi Obama.
Hamna lolote!.Hivi kweli una jeshi la wanamaji wewe au matarishi tu wa US navy?.
 
Back
Top Bottom