Hotuba ya Rais Kikwete kuuaga mwaka 2011

Umasikini wa watanzania haushii kwenye uwekezaji tu,kwani kwenye madini hakuna wawekezaji?je ni nini tumefaidka na uwekezaji huo,Tulikuwa na kiwanda cha zana za kilimo Mbeya hakikupata mwekezaji?Viwanda vya nguo ili pamba inayolimwa kanda ya ziwa ifanyiwe kazi hapa hapa,hivyo viwanda havikupata wawekezaji?
Na je kuna tofauti gani ya hotuba zake ama salamu za mwaka mpya ambazo JEY KEY amekuwa akizitoaambazo zimefanyiwa kazi na impact ikadhihirika?matokeo yake Rais anawauliza tena wananchi malimbikizo yatakoma lini,mwalimu analalamika Rais analalamika hapo kuna kitu?
Hivi ni kwanini asizungumzie UFISADI ambao ndio unalimaliza Taifa hili pia,ufisadi ndio unaleta umasikini kama sio kuchangia kwa asilimia kubwa,kumbuka ukizungumza kilimo kwanza utazungumzia pembejeo pia hamjui kama zilifanyiwa ufisadi kila inapofika muda wa usambazaji?angalia miradi hewa,mfano ni kule Tanga ambako mwisho wa siku wabunge wa CCM-magamba wakapokea rushwa ili kuzima sakata la ufisadi uliofanyika au hamkumbuki Kafulila aliwataja kwa majina,sasa haya ni mambo makubwa ambayo alitakiwa kuyazungumzia pia kwani ni kikwazo katika maendeleo ya taifa hili,leo ameleta hadithi ama historia yenye lugha ili watu waone anajali anajali kitu gani walimu tu bado hajatimiza,ngoja nisali kwanza maana ni hasira tupu binafsi sijaona hotuba wala salamu

Good points;

Ufisadi katika madini ni swala ambalo liko delicate sana kama mafuta ..

Rais nafikiri amekwepa kuongelea Symbion kama ambavyo chadema wamefyata mkiya kuongelea symbion kwasababu kuna bwana zao wakubwa hapo

Halikadhalika kuongelea Barricks ni sawa kutaka kuacha urais kama Qadafi alivyo uacha ..

Hiyo ndio reality ya New Worl Order kwa sasa
 
kama tumefanikiwa kwa nini shule zetu zinatoa wanafunzi butu, kwa nini tunashindwa kusomesha watoto chuo kikuu, kwa nini zahanati hazina dawa, kwa nini hata TRC yetu imekufa hivi hivi tunaona, ATC yetu imepaa tumebakia kwenda kigoma na Tabora, wakati wa mkoloni EAA ilienda sehemu nyingi tu.

Maendeleo ya namba kwamba chuo kilikuwa kimoja sasa hivi vipo 40 haya sioni kama ni maendeleo.

Maendeleo ni both numbers and quality; huwezi ku generalize tu kwamba vyuo vyetu, shule zetu, etc ni mbovu zinatoa wanafunzi wabovu that is being unrealistic..

Viwanda vimekufa kama ujamaa ulivyokufa; viwada binafsi vinaanza kuongezeka ku-take over from goverment industries..
 
@ Topical
Unaona ni sawa JK kutozungumzia au kutogusia issue tata ya nyongeza ya Posho za wabunge katika kipindi amabcho tunaabiwa hata hazina imekaukiwa au kuna kitu anakwepa . Je hilo jambo halikugsa, haligusi na halitagusa jamii nzima.
 
Sidhani kama kuna haja kuongelea jambo ambalo unatakiwa kutoa maelezo kwa ofisi ya bunge period

Again siyo kweli kwamba hazina imekauka, wewe unapata taarifa zako kutoka kwa nani? zitto? au slaa

Nenda wizarani taifa lina changamoto lakini halijakauka; tunakusanya TRA kupita wakati wowote katika historia ya nchi hii..
Of course tuna tatizo la matumizi mabaya hasa kwa wataalam (experts) maofisa wa serikali ndio wanaongoza kwa uwizi, lazyness, lack of creativity, lack innovations to improve public service..ni mapambano ambayo hata chadema/cuf wakichukua nchi watayakuta ..

Mimi nafikiri alichosahau ni "poor public services from public institutions to wananchi" huu ni msiba mkubwa wa taifa hasa maofisa wetu ni hawahudumia wananchi na hii spirit is dying day by day..
 
Maendeleo ni both numbers and quality; huwezi ku generalize tu kwamba vyuo vyetu, shule zetu, etc ni mbovu zinatoa wanafunzi wabovu that is being unrealistic..

Viwanda vimekufa kama ujamaa ulivyokufa; viwada binafsi vinaanza kuongezeka ku-take over from goverment industries..
Maendeleo yanayotajwa yamelala kwenye namba tu ubora na uhalisia ni zero na ndio maana tunarudi nyuma baada ya kustabolaize yaani ups downs kwenye kila kitu thamani ya shiling, kuombaomba & employments.
We endelea kujipa false hopes ambazo hazitakusaidia.
Kinachotakiwa kukubali uhalisia wa mambo/tatizo na kujipanga upya.
 
Ya kuhusu wawekezaji wa ndani?

Wewe unataka kuwekeza? wapi?

Wewe na yule na mwingine ndio wawekezaji wa ndani? mpo fursa zimeelezwa pale

changamkeni msisubiri wahindi (watanzania) wakizitumia inakuwa nongwa
 
Angalia umeshaanza uwoga/hisia kama kawaida yenu eti mimi namtetea mleta hotuba na siyo hotuba what if mimi nikisema wewe unamshambulia mtoa hotuba na siyo hotuba..lol

Back to the topic; umuhimu wa teknohama unajulikana na inatakiwa kuhuishwa kwenye kila taasisi hilo halina taabu; sioni kwanini rais alizungumze hilo wakati kila taasisi inajitahidi kujiingiza kwenye teknolijia hiyo??

Sijaona tatizo kwenye hotuba yake; sijaona aliyekuja na criticism za maana kwa faida ya nchi ili nimuunge mkono zaidi ya stereotype za kila siku
Mbona kazunguzia kitambulishao cha taifa kitu amabcho kiko chini ya wizara ya mambo ya ndani. Hivi wewe unajua Kitambulischo cha taifa kina au kitakuwa na faida gani kwa mtanzania.

Tatizo kwenye hotuba lipo lakini Matatizo ya tanzania hayaishi kwa hotuba ya mwaka mpya. mambo aliyoyongelea ni yale aliyoyapa priority yeye( Hio ndio Tatizo). Lakini ukiangalia kitaifa na maendeleo kuna mambo ya muhimu yalitakiwa kutajwa.Mii ndio Nimetolea mfano katika dunia tuliypo sasa neno TEKNOHAMA halikutakiwakuosekana.

Katika Nchi inayotegema UTALII tuulitakiwa tusikie RAsi anaongeleaa kuhusu mambo ya uuzwai wa wanyama. yanazungumziwa. maa una matukio yaligusa jamii.

Katika hali ya uchumi tete na mfumuko wa bei na hazina Kukaukiwa tulitaiwa tusikerasi anasema nini kuhusu Posho za wabaunge.

Yaani kuna mambo ya msingi yanayogusa yaligusa na yatayogusa jamii kama ulvyosema hajayaongelea.
 
Maendeleo yanayotajwa yamelala kwenye namba tu ubora na uhalisia ni zero na ndio maana tunarudi nyuma baada ya kustabolaize yaani ups downs kwenye kila kitu thamani ya shiling, kuombaomba & employments.
We endelea kujipa false hopes ambazo hazitakusaidia.
Kinachotakiwa kukubali uhalisia wa mambo/tatizo na kujipanga upya.

Uhalisia upi? mkuu

Mimi nina ndugu zangu kibao wamepata division two; shule za kata to be specific kutoka Dodoma (kondoa); wanaenda chuo mimi nazipenda sana hizi shule za kata; japo sipingi kwamba zinatakiwa kuboreshwa zaidi lol

Never loose hope; kujipanga ni kila siku katika maisha
 
Mbona kazunguzia kitambulishao cha taifa kitu amabcho kiko chini ya wizara ya mambo ya ndani. Hivi wewe unajua Kitambulischo cha taifa kina au kitakuwa na faida gani kwa mtanzania.

Tatizo kwenye hotuba lipo lakini Matatizo ya tanzania hayaishi kwa hotuba ya mwaka mpya. mambo aliyoyongelea ni yale aliyoyapa priority yeye( Hio ndio Tatizo). Lakini ukiangalia kitaifa na maendeleo kuna mambo ya muhimu yalitakiwa kutajwa.Mii ndio Nimetolea mfano katika dunia tuliypo sasa neno TEKNOHAMA halikutakiwakuosekana.

Katika Nchi inayotegema UTALII tuulitakiwa tusikie RAsi anaongeleaa kuhusu mambo ya uuzwai wa wanyama. yanazungumziwa. maa una matukio yaligusa jamii.

Katika hali ya uchumi tete na mfumuko wa bei na hazina Kukaukiwa tulitaiwa tusikerasi anasema nini kuhusu Posho za wabaunge.

Yaani kuna mambo ya msingi yanayogusa yaligusa na yatayogusa jamii kama ulvyosema hajayaongelea.

Sawa kabisa wala asingeweza kuongelea kila kitu kwa siku moja au kwa hotuba moja..

Kuna mambo mengi ambayo wewe unaweza kuona ni muhimu lakini rais ameona yaliyo muhimu yatakayo gusa taifa siku zijazo not limited to but includes hayo aliyoyataja ..kuna tatizo na hayo aliyoyataja?
 
Ni kweli kwamba shida yetu ya umasikini ni wawekezaji?

Maana naona keshalipatia jibu tayari lile swali la kwanini sisi masikini lol

ili tuendelee hatuhitaji tena Ardhi,Watu,Utawala Bora na Siasa safi

ili tuendelee tunahitaji Wawekezaji na Misaada- J.k
 
..."Kumchagua Kikwete katika uchaguzi huu wa 2010 ni janga kubwa la Kitaifa." alisema Dr Slaa. Maneno yake yanazidi kujidhihirisha kila siku iendayo kwa Mungu. Mungu inusuru nchi yetu.
 
His brain are so limited! he was 50/50 back then....now he is kaputi (meathead) and that was the best choice of the socialist party....77yrs ya mkoloni ndio imekifanya chama cha hicho kiishi miaka 50, uhuru gani tunaosherekea kilaza. mmerithi sheria za mkoloni za ungandamizaji ndio mko hai...sasa tuongee kuibadalisha katiba unahunyahunya. tunataka katiba inatuambia wanyama wote wanahakii...hakuna ngururewe aliyeko juu ya sheria. ukiua na wewe unauawa.

Matenos si usted puedes
 
Sidhani kama kuna haja kuongelea jambo ambalo unatakiwa kutoa maelezo kwa ofisi ya bunge period

Again siyo kweli kwamba hazina imekauka, wewe unapata taarifa zako kutoka kwa nani? zitto? au slaa
Hata magufuli kamtoa nishai Juzi Mk ullo kuwa wakandarasi i wamembana wanataka pesa zao. Kwa jambo hilo na mifano mingine mingi kama unasoma between the lines unatakiwa kujua kuwa hazina haiko sawa kwa sasa katia kubalce income na expenditure zake .

Nenda wizarani taifa lina changamoto lakini halijakauka; tunakusanya TRA kupita wakati wowote katika historia ya nchi hii..
Of course tuna tatizo la matumizi mabaya hasa kwa wataalam (experts) maofisa wa serikali ndio wanaongoza kwa uwizi, lazyness, lack of creativity, lack innovations to improve public service..ni mapambano ambayo hata chadema/cuf wakichukua nchi watayakuta ..
Kwa sentesi fupi ya uliyoeleza hapo juu tunaweza kusema Tuna viongozi wasio na dira na tatizo la usimamizi mbovu.

Na ukisema Lack of innovation kuimprove public service moja ya hiyo innovation iko kwenye TEKNOHAMA. Kama kiongozi mkuu haoni umuhimu wa kuitaja TEKNOHAMA katika hotuba zake nani anataiwa kuwa innovative. Kiongozia anatkiwa awe na VISION then kupitia VISION yake ndio innovative ideas zinakuja.
Mimi nafikiri alichosahau ni "poor public services from public institutions to wananchi" huu ni msiba mkubwa wa taifa hasa maofisa wetu ni hawahudumia wananchi na hii spirit is dying day by day.

Sasa unaona mimi nimeongea neno TEKNOHAMA niiwa nalenga kitu kama hiki. Labda wewe huunielewa. Wewe unaongelea Problem ya tatziao la huduma kwa jamii. Mimi nimeongea rais Kutooongoolea jinsi SEKTA ya TEKNOHAMA ilivyo na fursa za za kusaidia kutatua na upunguza changamot kwenye sehemu nyingi zinazota huduma wa jamii.

Maaana yake wewe unaongelea Problem mimi nimeongela Problem na solution ambayo Rais anatakiwa kuongelea.
 
Mara kadhaa unawasikia watu hapa nchini na kwingineko duniani wakiuliza kwa nini nchi za Afrika, Tanzania ikiwemo ni maskini wakati rasilimali zimejaa tele. Moja ya sababu kubwa ni kutokuwepo kwa uwekezaji wa kutosha wa kuzigeuza rasilimali hizo kuwa bidhaa na huduma za kuuza katika soko na kuwapatia mapato wamiliki wake watakayoyatumia kuboresha hali zao za maisha. . Chukua, kwa mfano, mtu mwenye msitu mkubwa na mzuri anayetaka uwe shamba la kuzalisha mazao yatakayomwezesha kupata mapato yatakayosaidia kubadili maisha yake. Haitakuwa hivyo mpaka pale atakapochukua panga na jembe akafyeka na kulima, baadae akachukua mbegu akapanda, akaweka mbolea, akapalilia, akavuna na kupeleka mazao sokoni kuuza akapata pesa, atakapozitumia kujipatia mahitaji yake ya maisha. Kufyeka, kulima, kupanda, kupalilia, kuvuna na kupeleka sokoni ndiyo uwekezaji.
Hotuba iko shaghalabhaghala kweli kweli, kwa mfano kipengele hiki cha hotuba, inaonekana kama vile anazungumza na wawekezaji wa ndani na huku kama ni wa nje...

On top of that, hakuna solution ya kuhakikisha kuwa tunazigeuza rasilimali hizo na kuzifanya bidhaa na wakati ni wazi hadi madini na everything else za rasilimali zetu vinasafirishwa bila kuwa proccessed?

Mnajuwa ni kiasi gani cha kazi na mapato ya Taifa vinapotea kwasababu hii?

Tanzanite yenyewe hadi last time si nasikia inapelekwa India kuwa processed? Kama umemwambia mwananchi kuwa kuwekeza ni sawa na "Kufyeka, kulima, kupanda, kupalilia, kuvuna na kupeleka sokoni mara baada ya kununua shamba" Je wananchi wanajuwa namna ya kufanya hayo?

Hivi huo mfano ameulekeza kwa mwananchi mwekezaji wa ndani ama wa nje?

Na mbona bado sioni kabisa ni kivipi mfano huo ni relevant na uwezo wa mwananchi ama wananchi kutokuweza kuwekeza?

Labda kama aliyalenga makampuni ya nje.

Ok, lets say mwekezaji huyo ni wa ndani na ni mkulima, ina maana kweli mh rais hajui matatizo yanayowakabili wakulima?

Na yanayowakabili wawekezaji wa ndani mbona ni simple tu?

Si waangalie ni bidhaa gani tunaweza kuzalisha halafu tuzizalishe kwa viwango vinavyohitajika kwenye masoko hayo ya kimataifa?

Whats so hard there? Ndo huo ukiritimba or beurecracy?

Bado tu mh rais unastruggle ku define our problems? Hivi wewe ni Sultan kutoka wapi?
 
Sawa kabisa wala asingeweza kuongelea kila kitu kwa siku moja au kwa hotuba moja..

Kuna mambo mengi ambayo wewe unaweza kuona ni muhimu lakini rais ameona yaliyo muhimu yatakayo gusa taifa siku zijazo not limited to but includes hayo aliyoyataja ..kuna tatizo na hayo aliyoyataja?

Yes tatizo ni Priority . Katika Dunia tuliyopo na matukiyo yaliyotokea alitakiwa kutaja
  • TEKNOHAMA
  • UUZAJI WA WANYAPORI NJE
  • POSHO ZA WABUNGE
Kwangu haya ni muhimu kuliko hata habari za maharamia wa Kisomali
 
Back
Top Bottom