Hotuba ya Rais Kikwete, Bungeni Dodoma - Novemba 07, 2013

KakaJambazi

JF-Expert Member
Jun 5, 2009
18,711
12,067
Updates:

Saa 10:20 jioni: Wabunge wote wameshaketi na viongozi wote, ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Mkuu n.k wameshafika na Rais Kikwete anawasili bungeni.

Saa 10:25: Spika Makinda anamkaribisha Mhe. Rais ili aweze kulihutubia Bunge

- JK anaanza kufafanua juu ya suala la Katiba Mpya

- Anaongelea mauaji ya Ndovu; anasisitiza Operesheni Tokomeza itaendelea, imesitishwa kwa muda kurekebisha madhaifu yaliyojitokeza

- Anaongelea suala ya JWTZ ndani ya Congo na sababu ya Tanzania kupeleka wanajeshi na anawasifu wanajeshi wetu kwa kazi nzuri

- JAMBO KUU LILILOMLETA BUNGENI ni kuzungumzia kinachoendelea katika Jumuiya ya Afrika Mashariki; anaanza kufafanua.

- JK anasisitiza, pamoja na vitimbi wanavyotufanyia ndani ya EAC, Tanzania haijiondoi ndani ya Jumuiya. Hatoki mtu!

- JK anadai kuwa Tanzania haijaalikwa kwenye mikutano ilofanywa na haijakataa mwaliko wowote

- JK: Hatujaunga mkono kuharakishwa kwa shirikisho la kisiasa ili mambo muhimu kwanza yawekwe sawa. Huu ni msimamo wa watanzania na si wa JK. Watanzania wanataka umakini mkubwa katika maamuzi haya na hawana shida na kuanzishwa kwa shirikisho

- JK amemaliza na sasa Pinda anatoa neno la shukrani.

===== Hotuba Yote =====

 
mda si mrefu rais kikwete atalihutubia bunge. tbc tayari imeshajiunga dodoma live bungeni dodoma kurusha hotuba ya mh. rais, namuona edwad lowasa, kamati ya uongozi ya bunge na kamati ya mapokezi zipo pale langoni tayari kwa mapokezi ya rais
 
makam wa rais,waziri mkuu, rais wa znz pamoja na viongozi mbalimbali wa kitaifa wapo kwenye line up ya mapokezi
 
Nipo viwanja vya bunge nje kwenye maspika. Mh rais keshawasili.
 
namuona kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, freeman mbowe, hamad rashid mohamed, pamoja na wabunge kadhaa pale
 
Habari Wanajamvi.

Tunafuraha kuwaunganisha moja kwa moja kupitia Television ya Taifa ili kuwaletea hotuba ya Mh. Rais Dr. Jakaya Kikwete akihutubia Bunge leo hii.

Kiunganishi chetu cha matangazo mtandaoni ni kilekile:

StarTV Live | StarTV

Karibuni na endelea Kutazama Star TV.
 
Namwona Kigwangala yupo katikati ya Lowasa, Chenge na Filikunjombe. Wenzie wanapiga stori yeye anajichekesha chekesha hana anayempa attention. Duh! Kweli wenzie wamemdharau!
 
Sasa ivi shuhuli zimeanza anaesubiriwa ni rais tu kuingia bungeni chanel zote hazionyeshi ni tbc tu ipo live
 
Pale nje namuona mbowe akijiongelesha na waziri mkuu akisubiria kumpa mkono rais safi sana
 
Namwona mh flan simjui jina anakimbia kuingia, nahisi anaogopa kuonekana amechelewa.
 
suti zimepigwa kweli kweli leo, naona wamezinunua leo kabisa hizi, hasa kigwangalla na mbowe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…