Hotuba ya Rais Kikwete 30.6.2012

Hotuba ya Rais Kikwete 30.6.2012

Kujiandaa na lolote kama lipi kwa mfano? funguka..

Isn't obvious kuwa people are not buying your stories any more? Busara ni kujiandaa kwa kuacha madaraka vizuri pamoja na madhaifu yenu jaribuni kutatua mgogoro huu inavyotakiwa Rais anaonyesha kukosa busara na kutaka kutumia mabavu huku akishindwa kuonyesha nia ya dhati ya kutatua mgogoro huu. Pale anapoendeleza malumbano yasiyo na tija na huku ana uwezo wa kutatua matatizo haya mara moja kwa ufupi Serikali imejaa mizaa tupu.........................kujiandaa kwa lolote ni kujua kuwa Watanzania si makondoo na kwa style mnayotumia things can get outta control very soon jua tu kuwa this can be fixed though its sad kuwa washaharibu mno
 
Tuna mifano kadhaa ambayo vyombo vya usalama vinajichukulia sheria mkononi. Kama yaliyotokea kwa Zomba kuua wafanyabiashara wa madini kule msitu wa Louis Mbezi aliagizwa na serikali au ilikuwa ni mipango yake binafsi kuwachomowa waathirika?

Candid Scope, hili tatizo halikustahili kufika hapa lilipofikia. Ni kwasababu ya arrogance ya watu wenye madaraka. Hata hivyo,siamini kabisa kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinajichukulia sheria mikononi bila consent ya serikali. Ni kweli kabisa watanzania wanahitaji madaktari kuwa kazini bila mizengwe yoyote. Ila pia kosa kubwa limefanyika kwa kumuumiza Dr. Ulimboka maana watu wengi hawaamini kama yale mambo yamemkuta bila mkono wa serikali...na hisia haziji hivi hivi...people are connecting the dots
 
Last edited by a moderator:
Huyu bwana Juma Mgaza ndo nani wakuu.Inaonekana yeye ndo alimwokoa Dr Ulimboka.Na kama ni kweli i think he will be the next to follow the foot step.Manake chini ya hutuba ya mkuu kamrusha yangu macho

hata mimi nimeshtuka mkuu kwanini amshukuru Mgaza kwa msisitizo kwenye hotiba yake. sawa alikuwa wa kwanza kumuona majeruhi lakini hyo concern ya mkuu kama siielewi vile. i smell something fishy...
 
Unajua uungwana unatuzidi sana, siku moja tutajikuta na Police nao wanagoma. Labda kweli tufanye jaribio, Police wagome masaa 24 tu tuone kitakachotokea.
Jamani ee, sheria ni sheria tu. Inafahamika kwamba Dr. haruhusiwi kugoma, full stop. Wamegoma - wamejifukuza, BASI. Kwa heri.
Unaona maajabu ya Mungu? Kaongoza migomo, kajikuta anahitaji huduma ya waliogoma.

Maajabu ya Mungu,ni kutaka kumpoteza ilo ma dr waogope,ila akawaumbua bado yupo hai,na wananchi ss wameelewa
 
Isn't obvious kuwa people are not buying your stories any more? Busara ni kujiandaa kwa kuacha madaraka vizuri pamoja na madhaifu yenu jaribuni kutatua mgogoro huu inavyotakiwa Rais anaonyesha kukosa busara na kutaka kutumia mabavu huku akishindwa kuonyesha nia ya dhati ya kutatua mgogoro huu. Pale anapoendeleza malumbano yasiyo na tija na huku ana uwezo wa kutatua matatizo haya mara moja kwa ufupi Serikali imejaa mizaa tupu.........................kujiandaa kwa lolote ni kujua kuwa Watanzania si makondoo na kwa style mnayotumia things can get outta control very soon jua tu kuwa this can be fixed though its sad kuwa washaharibu mno

Watu wengi bado wanaiamini serikali na maelezo ya Rais; of course kuna watu wengi pia ambao wameamua kuwaamini wapotoshaji na wapingaji wakubwa..

Bottom line election 2015 ita determine nani anasema kweli au nani anatafuta popularity kwakutumia migongo ya watu maskini

In this case wananchi wengi wako against madrs..except few political elites who can afford to pay private hospitals..

na madrs hawana hoja kwa maelezo ya JK na kwa mtu mwenye chembe ya UTU na nidhamu kazini..
 
Kwahiyo kwenye hii kesi as you stated "vyombo vya usalama" vilijichukulia sheria kwa maslahi ya nani? Mimi ninachoona ni clear contradiction kwenye hotuba nzima, achana na ya Zombe kwanza kwa suala hili itakuwa kazi sana kwa Kikwete and co kusafisha mikono yao, hawatamaliza hii ishu kama walivyozoea kwa kusema wacha ni upepo utapita..........the damage is already done mi friend

Ningependa kujadili zaidi suala la Madaktari kufanya uamuzi wa kusitisha mgomo na kuamua kubaki kuendelea na huduma, la sivyo hawakubaliani na ridhaa ya seriakali, basi waondoke na kwenda huko wanaokofikiria watapata mafao yanayodai. Kwamba serikali imehusika katika kifo cha Dr. Stephen au la mimi sijui, na kinachoongelewa hapa ni tetesi zisizothibitishwa mpaka sasa.

Serikali ina idara nyingi na njia mbalimbali za kumaliza matatizo, ukianza kufatili utaumiza kichwa bure kwani hayo ni mipango migumu kuifumbua wakati waliopanga wana njia zote za kufifisha kiini cha ukweli. Cha kumshukuru Mungu waliomteka Dr. Stephen hawakumwua na imesaidia kupata ukweli fulani. Huenda hao watekaji wamekiuka kagizo la wakuu wao, mkinzano huo wanaujua wao na kwa sababu zao wenyewe. Ndio maana serikali ye yote duniani ina kitendo cha siri cha inteligensia, hakuna asiyejua hili. Tutalalamika hatimaye tutapoa. Kwa wenye uelewa hatupotezei muda kujadili hilo, na kama madaktari wangekuwa na uungwana na utu katika kudai haki zao na kupima kwa busara hayo pengine yasingetokea.

Kosa ambalo madaktari wamelifanya kuwekea rahani uhai wa wagonjwa ili kuishinikiza serikali jambo ambalo halikubaliki. Utaona hospitali za mashirika ya dini ndizo za kwanza kutekeleza uamuzi wa sirikali kuwafukuza madaktari walio kwenye mgomo kwa vile mashirika ya dini yanajali kwanza uhai wa binadamu na dhana nzima ya kuwajibikaji.

Kadiri ya Hotuba ya Rais, kiasi kikubwa cha madai ya madaktari yalishashatekelezwa, na sitegemea kwamba madai yote yangekubalika kwa vile mengine yako nje ya uwezo wa serikali. Kumbuka unaporatibu mishahara ni kitu cha kutumu kwa maisha, katu siku serikali haiwezi kupunguza kiwango cha mishahara ila kukipaisha. Kwa hiyo busara na uratibu wa kiuchumi katika idara ya utumishi na hazina ndio wenye kupima kiwango sahihi kinachoweza kulipwa kadiri ya uwezo wa serikali, hali ya uchumi wa nchi na uwezo wa idara ya utumishi kadiri ya uchumi wa nchi. Vinginevyo ni kudai bila kujua taratibu na sheria za ajira na uchumi wa nchi. Tukumbuke pesa nyinzi zinazoahidiwa toka kwenye bajeti ya serikali haziko hazina bali ni pesa hewa zinazotegemewa kutoka matarajio ya vyanzo mbalimbali, kwa maana hiyo malengo yanaweza kufikiwa au yasifikiwe.
 
imetulia.....imeeleza bayana madai na uwezo wa serikali...! asieweza kufanya kazi aondoke ili serikali itafute replacement

Haijatulia mkuu, uwezo huo mdogo ni kwa watumishi wengine tu, wanaosinzia na kugonga meza mil 10+ zipo? na kila kukicha posho zinaongezwa tu kwa lipi wanalofanya? kupigana vijembe? kama uwezo ni mdogo basi kuwe na uwiano mzuri(si kulingana mishahara, la!) inawezekanaje afisa kilimo amegraduate alipwe 446,000/= halafu Maji marefu, sugu na wengine walipwe 10+ mil? kuna uwiano hapo? Acheni kuwa fooled kirahisi hivyo waTZ, TAFADHALI Mahesabu think big!
 
Itakuwa vizuri kama The Hague ikituona nasisi hapa TZ. Siyo vizuri ikaishia Kenya.
Unaipenda hii au hapana?

Anza kupeleka barua na watuhumiwa; omba msaada US na washirika wako wote (mfanye vizuri vile vikao vyenu vya jumuia) ..

Tutakutana mahakamani ..au vipi?
 
Kumbe unapiga mkwara tu..JK anajua namna ya ku-deal na hiyo mikwara wewe..

Nilikuwa nakupa namna itakayokupa easiest money..endelea kuwa na hatred kwa waarabu, wairan na waislamu wa Tanzania na nje..utakuwa darling wa US..na watakupa support umwondoe huyu JK muislam mbaya sana anaharibu Tanganyika aliyoiasisi st. nyerere..ok

Acha unafiki wa kila kitu kuingiza udini.Ndiyo maana Watanganyika wanasema CUF ni tawi la Uamsho...Kila kitu udini wapi na wapi wewe jamaa....?
 
Uboreshwaji wa MAZINGIRA ya kazi mbona yanakwepwa Sana....!
 
Ningependa kujadili zaidi suala la Madaktari kufanya uamuzi wa kusitisha mgomo na kuamua kubaki kuendelea na huduma, la sivyo hawakubaliani na ridhaa ya seriakali, basi waondoke na kwenda huko wanaokofikiria watapata mafao yanayodai. Kwamba serikali imehusika katika kifo cha Dr. Stephen au la mimi sijui, na kinachoongelewa hapa ni tetesi zisizothibitishwa mpaka sasa.

Serikali ina idara nyingi na njia mbalimbali za kumaliza matatizo, ukianza kufatili utaumiza kichwa bure kwani hayo ni mipango migumu kuifumbua wakati waliopanga wana njia zote za kufifisha kiini cha ukweli. Cha kumshukuru Mungu waliomteka Dr. Stephen hawakumwua na imesaidia kupata ukweli fulani. Huenda hao watekaji wamekiuka kagizo la wakuu wao, mkinzano huo wanaujua wao na kwa sababu zao wenyewe. Ndio maana serikali ye yote duniani ina kitendo cha siri cha inteligensia, hakuna asiyejua hili. Tutalalamika hatimaye tutapoa. Kwa wenye uelewa hatupotezei muda kujadili hilo, na kama madaktari wangekuwa na uungwana na utu katika kudai haki zao na kupima kwa busara hayo pengine yasingetokea.

Kosa ambalo madaktari wamelifanya kuwekea rahani uhai wa wagonjwa ili kuishinikiza serikali jambo ambalo halikubaliki. Utaona hospitali za mashirika ya dini ndizo za kwanza kutekeleza uamuzi wa sirikali kuwafukuza madaktari walio kwenye mgomo kwa vile mashirika ya dini yanajali kwanza uhai wa binadamu na dhana nzima ya kuwajibikaji.

Kadiri ya Hotuba ya Rais, kiasi kikubwa cha madai ya madaktari yalishashatekelezwa, na sitegemea kwamba madai yote yangekubalika kwa vile mengine yako nje ya uwezo wa serikali. Kumbuka unaporatibu mishahara ni kitu cha kutumu kwa maisha, katu siku serikali haiwezi kupunguza kiwango cha mishahara ila kukipaisha. Kwa hiyo busara na uratibu wa kiuchumi katika idara ya utumishi na hazina ndio wenye kupima kiwango sahihi kinachoweza kulipwa kadiri ya uwezo wa serikali, hali ya uchumi wa nchi na uwezo wa idara ya utumishi kadiri ya uchumi wa nchi. Vinginevyo ni kudai bila kujua taratibu na sheria za ajira na uchumi wa nchi. Tukumbuke pesa nyinzi zinazoahidiwa toka kwenye bajeti ya serikali haziko hazina bali ni pesa hewa zinazotegemewa kutoka matarajio ya vyanzo mbalimbali, kwa maana hiyo malengo yanaweza kufikiwa au yasifikiwe.

Jamani wana JF tujitahidi kuonyesha kwamba tuna akili timamu. Hata kama hazimo kiasi hiki, tujitahidi kujenga hoja.

Candid, ili nisikuite Candida hebu nieleze ni nchi gani Duniani iliyoendelea kwa kulipa mishahara mikubwa kwa wanasiasa? Ni idara gani ya utumishi inayowapangia mishahara mikubwa wabunge bila kufuata hiyo asilimia 20 - 25 huku wananchi wakihangaika na kodi.

Wapi ktk Dunia unayoifahamu utakuta wanaendelea huku Mbunge halipi kodi.

Tanzania! This is a Banana republic.
 
hata sikumbuki ni lini niliwahi kusikiliza hotba ya raisi
 
Acha unafiki wa kila kitu kuingiza udini.Ndiyo maana Watanganyika wanasema CUF ni tawi la Uamsho...Kila kitu udini wapi na wapi wewe jamaa....?

Ndio maana watanganyika wanasema CDM chama cha kanisa; kila kitu udini wapi na wapi wewe jamaa??

Naona unadandia treni kwa mbele..pole
 
Rais JK kaongea kwa watafiti wa mambo ni wazi madaktari hawewezi kufanikiwa na wengi watapoteza kazi J, tatu Madaktari wengi wataripoti kazini...
 
images

Huu ndio uamuzi Mgumu tunaotazamia ambao Kikwete ametamka leo.
Kauli ya Rais Kikwete imetulia na ameeleza ukweli ambao serikali ilivyochukua hatua na tahadhari dhidi ya madai na migomo ya madaktari. Pia imesaidia kutoa picha upande wa pili ambao wengi hutukuweza kuelewa kwa uwazi. Aliyoongea Rais kwa wenye kujua hali halisi ya uchumi wa nchi yetu na matatizo mengine ameeleweka. Kwa waajiriwa wa serikali wanajua mishahara wanayolipwa.
Dao kubwa hilo la Madaktari la Shilling 7,000,000 lisilozingatia uwezo wa serikali na uboreshwaji wa huduma nyingine za afya na hali kadhalika kutojali uboreshwaji wenye uwiano na idara nyingine za serikali usipishane kwa kiwango kikubwa mno. Ni mambo yale yale yaliyokuwa yanalalamikiwa na wananchi dhidi ya wabunge, kwani wengine wanavyohangaika na njaa wengine wanataka wawe wanaichi kama wako peponi.

Mishahara ya serikali kupandishwa kila mwaka nimeona tu Tanzania, kwani nchi nyingine huchukua miaka mingi hadi kima kipandishwe, kwani upandishwaji wa mishahara ni sababu nyigine inayodhoofisha uchumi na mfumuko wa bei kupanda holela. Ukishapandisha mishahara lazima kila kitu kitapanda, kodi nayo itapanda hakuna unafuu ila ni kuendelea kupiga mark-time. Mfano Marekani kwa wastani wa zaidi ya miaka 15 mishahara imepandishwa mara moja tu kipindi cha utawala wa Rais wa zamani George Bush kutoka $5.15/75 na kufikia $7.25/75 per hour kwa kima cha chini.

Nchi nyingi zina utaratibu kama aliofafanua Rais Kikwete kwamba asiyekubaliana na mshahara basi aache kazi aende kwa mwajiri mwingine ambaye atampa mshahara anaoutaka. Hii ndiyo sababu nchi kama za Ulaya na Marekani utaona watu hawalalamikii mishahara, ila huacha kazi na kwenda kwenye makampuni mengine ambayo hulipa zaidi kidogo. Kutokana na tatizo hilo utaona idara za elimu hasa walimu vyuo vya serikali wamejaa wahadhiri wa kumwaga toka mataifa mengine na kabisa toka Afrika kama nchini Marekani kwa sababu wamarekani hupenda kufundisha vyuo binafsi ambako hulipwa vizuri zaidi na hakuna kodi nyingi kama serikalini.

Madaktari nchi nyingi hawategemei malipo mahospitalini tu, bali wana ziada ya mitandao katika mashirika mengine na zahanati ampako hufanya part time, na huko ndiko wanakopata ziada ya kuendeshea maisha yao. Hata secta nyingine nchi tajiri duniani wafanyakazi hawategemea pato moja tu vinginevyo kuna ziada ya muda wa kazi ambao huwaongezea pato, vinginevyo wanakuwa na pato la ziada kwa kufanya kazi nyingine part time au kujiajiri baada ya kazi.

Kwa ufafanuzi wa Rais Kikwete nakubaliana naye Madaktari ambao hawako tayari wajiondoe na kwenda kwa mwajiri ambaye wanaona atawalipa kiwango wanachokitaka cha kufikia millioni 7 kama wanazolipwa wabunge. Kuendelea kuidai serikali kiwango ambacho serikali haina uwezo ni sawa na kunyonga mzazi wako kumdai zaidi ya uwezo unaomruhusu.

Pamoja mkuu. Ni kweli kabisa. Hakuna anayewalazimisha kubaki kwa mwajiri asiyetaka kuwaongeza mshahara wanaotaka wao. Naunga mkono kabisa kuwa waende wakatafute green pastures. Na usemavyo kuwa nchi nyingine wafanyakazi wanafanya part time baada ya saa za kazi ni kweli. Na hawa wetu wanafanya sana tu lakini si baada ya saa za kazi bali wakiwa ndani ya saa za kazi na hakuna anayewauliza. Pia wamejiajiri, wana maduka ya madawa, dispensary, na miradi mingi tu. Sijui kwa nini hawaridhiki jamani? Hii pesa iliyomuua nabii ISSA haijai mfuko ndugu zangu. Ridhikeni na mnachopata na kama hamridhiki, achieni ngazi! Shs 7,700,000/ ni mshahara wa walimu takribani 20 wenye shahada ya kwanza baada ya kukatwa kodi. Wacheni hizo jamani! Jaribuni kwenda kuajiriwa hospital za binafsi muone utalipwa sh ngapi kwa mwezi, na uthubutu kuwa na kazi za part time nje ya kituo ulichoajiriwa wakati wa kazi uone kama hujafukuzwa kama mbwa bila majadiliano. Mmebembelezwa saaaaaana sasa mnajiona ninyi ni MUNGU anayeshikilia uhai wa watu. Lakini muogopeni MUNGU MUUMBA aliyewapa uhai mlionao. Mnavyofanya msifikiri mnaikomoa serikali, mnajikomoa wanyewe kwa sababu kwake yeye BWANA MUNGU mtajibu kuhusu kila roho mliyoiacha ikatoka kwa migomo yenu.

Jamani, nilikuwa nawaza kwa sauti!
 
Mh.Rais watumishi wote wa serikali ni muhimu katika jamii,kila mtumishi kwa kada na nafasi yake. Be both wise and strong katika nia na maamuzi ya kushughulikia kero za watumishi.Ulianza kuwa grade wewe mwenyewe kwa kuona kada moja ni muhimu zaidi kuliko kada zingine ,hivyo kubaliana na wanachokitaka otherwise sijui utas
 
Watu wengi bado wanaiamini serikali na maelezo ya Rais; of course kuna watu wengi pia ambao wameamua kuwaamini wapotoshaji na wapingaji wakubwa..

Bottom line election 2015 ita determine nani anasema kweli au nani anatafuta popularity kwakutumia migongo ya watu maskini

In this case wananchi wengi wako against madrs..except few political elites who can afford to pay private hospitals..

na madrs hawana hoja kwa maelezo ya JK na kwa mtu mwenye chembe ya UTU na nidhamu kazini..

Umenikumbusha kuna jamaa alikuwa anahojiwa kwenye televisheni huku anamsukuma mgonjwa wake kwenye kibaiskeli pale maeneo ya MOI yeye japo mgonjwa wake alikosa matibabu lakini aliungana na madaktari na kuitupia lawama Serikali kwa kushindwa kushughulikia mgogoro wa madaktari huyo mtu sensible kweli mimi narudia kusema kwa mwananchi wa kawaida kuelekeza nguvu zake kulaumu madaktari ni kupoteza pumzi bure kwani hakuna sehemu daktari alipofunga mkataba na mwananchi kutoa huduma bora za afya na mengineyo lakini still hatustaili kadhia tunayopata kwa kukosa huduma za afya kutokana na mgomo so what should we do? Sahihi kabisa tukimwajibisha aliyepewa dhamana..........
 
Candid Scope, hili tatizo halikustahili kufika hapa lilipofikia. Ni kwasababu ya arrogance ya watu wenye madaraka. Hata hivyo,siamini kabisa kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinajichukulia sheria mikononi bila consent ya serikali. Ni kweli kabisa watanzania wanahitaji madaktari kuwa kazini bila mizengwe yoyote. Ila pia kosa kubwa limefanyika kwa kumuumiza Dr. Ulimboka maana watu wengi hawaamini kama yale mambo yamemkuta bila mkono wa serikali...na hisia haziji hivi hivi...people are connecting the dots

Ni kweli kwamba tukio la Dr. Stephen kuna mizengwe toka serikalini jambo ambalo huanyika kwa siri kila mmoja wetu anajua serikali po pote zina intelijensia katika kuzima mambo fulani, lakini jambo hilo limefanyika wakati mbaya ambapo serikali inatoa tamko la kuwafukuza madaktari walio kwenye migomo na kuwasitiri wenye kujali wajibu wa taaluma yao kulinda uhai wa raia.

Kwa hotuba ya Rais inaonyesha wazi serikali imejitahidi sana katika kusikiliza madai yao, lakini kwa akili ya kawaida tu huwezi kutegemea kwamba madai yote yatekelezwe kadiri unavyotaka kwa kuwa chunguni kule chakula si cha madaktari tu, wote wanatumbulia macho chungu kile, na mwenye kutunza chungu anajua mgao mwingine, anabidi bakishe kwa ajili ya mgao mwingine vinginevyo wengi watakufa njaa wakijali mmoja tu.

Milioni 7 wanazodai madaktari ni mno ukilinganisha na uwezo wa serikali, na hata kama chama kingine kiingie madarakani katu hawatawaze kutoa dau hilo kwani kuna kazi hadi kufikia huku kitu ambacho kitatuchukua muda mrefu.

Rais alitakiwa kuyaweka wazi haya hadharani mapema wengi tungeelewa ukweli wa pande zote mbili, kwani kwa muda mrefu tumekuwa na uelewa wa madai ya madatari tu bila kuona upande wa pili.

Kwa sasa ukweli ni serikali ipo sahihi katika kutoa hitimisho la mgomo huo, na madaktari vichwa ngumu waende wanaokoona watapata mafao hayo, na wadaktari wazalendo wenye kujali uhai wetu ndio tubaki nao hata kama ni wachache bora kuliko kuwa na kundi lisilojali uhai wetu.
 
Kimtazamo hapa kwa kutumia akili ya kawaida utagundua kuwa mpango wa kumuua dr ulipangwa na serikali nzima. Kwanini prezoo akurupuke na kuitetea serk na ili hali jambo hili linaweza kupangwa kuanzia kwa pm tu akaamrisha watu wa chini wakatekeleza bila yeye prezoo kujuwa? Alitakiwa asitetee kwanza aamrishe uchunguzi wa kina ufanyike ili kubaini ukweli wa jambo hilo kwani "lisemwalo lipo, kama halipo basi, laja" Hii inaleta mashaka kdogo.Ikiwa uchunguzi utabaini kuwa jambo hili lilitekelezwa kwa amri ya kiongozi wa juu kabisa serikalini ambaye si prezoo, atasemaje? Kwanini anasimama asbuhi hivi kuisafisha serikali ili hali mambo mengi machafu yamefanyika na viongozi wakubwa wa serk bila yeye kuhusika na wakawajibishwa? We have to think deep here.

Ni mtazamo wangu tu lakini.
 
Back
Top Bottom