Umetoa mfano wa Bloomberg. NYC ina matatizo mengi sana ya kifedha, mwaka jana kwa mfano, hela ya kusafisha snow iliisha kabla ya wakati, walimu wanakimbia inner city schools kwa sababu hawalipwi vizuri, police wengine wa NY wanaondoka kwenda PD za miji ya jirani wanakolipwa vizuri zaidi. Yote haya ni matatizo ambayo Bloomberg angeyatatua kwa kutoa tu hata robo ya utajiri wake lakini hajafanya hivyo, kwa sababu siyo njia muafaka ya kutatua tatizo. Leo MO anajenga mashule, mahospitali, visima nk, ikitokea akaamua kutogembea tena, au kushindwa uchaguzi na akaja mbunge hohehahe itakuwaje?
Dawa ni kufanya kazi bungeni kama alivyoomba kura kuwakilisha wananchi. Yeye si fisadi, lakini atunge sheria kwamba hela zote zilizoibwa na akina Chenge zirudishwe na mikataba mbali mbali ya kifisadi isainiwe upya. Akifanya hivyo zitapatikana hela nyingi za kujenga shule, barabara, visima na mahospitali na yeye hatatoa hela mfukoni mwake, badala yake hela zake atatanua biashara zake zaidi, ataajiri watu wengi zaidi na atalipa kodi zaidi. hivi ndivyo atakavyoleta maendeleo.
Balantanda said:Basi si vizuri kumhusisha Mohammed na tuhuma hizi(kuziweka tuhuma hizi kwenye habari hii ni sawa na kumhusisha moja kwa moja na tuhuma hizi) maana kipindi zinatokea dogo alikuwa zake shule na kampuni(kama sikosei) ilikuwa chini ya baba yake mzee Ghulam Dewji,kumhusisha Mohammed na tuhuma hizi ni kumuonea tu...Cha msingi ni kumpongeza kwa haya aliyowafanyia wananchi wake,ni tofauti kabisa na wabubge wengi(hasa wa CCM)
Balantanda,
..tayari nimeshampongeza Mheshimiwa Mohamed kwa juhudi na michango yake.
..lakini baada ya kumpongeza ndiyo nikakumbuka haya mambo ya michele mibovu.
..ni vigumu kutofautisha kati ya kampuni na wenye kampuni. naweza kukubaliana na wewe kwamba Mo alikuwa shuleni miaka ya 90, lakini kampuni anayoiongoza sasa hivi ni hiyohiyo iliyokuwa ikituhumiwa wakati ule.
..I am trying to find the facts, na inawezekana kabisa zinaweza kuisafisha kampuni ya mheshimiwa mbunge.
NB:
..kuna makampuni leo hii yanachunguzwa kwa kushirikiana na Nazi Germans in the 40s.
Bill Gates hakutaka kuzitumia haki zake za kiraia lakini sio kweli kuwa utajiri wake umemkataza kuingia kwenye siasa.
Mayor wa New York City ni Billionare na ni mwanasiasa. Hivyo utajiri haumnyimi mtu haki zake za kikatiba.
Zakumi, Zakumi, Zakumi nani kasema utajiri wa Bill Gates umemkataza kuingia kwenye siasa. Yeye ameamua kuutumia utajiri wake kuwawezesha wasio na uwezo bila malipo kama ya kupewa cheo tofauti na huyu Dewji anayeutafuta ubunge kulinda biashara zake. Pesa anazozitoa kutoka mfukoni mwake akiwa mbunge na mfanya biashara ni aina nyingine ya uwekezaji - kuna namna atazirudisha tu, huo ndio ukweli.
Zakumi, Zakumi, Zakumi Mayor wa New York hawezi kutoa hela mfukoni mwake kutatua matatizo ya wana New York kwa mipango ya zimamoto. Wana New York wanalipa kodi na wanataka kuona kodi zao zinatumika ipasavyo kama ilivyopangwa. Mayor wa New York analipa kodi na vyanzo vya mapato yake viko wazi kwa yeyote anayetaka kujua. Duh, Zakumi wewe ni Mtanzania kweli kweli.
Duh, jamani lakini mkuu wangu anatisha!.. kuwa na fedha au tajiri sii sababu ya kufanya yote haya ni MOYO wa kuipenda nchi na wananchi wako.
Keil,Angekuwa anawapenda wananchi wake asingeweza kujiingiza kwenye biashara ya kuagiza chakula kibovu ambacho hakifai kwa matumizi ya binadam. Wenye kumbukumbu watakumbuka kwamba aliwahi kuingia kwenye kashfa hiyo na kibaya zaidi mashahidi wote muhimu walipotea mmoja baada ya mwingine na kesi ikaisha. Kwa anayetaka details aende ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali aulizie.
Ni mfanya biashara, yuko hapo anafanya biashara na kulinda maslahi yake. Kwa kitendo cha kuwa Mbunge anakuwa na access ya kumuona Waziri yeyote na hata akitaka kwenda Ikulu kuonana na Mkulu anaweza kupata access kirahisi ukilinganisha na akiwa mfanya biashara wa kawaida tu.
Hivi kuna mfanya biashara anaweza kumwaga hela zote hizo bure bure tu, kisa eti anawapenda wananchi wake? Mbona mishahara ya wafanyakazi wa Kampuni yake ni duni? Angeanzia kuboresha mishahara ya wafanyakazi wake ambao wanamzalishia ndipo aende kumwaga hizo hela.
Mwisho kabisa, hakuna ambaye anaweza kuverify kwamba vitu alivyofanya vina thamani ya fedha hizo alizoandika, Wengi wamekuwa waki-inflate bei ya vitu wanavyochangia ili waonekane wamechangia hela nyingi sana na kumbe ni utapeli mtupu. Kuna kipindi tuliwahi kuletea news kutoka kwenye gazeti kwamba dawati moja lina gharimu shilingi laki 4! Kwa kutumia mbao za kutoka wapi? Sana sana mbao zinazohitajika ni 2 au 3, ambazo haziwezi kufika shilingi laki moja na ufundi bei ya dawati haiwezi kuvuka laki moja na nusu, hata kama hilo dawati limechongwa Dar.
Ngoja nichukue calculator nijumlishe hizo hela alizotoa masaada !!
Adaiwe vipi tax ikiwa mliweka exemption!ukishajumlisha na kupata jibu lake toa $25m ya kodi ya edible oil ambayo hajalipa.
jibu lake ndio faida ya ubunge wake
hakupewa exemption babu ila kwa ajili yeye ni mchangiaji mkubwa ndani ya ccm basi kodi halipiAdaiwe vipi tax ikiwa mliweka exemption!
Nifahamishe mkuu, navyojua mimi mafuta yalifutwa kodi na serikali kuingia mkataba na mashirika yote ya mafuta, hivyo najaribu kuelewa hoja yako!hakupewa exemption babu ila kwa ajili yeye ni mchangiaji mkubwa ndani ya ccm basi kodi halipi
siwezi kuamini bob unatetea peanuts huku ukiibiwa mahela kibao
hizo ndio faida anazozipata za kuchangia na kuwa mmbunge
Inajulikana kama kampuni iliyojaa harufu ya damu ay Watanzania.So jibu unalo kuwa ni za ufisadi ama???.Kaka/dada unaijua vizuri kampuni ya Mohammed Enterprises??
Habari usiyoijua ni mpya. Nikimaanisha kuwa kama ulikuwa unalifamu hili ungekuwa umeshaliweka hapa siku nyingi.HOTUBA YA MHESHIMIWA MOHAMMED DEWJI YA MKUTANO MKUU WA CCM WILAYA YA SINGIDA MJINI TEREHE 25/04/2009
hakuna haja ya kujadili leo,imepitwa na wakati hii.
..lakini hawa Mohamed Enterprise si walikuwa wanatuhumiwa kuingiza na kuuza mchele mbovu nchini?
..nakumbuka kulikuwa na mjadala mkali sana bungeni miaka ile. hivi mmesahau maelezo ya mheshimiwa Semindu Kisange Pawa bungeni kuhusu mchele wa Mohamed Enterprise?
..halafu kuna kifo cha Dr.Fupi, aliyekuwa Mkemia Mkuu wa serikali wakati ule. wako wanaodai kifo chake kilitokana na maamuzi yake kuhusu sakata ya mchele huo mbovu.
..hivi kuna anayefahamu kesi ile ilikwisha ktk mazingira yapi?
Mh... Pesa zote hizi kazitoa wapi?! Kama siyo za ufisadi????
Unakiri au unakataa?Jokakuu:
Kulikuwa na kesi moja kuhusu unga wa ngano uliooza. Kesi hii ilikwenda kwa Mrema na bungeni. Kwenye kesi hiyo Mohamed enterprise ilikuwa victim ya extortion ya tapeli mmoja ambaye nina undugu naye. Siwezi kutoa details zaidi kwa sababu zangu mwenyewe.
Kama unayozungumzia hiyo kesi, basi kuna mambo mengi sana yalikuwemo. Lakini utapeli ulitia chumvi kwa kiasi fulani.
Wenye masikio yakusikia na wasikieZakumi,Balantanda,
..I dont remember the exact details, lakini suala la Mohamed Enterprise lilifika mpaka Bungeni.
..Wabunge machachari kama Semindu Kisange Pawa walikuwa mstari wa mbele kufuatilia suala la uingizwaji nchini wa mchele mbovu.
..pia kulikuwa na kesi mahakamani, na inasemekana mashahidi kama watano hivi walikufa kabla hawajatoa ushahidi wao. Mkemia Mkuu wa serikali, Dr.Fupi naye alifariki, na kuna watu wanahisi alifanyiwa kitu mbaya.
..Jamii Forums ni jungu kuu hili, kwa hiyo nahisi kwamba tunaweza kupata ukweli wa kilichojiri wakati wa sakata/kashfa ile.
NB:
..kashfa hii ilitokea miaka ya 1990 -- 1994.
WeBalantanda,
..tayari nimeshampongeza Mheshimiwa Mohamed kwa juhudi na michango yake.
..lakini baada ya kumpongeza ndiyo nikakumbuka haya mambo ya michele mibovu.
..ni vigumu kutofautisha kati ya kampuni na wenye kampuni. naweza kukubaliana na wewe kwamba Mo alikuwa shuleni miaka ya 90, lakini kampuni anayoiongoza sasa hivi ni hiyohiyo iliyokuwa ikituhumiwa wakati ule.
..I am trying to find the facts, na inawezekana kabisa zinaweza kuisafisha kampuni ya mheshimiwa mbunge.
NB:
..kuna makampuni leo hii yanachunguzwa kwa kushirikiana na Nazi Germans in the 40s.
Mkandara,Huyo mkemia atasema anavyotaka lakini ndiye asiyeweza kazi yake.. NI mtu alotakiwa kufukuzwa kazi kwani wakati wa sakata hili mali zote nchini zilikuwa zinaingia feki na mbovu toka madawa hadi chakula..Ni majuzi tu serikali kwa msisitizo mkubwa toka juu ndio wamevamia maduka ya watu na kukusanya mali za kijinga kijinga (feki) toka kwa walalahoi na sio kufuatilia swala la Madwa na vyakula. Mkuu wangu hadi leo hii tunavyozungumza vyakula vingi ktk supermarkets nchini ni expired product ambazo wafanya biashara baada ya muda kupita kugongesha mhuri mpya..Just in case na they get away with it!..Nakupa haswa dataz za wabangaizaji mjini mkuu wangu hakuna cha Mkemia wala baba yake mkemia.. Huyo Mkemia alikufa kwa kihorohoro cha kesi iliyokuwa ikimkabiri yeye mwenyewe..
Hawa waheshimiwa CV zao kwa sasa zimeleta mushikeli ndani ya nchi hii kwahiyo hata wakitoa kitu tunajua kwamba wanaturudishia kile kidogo chetu.
Mkuu unajua mimi habari za udaku siziwezi, nimeandika hivyo kwa sababu sioni la maana hapa. Kama wewe unaujua ukweli weka wazi.Mkandara,
Does another wrong right the other. Huyo mkemia alikufa kwa kesi gani gani vile?