Hotuba ya kumaliza mazishi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hotuba ya kumaliza mazishi

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by ELNIN0, Dec 15, 2009.

 1. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #1
  Dec 15, 2009
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Hotuba ya kumaliza mazishi!!!

  Mwenyekiti wa kamati ya mazishi akainuka na kuanza kusema "kinachofuata sasa ndugu wafiwa na marafiki wa marehemu ni kusoma historia fupi ya marehemu tuliyemzika hapa leo. karibu ndugu uliyeandaliwa kwa shughuli hiyo"

  Ifuatayo ni historia fupi ya marehemu tuliyemlaza ktk nyumba ya milele.

  Marehemu alizaliwa juu ya mti ambapo mzazi wake alijihifadhi baada ya kukimbia mafuriko miaka 26 iliyopita, hakubahatika kupata kazi ya
  maana japo alisoma mpaka kidato cha tano, aliamua kuacha shule mwaka juzi baada ya kuona elimu haina mpango kwake. marehemu alikuwa kero kwa familia yake hasa kwa tabia yake chafu ya udokozi wa mboga, uongo, uvutaji bangi, ubakaji wa mifugo na baadae ushoga.


  Mimi binafsi mjomba wake nimefurahishwa sana na kifo cha marehemu huyu kwani alishawahi kunipakazia kuwa nimekufa kwa kipindu x2 kiasi kwamba ndugu wote wakakusanyika na kunililia msiba.

  Mtoto alitutia hasara sana kwani alikuwa mwizi wa vitu vya ndani na pesa! pia tumepoteza gharama kibao kumsomesha lakini aliishia kuwa shoga
  tangu tarehe 06/04/99. marehemu hakuugua bali kifo chake ni cha kujitakia kwani kajiua baada ya kukosa nauli ya kwenda Mombasa kuhudhuria onyesho la vikundi 3 vya mduara. Kwa niaba ya familia, wazazi na ndugu wa marehemu tunatoa pongezi kwa Mungu kwa kutupunguzia kero.
  asiilaze roho ya marehemu peponi wala asimpumzishe, kama kuna mkong'oto huko ampe kiaina.

   
 2. GP

  GP JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  hahahaaaaaa, sio mchezo.
  misiba mingi watu hawasemi ukweli kwenye kutoa wasifu wa marehemu!.
   
 3. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #3
  Dec 15, 2009
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hahahahaaah nadhani katika misiba mingi watu hushukuru kimoyomoyo!
   
 4. GP

  GP JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  kuna mshkaji alikua anamsumbua sana demu wangu longtime, si akafa bana!, nilishukuru kimoyomoyo.
   
 5. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #5
  Dec 15, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Duh huyu nae msomaji hafikirii atakufa siku moja?
   
 6. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #6
  Dec 15, 2009
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kwa kuwa ni burudani sawa. Lakini japo waafrika ni masikini wa pesa na mali, tumekuwa matajiri wa social cohesion. Hayo yaliyosemwa msibani hutayasikia kokote Afrika. Tunafundishwa naturally, kwamba hata adui yako akifa unasikitika na kushituka, maana inakukumbusha kwamba nawewe zamu yako ipo mbioni.

  Leka
   
 7. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #7
  Dec 15, 2009
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Tuwe na utamaduni wa kusema ukweli kuhusu wasifu na magonjwa yanayosababisha vifo kwa marehemu wetu, kama mwanao alikuwa kibaka toa wasifu wake bila kufisha hivyo hivyo kama alikuwa changu au shoga.

  Anaweza kuwa kafa kwa ngoma, lakini baba mzazi ukasema kapata ajali ya trekta au kagongwa na bajaji. Wabongo bwana...
   
 8. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #8
  Dec 16, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160

  Mkuu kuanzia hapo ukaanza kujimegea bila mshindani! raha ilioje!
   
 9. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #9
  Dec 16, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,381
  Likes Received: 22,250
  Trophy Points: 280
  Kwa kwere babangu hii ya reo imevunja santuriza mbavu zangu
   
 10. Guyana Halima

  Guyana Halima Member

  #10
  Dec 16, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 78
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ingekuwa ivyo, ukitokea msiba tungekuwa tunasubiri kwa hamu mtu azikwe ili tusikie fichua fichua za the late!!
   
 11. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #11
  Dec 16, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,421
  Likes Received: 3,770
  Trophy Points: 280
  Zamu zisitufanye tuseme uwongo.......... Kama uliweza kumchukia mtu akiwa mzima, kwa nini kifo kifute hayo yaliyopelekea kumchukia.....???? Ndiyo maana haishangazi TZ kukuta mtu kalazwa hospitali, ukimuuliza hali yake..... atakwambia mimi mzima..........YAANI KAMA VILE TUMEKARIRISHWA MAJIBU.......!!!!
   
Loading...