Hotuba ya dhihaka! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hotuba ya dhihaka!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mzee wa inshu, Feb 18, 2011.

 1. m

  mzee wa inshu Member

  #1
  Feb 18, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa mara nyingine tena nitoe pole kwa watanzania wenzangu waliopatwa na janga la mlipuko wa mabomu hapo juzi. Namuopmba mwenynezi Mungu awape faraja kwa rehema zake!n

  Nirejeree kauli ya serikali iliyotolewa na mh rais usiku wa kuamkia leo juu ya msiba wa kitaifa uliosababishwa namlipuko wa mabomu kwenye kambi ya JWTZ maeneo ya gongo la mboto.

  Nimwsikiliza sana hotuba hii na kwa makini, cha kusikitisha ni kuwa inaonyesha ni kwa kiasi gani ambavo raisi wetu hayuko makini ama bado anaendekeza mizaha katika mambo mazito yanayo gharimu uhai wa watanzania wenzake.

  1.Nilitegemea angetangaza hatua kali kuchukuliwa kwa watu wote watakao bainika ama kwa makusudi au kwa uzembe kusababisha tukio hili.

  2.Nilitegemea kutangaza kulipa fidia kwa majeruhi na ndugu wa marehemu na sio
  kifuta machozi kama alivo ahidi kwani hiyo ni lugha ya kisanii haiko wazi. kifuta j machozi inaweza kuwa hatt shiligi alufu moja(1000/=)

  3.Sikutegemea raisi kumwaga sifa lukuki kwa uongozi wa JWTZ kwa wakati huu ilihali akifahamu fika kuwa uzembe nakiburi cha kufanya kazi kwa mazoea ndivyo sababu ya majanga haya.

  Sikutegemea kuona mkuu wa majeshi na waziri wa ulinzi wanaendelea kukaa meza moja na mheshimiwa raisi mpaka muda huu. Wanaendelea vipi na kazi wasiyo iweza? Kiburi cha kutokujiudhuru wanakipata wapi? Kama hawataki kujiudhuru kwanini asiwatimue? je, wanafanya kazi kwa maslahi ya nani, wananchi au maslahi ya mtu binafsi?

  4.Nilitegemea rais na Baraza iake la usalama la taifa wangekaa usiku huo huo wa tukio na kuamka asubuhi ya jana na mkakati mzito nasio kulala na wake zao huku wananchi wakiteseka kwa uzembe wao.

  5.Rais anakumbuka leo kuomba msaada kutoka nchi rafiki juu ya namna bora ya kuhifadhi silaha na zana za kijeshi, hivi kumbe baada ya tukio la mabomu ya mbagala mlikuwa mnakunywa mvinyo bila ya kuchukua hatua yoyote ?

  6. Anaomba imani ya wananchi kwa serikali yake na jeshi na kutoa ahadi ya kuto kutokea tena kwa tukio kama hili.
  Je, ni mtanzania gani hivi leo ataamini ahadi hewa za vioongozi wasio aminika? Mheshimiwa unasahau kuwa wewe na mtoto wa mzee rukhsa mlisha wahi kutoa ahadi kama hizi wakati wa tukio la mbagala?

  Je, inapotokea kuwa mmeshindwa kusimamia kile mlicho ahidi kwa wananchi, nini tena mnasubiri au mnataka wananchi wawafanye nini?


  Mh Rais, wananchi wako tunakupenda sana ila aibu, upole, ukimya na kuwaonea haya watu wanao kuangusha na kuishi kwa gharama ya damu za watanzania wenzetu inatufanya na wewe tupatw na fikra za kukujengea chuki kama kikwazo kwetu.

  Mh, hao wanajeshi ni watanzania wenzetu, kama wanavurunda wachukulie hatua mara moja bila woga wasa kusita kwani hizo silaha hawanunui kwa pesa yao ya mfukoni, ni kodi zetu sisi masikini tuliojinyima kununua madawa ya hosipitali na vitabu vya watoto wetu mashuleni.

  ''TUNAJENGA NCHI KWA JASHO NA DAMU, WANAOBOMOA WASIACHIWE KAMWE''


   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  mimi simpendi km una mpenda ni wewe usiwasemee wananchi eti sisi wananchi wako tunakupenda nani anampenda mtu anayevurunda kila kitu. na wewe acha kuuma na kupulizia keshachemka basi tena.
   
 3. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Ukisikia raisi popompo duniani ni huyu wa kwetu.
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Damu waliyomwaga ni Kafara kwa taasisi ya Freemasons ambayo tunasikia 50% yao wanaabudu huko!
  Kila kitu kilikuwa calculated jamani, ndio maana hamtakaa msikie mtu kuwajibishwa, ndiyo masharti ya Ibada za huko!
   
 5. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
   
 6. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #6
  Feb 18, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo JK ni member wa freemansons?
   
 7. G

  Gathii Senior Member

  #7
  Feb 18, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 164
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nawapa pole wahanga wote waliothirika directly au indirectly.

  Nashindwa kuelewa kabisa,ila hii nchi yetu ni ya ajabu..kama huwezi ku-act basi bora unyamaze,unachosema kinaumiza watu zaidi.
  Kweli kuna sababu ya kulipongeza jeshi?hii inatoka kwa dhati kabisa moyoni mwake?-hata kama wasingepongezwa hivi kweli kabisa kuna mwanajeshi hata mmoja angelalamika kweli kwa kutopongezwa?

  Kweli Mwenyezi Mungu ametuumbia watu,daah!!!!

   
 8. Kbd

  Kbd JF-Expert Member

  #8
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 9, 2009
  Messages: 1,264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Muheshimiwa umeanza vizuri sana maana hata mimi ile hotuba yake imenikera sana sana sana. Inaendelea kutuonyesha how shallow the president is, he can not be bold on serious issues like this........in short he is incompetent. Sasa hapo kwenye blue muzee ume-generalize. Nakuhakikishia mimi simpendi hata kidogo, simpendi hata kumuona wala kusikia maneno yake. In fact i hate him with passion.
   
 9. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #9
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mambo ya USWAHIBA hayo. Atimuliwi mtu hapo.

  Je tanzania tutafika kweli?
   
 10. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #10
  Feb 18, 2011
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  kuna cha kuuliza tena hapo? pigia jibu mstari
   
 11. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #11
  Feb 18, 2011
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  hawezi, tena hatawezi, na hatokuja kuweza kuwatimua hao mafirauni kwa maana hilo ndilo kundi lililoiba
  kura pamoja so do we think it can be possible
   
 12. Panga la Yesu

  Panga la Yesu JF-Expert Member

  #12
  Feb 18, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata Mimi sikupendi JK lakini imeandikwa tuwaombee adui zetu, nitaendelea kukuombea uache upuuzi wako
   
 13. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #13
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Bwn PJ kwa kuongezea wandugu si mnakumbuka mnajimu mkuu nchi hii ya Wadanganyika Sheik Yahaya kipindi cha uchaguzi si alihaidi kumlinda Mh Raisi kwa majini?????????
  Sasa huyo mkuu kwennye njego wa Magogoni aliwahi kuakanusha hiyo kauli ya kulindwa na majini??????????? Kama analindwa na majini je, yatafanya kazi bila sadaka????????
  Kwa hiyo majibu ya maswali tunayo majini yanakunywa damu ya watu, matambiko sadaka lazima zitolewe, haijalishi kivipi, kama tulikuwa hatujui funguka macho. Huo ni ulimwengu wa kiroho, mapepo yanavuna watoto na watu wa Tanzania!!!!!!!!!!!! Huyo Raisi wetu akanushe kulindwa na majini, aruhusu ibada za nguvu zifanyike kuondoa hayo majini Ikulu, KWA KIBALI CHAKE na yeye mwenyewe ashiriki, watu wa Mungu aliye hai wataomba na kufanya ibada huko Ikulu, kutimua hayo madudu yanayoleta mabaraa na maangamivu ya watu. Na kwa jina la Bwn Yesu nakuhakikishia majini yataondoka na nchi itapona majanga ya ajabu!!!!!!!!!!
   
 14. s

  smz JF-Expert Member

  #14
  Feb 18, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hata kama ubavu wa kuwatimua hana, kulikuwa na haja gani ya kuwasifia?? Maana mtu anasifiwa kwa kufanya jambo jema. kwa maana hiyo hawa JW kuacha mobomu yalipuke yenyewe na kuua watu ni jambo jema hadi kusifiwa na mkuu wa nchi, kwekli??
   
 15. m

  mzee wa inshu Member

  #15
  Feb 18, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  '' wananchi wakidai haki yao,risasi, mabomu ya machozi vinatumika dhidi yao na hata kuwajeruhi na kuwauwa''


  ila ''wakubwa wakivurunda mambo na kusababisha hasara na vifo kwa wananchi wanapongezana kwa kugonga bilauri za mvinyo na bia''
   
 16. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #16
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Ni jema kwa Kikwete na Serikali yake......
   
 17. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #17
  Feb 18, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  Moyo wangu hauamini kabisa kama mabomu haya yamelipuka bahati mbaya... Something fishy is going on!...
  Ona sasa, tushasahau Dowans....waziri mkuu kudanganya bunge... Upepo wa
  Nguvu ya uma...
   
 18. m

  mzee wa inshu Member

  #18
  Feb 18, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ''stand with any body who stands wright, stand with him while he is wright but part him when he goes wrong'
   
 19. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #19
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Akasema ''Shida zenu ni shida zangu pia'' sijui anaujua mgao wa umeme?
   
 20. d

  dorry Senior Member

  #20
  Feb 18, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  swala la kikwete kupendwa kupendwa na wananchi asahau labda hao mapopompo wenzake. Jk ni janga la kitaifa, pasua kichwa. alipofikia sasa panatosha unasifia wauaji wa raia!!! This is beyond the tolerable.
   
Loading...