Hotuba nyingi za viongozi wa Afrika kwenye mkutano wa UN zimejaa malalamiko

Watawala kutoka Afrika hasa kusini mwa Sahara desert,ni wajinga wa kutupwa,hizo hutuba uko UN ni ishara ya ujinga wao,ambao wamejikita katika kutoa lawama badala ya kutafuta suluhu ya matatizo,wao wanawaza chaguzi tu kuliko kutatua matatizo ya wananchi.
sio wote
 
Viongozi wa nchi zote za dunia wanakutana Marekani kwenye mkutano mkuu wa Baraza la usalama la umoja wa mataifa (General Assembly of United Nations). Hotuba nyingi za viongozi kutoka Afrika ni za malalamiko kuhusu nchi za Magharibi na Marekani kama chanzo Chao kikuu Cha matatizo kwenye nchi zao. Hotuba nyingi za viongozi wetu ni kuhusu wazungu kutotimiza ahadi zao za kutoa mapesa kwa nchi za Afrika kugharimia miradi Yao, madeni makubwa wanayodaiwa na ukosefu wa masoko na technology.

Bahati mbaya sijamsikia kiongozi wetu hata mmoja akizungumzia shida wanazozisababisha wao wenyewe kama vile:
1. Kuiba kura kwenye chaguzi
2. Kung'ang'ania madarakani
3. Wizi wa mali za wananchi wao na ubadhilifu.
4. Matumizi mabaya ya mikopo wanayopewa.
5. Kushindwa kukusanya kodi
6. Rushwa kwenye nchi zao.
7. Viongozi kujiwekea kinga za kutokushitakiwa.

Bahati mbaya nchi za Magharibi wanayajua madhaifu yote ya viongozi wa Afrika, ndio maana wakati wa hotuba za viongozi kutoka Afrika Wazungu wengi wanapuuza na wanatoka nje.

Afrika hawana mshipa hata mmoja wa aibu, kazi Yao ni kuwanyooshea vidole nchi za Western na kusahau udhaifu wao kwanza.

Mfano, nani anawazuia nchi za Afrika kuuziana bidhaa wao kwa wao kwa kutumia fedha zao. Nani kawazuia waafrika kuondoa VISA kati ya nchi na nchi ili watu Waafrika wawe huru kwenda na kutoka nchi nyingine ya ya Africa kufanya kazi au biashara? Nani kawazuia waafrika wasilime chakula Chao? Nani kawazuia kukusanya kodi?
Hivi wewe hujui kwamba wazungu ndio wezi wakubwa, hujui bara la Afrika wameiba mali nyingi sana ndio hayo maendeleo yao uyaonayo. Acha walalamike buana.
 
huyu wazungu hawawezi kumpenda, kumvumilia wala kumsikiliza, hata mkutano wa mwaka uliopita ambao ulikua mkutano wake wa kwanza aligonga vyuma haswa..

Huyu jamaa anagongelea misumari ya moto sana, na ndie pekee hana mchezo wala hatanii angependelea usawa kwenye majukwaa ya maamuzi tangu kupanga, kuamua na kutekeleza.
 
ni heri ya yule anaetoa kuliko anaepokea. Wazungu hawatoi misaada bali wanatoa chambo. Kuna wazungu wengi huko kwao ambao ni maskini sana na wenye uhitaji wa kusaidiwa lakini hawapewi misaada hiyo, iweje wakupe msaada wewe mwafrika mvivu mwenye ardhi kubwa ya kulima, kufuga na kuvua? think critically blaza.
Ndo maana nimesema wazungu wanatoa ili kuchukua baraka zetu.
Mkono utoao ni sawa na bomba lililowazi limwagalo maji.

God bless the hand that give.
Ni heri kutoa kuliko kupokea.
 
Hivi wewe hujui kwamba wazungu ndio wezi wakubwa, hujui bara la Afrika wameiba mali nyingi sana ndio hayo maendeleo yao uyaonayo. Acha walalamike buana.
Walichoiba hata robo hakijafika ukilinganisha na mali chekwa tele zilipo.
Achaneni na propaganda za chuki za mapanafricanist
 
actually,
kwa tones za viongozi wengi wa Africa, hawako tena na interests za misaada ya ng'ambo wanahitaji tu usawa katika kupanga, kuamua na kutekeleza agenda za pamoja kwa maslahi ya wote.
kwani hawajui kuwa umoja wa mataifa unamilikiwa na nchi za Magharibu hasa Marekani? Kama wanaona umoja huu hauko sawa je, umoja wao wa AU unasemaje na kuamua nini? Kwanini kila nchi inakwenda kusema jambo lilelile kwa kulalamika na kutoa lawama? Hawatasilizwa kama hawataziweka sauti zao zote kwenye mdomo mmoja wa African Union useme na kuamua kama Bara.
 
Walichoiba hata robo hakijafika ukilinganisha na mali chekwa tele zilipo.
Achaneni na propaganda za chuki za mapanafricanist
Tuache kulinda mali iliyopotea bali iliyobakia. Kuna siku nilisema Afrika tuzifute kumbukumbu zote za biashara ya utumwa na ukoloni kwenye bara letu. Tuyabomoe majengo yote yanayotunza kumbukumbu hizi na kujenga shule, mahoteli, sehemu za starehe na vitu vingine vinavyofurahisha kwenye maeneo hayo. Kuendelea kutunza kumbukumbu za kijinga kwa vizazi vyetu ni kuviambukiza ujinga na unyonye wajukuu zetu.

Tuachane na walizoiba tuanze kulinda hizi zilizobakia. Wazungu bila kuiba mali zetu hawezi kuishi salama, watatupiga tena.
 
kwani hawajui kuwa umoja wa mataifa unamilikiwa na nchi za Magharibu hasa Marekani? Kama wanaona umoja huu hauko sawa je, umoja wao wa AU unasemaje na kuamua nini? Kwanini kila nchi inakwenda kusema jambo lilelile kwa kulalamika na kutoa lawama? Hawatasilizwa kama hawataziweka sauti zao zote kwenye mdomo mmoja wa African Union useme na kuamua kama Bara.
sawa ngoja tujaribu ndio mwanzo. Nadhani nawe unakiri kila kiongozi wa Africa analalamika, huo ni mwanzo wa kua na Sauti moja yanye nguvu kama waafrica wote wanalalamikia kitu icho icho na huo ni mkakati pia.

wakati muafaka hawataenda wote ataenda moja tu kuwakilisha sauti ya Africa nzima.
 
Shida yao itakuwa ni nani atalifunga paka kengele? Kuna watu walijaribu kukaribia kulifunga paka kengele lakini walikiona cha moto; akina Nkrumah, Gadafi na wengine lukuki.
 
Tuache kulinda mali iliyopotea bali iliyobakia. Kuna siku nilisema Afrika tuzifute kumbukumbu zote za biashara ya utumwa na ukoloni kwenye bara letu. Tuyabomoe majengo yote yanayotunza kumbukumbu hizi na kujenga shule, mahoteli, sehemu za starehe na vitu vingine vinavyofurahisha kwenye maeneo hayo. Kuendelea kutunza kumbukumbu za kijinga kwa vizazi vyetu ni kuviambukiza ujinga na unyonye wajukuu zetu.

Tuachane na walizoiba tuanze kulinda hizi zilizobakia. Wazungu bila kuiba mali zetu hawezi kuishi salama, watatupiga tena.
Umenena maana hayana msaada wowote wenzetu wa Asia sidhani Kama Wana matakataka ya hayo thus Wana maendeleo wao walishavuta hizo kumbukumbu za kipumbavu
 
Rais wa nchi kufunga safari toka Africa hadi US ili kuhutubia nusu saa ni matumizi mabaya ya muda na fedha ndo maana viongozi wanaojielewa huwa hawaendi wanatuma wawakilishi tu, unaenda when it's really necessarily.
 
Umenena maana hayana msaada wowote wenzetu wa Asia sidhani Kama Wana matakataka ya hayo thus Wana maendeleo wao walishavuta hizo kumbukumbu za kipumbavu
Tunahifadhi ujinga kuja kuwaonyeaha Wazungu namna walivyotutweza inatusaidia nini? Waafrika ni wajinga kupindikia. Tunazalisha kikazi dhaifu sana. Hii ni sawa na baba kutunza picha za mkasa wa kulawitiwa na rafiki zake ili aje awaonyeshe watoto na wajukuu zake.
 
Rais wa nchi kufunga safari toka Africa hadi US ili kuhutubia nusu saa ni matumizi mabaya ya muda na fedha ndo maana viongozi wanaojielewa huwa hawaendi wanatuma wawakilishi tu, unaenda when it's really necessarily.
90% ya viongozi wetu wameenda kule kama sehemu ya ukwapuaji, spending na kufanya shopping. Na wengine ni njia rahisi ya kwenda kufungua account kwenye mabenki ya Marekani na Ulaya kuficha pesa zetu.
 
ni kweli wamelalama sana.

Lakini pia yapo mambo ya msingi sana na ya maana wanayo yalalamikia mathalani kuhusu udhaifu wa taasisi za kidunia kama vile UN na Barazani la usalama katika kuchukua hatua katika majanga na migogoro duniani,

Kadhalika kutokua na usawa wa uwakilishi kwa Taasisi za kidunia kama vile WB, IMF, UN Security Council baina ya Africa, America, Asia, Ulaya n.k
hii imezorotesha utekelezaji wa mambo mengi sana na hata imefikia mahali inaonekana mfano anachafua mazingira mwingine halafu mwingine anapewa fedha za kutunza mazingira.

Rejea 17 Sustainable Development Goals utagundua na kubaini vizuri sana malalamiko yenye mantiki ya viongozi wa Africa huko UN.
Shukran kwa bandiko.
Una hoja nzuri sana mkuu, ukweli ni kuwa hili bara linapuuzwa sana kwenye kila kitu, limegeuzwa eneo la majaribio ya chanjo na kuvunia rasilimali tu tena kwa bei sawa na bure.
 
Lawama zitabaki palepale kwa nchi za kibeberu, hawa jamaa huwa hawataki kiongozi wa Africa anayejielewa, ukiingia madarakani ukawa na msimamo mkali wa kizalendo watakuletea zengwe tu! Hasa wakiona unaleta maproject makubwa ya ukombozi wa Kiuchumi ujue kabisa roho yako umeiweka rehani au nchi yako itadhoofishwa na makundi ya kigaidi, au kuwekewa vikwazo vya kijinga kijinga tu. Kama unataka ku-transform nchi Yako jitoe sadaka kwaajili ya Nchi yako.
Kweli mkuu tatzo viongoz wetu wengi hawawezi kujitoa sadaka.
 
Nimeona Hadi hao wanajeshi kina doumbia wa guinea anasema democracy imekuwa msamiati kwao ,kwmab Africa swla la democracy haliwezekani analazimisha kuaminisha kuwa waafrica wanapazwa kuchagua njia Yao ya kujitawal na siyo hyo democracy ambayo imekuwa Ni utamaduni wa kimagharibi
Anazo facts, unadhani mfumo wa demokrasia umeisaidia Africa?
 
Hiyo ni kweli, hata JPM alipojifanya ananunua ndege kwa pesa tasilimu na kujenga barabara na reli ya umeme, mabeberu wakamtangazia kuwa Tanzania imeingia uchumi wa kati. Kuingia uchumi wa kati maana haye huhitaji misaada wala mikopo ya riba nafuu inayotolewa kwa nchi maskini. Hii ilikuwa njia ya kumkomesha na wala sio kweli kwamba uchumi wa Tanzania umekuwa kwa kiasi hicho. Lakini, hii haisababishi nchi kuingia mikataba mibovu ya uwekezaji kwenye madini, gesi, nk, hiyo haisababishi nchi kushindwa kukusanya kodi kikamilifu, kupanga miji na ardhi yake kwa matumizi mbalimbali, kuzoa takataka au ...... Leo hii vinapimwa ardhi ya viwanja tu lakini haipimwi ardhi kwaajili ya kilimo, ufugaji na viwanda. Ardhi ya kilimo inageuzwa kuwa ardhi ya makazi huko vijijini, sijui watalima wapi.
Kwakweli hili jambo la kung'ang'ania kupima viwanja kwa ajili ya makazi tu ni miongoni mwa jambo linalonisikitisha sana. Kunasehemu nilinunua ekari kumi miaka Saba iliyopita na ilikuwa nje mji kabisa na hata Sasa ndio mji unasogea na bado hakujakuwa na watu wengi kivile. Cha kunishangaza wamekuja watu wa ardhi kwa ajili ya kurasimisha ardhi kwa wananchi ila wanachonikomalia ni kwamba hapo nilipo hawawezi kunipimia ardhi yote kama eneo la ufugali Wala kilimo na wanadai ni lazima nipime viwanja coz Hilo eneo sio rasmi kwa kilimo Wala ufugali Bali ni eneo la makazi. Kwakweli sijawaelewa naendelea kufuatilia kuujua ukweli na kiukweli wananishangaza sana.
 
90% ya viongozi wetu wameenda kule kama sehemu ya ukwapuaji, spending na kufanya shopping. Na wengine ni njia rahisi ya kwenda kufungua account kwenye mabenki ya Marekani na Ulaya kuficha pesa zetu.

Exactly. Kwenda hii mikutano uchwara ni vacation tu haina tija yeyote ile.
 
Back
Top Bottom