Hoteli ya nyota Tatu inajengwa Chato, Wana-CCM mnafurahishwa na kitendo cha kupeleka kila mradi wa ujenzi Chato?

Mnakaa kujadili Hoteli ya nyota 3? JF inabaki kuwa kioja/kituko. Lazima mfahamu kitu kimoja ndio sababu kunakuwa nna mabadiliko ya viongozi wa ngazi za juu. Hivi nyinyi na akili zenu zote mlifikiri hoteli za nyota 3 ni za miji flani flani tu? Wacheni wivu. Chato nao wanastahili kuwa na Hoteli hata ya nyota 5 nk.

Kama mna ushahidi kuna mkono wa JPM au kwa njia moja au nyingine ametumia rushwa wekeni ushahidi wacha - neni na majungu.
 
Ujasema hospital gani kuwa wazi au unamaanisha mloganzila hospital Kama ni hii ipo kibamba daressalaam.na lililokuwa jiji halijatoa RAIS.kinachowatatiza watu ni mfulilizo wa miradi ktk WILAYA moja.hapo tunajiaanda na ujenzi wa chuo Cha utumishi wa umma soon mh Mkuchika atatembelea mradi.
Mimi ushauri wangu ni kwambam
Kigoma kuna mradi gani ? mtwara ? songea ? we mtoto wa magufuli eti ?
Mtwara wanayo mbuga ipi? Kigoma - mradi wa machikichi uliofunguliwa na Mh. Kassim Majaliwa umefika wapi? Songea - Makaa ya mawe yanaendelea je?
 
Hoteli haitakaa iishe

Na kwa bahati mbaya ikaisha,no one will book any room there

Hoteli itageuzwa hosteli

I wonder who is the owner?Mawe?

This is useless,Chato will never progress,no one will buy anything there,it will never be an economic powerhouse sababu watu wana negative feelings about Chato....
Sijui TISS huwa wanamshauri nini Mzee?
 
View attachment 1715798
Maelezo ya Picha: Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja(Kulia) akikagua hoteli ya nyota tatu inayojengwa na Hifadhi za Taifa Tanzania inayojengwa Wilayani Chato mkoani Geita.
Mwalimu Nyerere akijua kabisa kuwa kuku wa taifa lazima aliwe na wote, aliamua almasi inayochimbwa Shinyanga Mwadui ikakatwe Iringa, ili Wanyalu nao wafaidike na madini hayo.

Hakupeleka kiwanda Cha Tancut Almasi Mara wala Butiama.
Magufuli amekuwa ni mtu wa kupendelea kwao tu utadhani Tanzania ni Chato tu.

1. Uwanja wa ndege mkubwa umejengwa Chato
2. Wanyama wamesombwa huko Serengeti, wamepelekwa Chato.
3. Uwanja mkubwa wa michezo kujengwa Chato.
4. Hospitali ya Kanda ya Ziwa imejengwa Chato.
Je, wanaccm mmeshindwa kukemea upendeleo huu?

Mjulisheni Mwenyekiti wenu kuwa anachokifanya sio uzalendo, ila ni ubaguzi. Anawabagua watu wasio wa Chato.

Kuku wa Taifa lazima aliwe na wote, hata watu wa Ileje na Tandahimba wanahitaji kwao kujengwe, sio kila kitu Chato tu

===

Naibu Waziri wa Utalii Mary Masanja akagua miradi ya utalii Geita​

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja amefanya ziara katika Mkoa wa Geita ambapo pamoja na mambo mengine amekagua miradi mbalimbali ya kiutalii inayotekelezwa na taasisi za Wizara ya Maliasili na Utalii mkoani humo, anaripoti John Bera (WMU) Geita.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (katikati) akiwasili kukagua hoteli ya Nyota 3 ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ( TANAPA) inayojengwa wilayani Chato mkoani Geita wakati wa Ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya mkoani Geita. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Eng. Charles Kabeho na kulia ni Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi Kanda ya Magharibi, Martin Loibooki.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Robert Gabriel kuhusu mpango wa Wizara ya Maliasili na Utalii wa kutaka kuanzisha Utalii wa Madini katika mkoa huo wakati wa Ziara yake ya Kikazi mkoani humo.

Akiwa katika ziara hiyo amefanya mazungumzo na viongozi wa Serikali wa mkoa na wale wa taasisi zilizo chini ya wizara kuhusu namna bora ya kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana katika mkoa huo.

Aidha, Mhe. Masanja ametembelea Mradi wa Ujenzi wa hoteli ya Kitalii ya Nyota 3 inayojengwa wilayani Chato mkoani Geita na kuagiza ujenzi wa hoteli hiyo ukamilike haraka ili watalii waanze kupata fursa ya kutumia huduma za malazi katika hoteli hiyo na kutembelea hifadhi mbalimbali zilizopo Kanda ya Ziwa.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kulia) akiwa anashuka kwenye hoteli ya Nyota 3 ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ( TANAPA) inayojengwa wilayani Chato mkoani Geita wakati wa Ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya mkoani Geita. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Eng. Charles Kabeho.

Amesema, Wizara ya Maliasili na Utalii itaendelea kushirikiana na uongozi wa Mkoa wa Geita kuhakikisha shughuli za utalii zinasonga mbele huku akitoa rai kwa viongozi hao kuweka mkazo katika zao la asali ambalo amesema likisimamiwa vizuri litaongeza mapato.

"Tuhamasishe zao la asali linalotokana na nyuki, sasa hivi kuna mnyororo mkubwa wa thamani ambao Serikali inaendelea kuupigania kwenye mazao ya misitu, hii itasaidia wananchi kuongeza kipato pia pato la Taifa,"amesema Mhe. Mary.

Aidha, ameongeza kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii iko katika mpango wa kuanzisha Utalii wa Madini ambao kwa Kanda ya Ziwa utasaidia kuongeza idadi ya watalii na mapato.
Haya ungeyasema yalipokuwa yanafanywa huko kwenu
 
Hoteli haitakaa iishe

Na kwa bahati mbaya ikaisha,no one will book any room there

Hoteli itageuzwa hosteli

I wonder who is the owner?Mawe?

This is useless,Chato will never progress,no one will buy anything there,it will never be an economic powerhouse sababu watu wana negative feelings about Chato....
Kuna kila dalili isikamilike
 
Kuna kila dalili isikamilike
... mzee alikuwa na dreams nyingi sana; kwenye ziara yake ya mwisho Kagera aliwaambia wana-Karagwe kwamba baada ya kustaafu makazi yake yangekuwa huko. Dah; kumbe Mungu ana plans zake.
 
Back
Top Bottom