Hoteli ya nyota Tatu inajengwa Chato, Wana-CCM mnafurahishwa na kitendo cha kupeleka kila mradi wa ujenzi Chato?

Wabunge wote wako pale kwa hisani yake. Watathubutu kusema chochote? Jamaa aliona mbali. Alijua akiwaweka kwenye nafasi hizo hawawezi kufungua mdomo kwani mtu hawezi kukata mkono unaomlisha. Na hii miradi inaashiria kitu kimoja: Bado yupo sana kuhakikisha ameikamilisha na kuisimamia. Yupo beyond 5 years to come. Labda watanzania wawe wakali kweli kweli tena kweli ashindwe kujiongezea muda. Ila bado ataweka kikaragosi chake atakachokiendesha remotely.
umemroga tayari.maneono yako haya kijana ymemkata
 
Hivi Mheshimiwa Rais wangu ingekuwa ndo ametoka Bagamoyo ambako ni very justifiable kwa miradi kama hii, si wangejenga hadi mahotel ya Nyota 5?! Si wangesema Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam umejengwa sehemu iliyobana kwahiyo uhamishiwe Bagamoyo?! Si wangesema msongamano wa magari kutoka Dar to Tegeta ni mkubwa sana kwahiyo ijengwe barabara ya juu kwa juu kutoka Mwenge hadi Bagamoyo?! Si wangesema ijengwe satellite city Bagamoyo ili kui-backup Dar es salaam?! Si wangehamishwa wanyama kutoka kila kona kupelekwa Saadan?! Hivi hata ile Mlonganzila Hospital ingejengwa Bagamoyo?

Ukweli ni kwamba, Bagamoyo ingekuwa na vigezo vingi vya kuhalalisha massive investments, vigezo ambavyo kwa Chato hata mtoto mdogo huwezi kumshawishi. Hivi kuna mtu kawahi kufika Masasi humu?! Kwa mara ya kwanza, nilienda Masasi last week. Ni mji mkubwa, umechangamka kweli kweli. Hivi Mheshimiwa Rais wetu angekuwa ndo Mkapa Masasi hivi sasa si ingekuwa ndo Manispaa huku ikipelekwa miradi kadhaa ili hatimae iwe ndo center ya kusini?! Kinyume chake, ukitembea Masasi unaona wazi yaliyopo hayatokani na upendeleo wowote wa serikali bali uchakalikaji wa wananchi wenyewe.
basi ujue amesha nyamazishwa nchi ina wenyewe hii
 
Hizi ni comments za mwisho mwisho kabisa .Ni kama vile zilikuwa ni unabii!
Enzi hizo watu wamechoshwa na kukata tamaa kweli kweli!! 😃😃 Yaani kama unamuombea Mubutu aanguke vile tena haraka iwezekanavyo!! Ila mwisho wa siku ndiyo hivyo tena!

Pole nyingi kwa wafiwa.😇
 
Kikwete alopojenga msoga tulilalamika
Mkapa hakujenga kwao tulilalamika
Jpm kajenga kwao tumelalamika
Sisi ni watu wa kulalamika tu

Ova
 
Naona sasa hio hotel wanapata watalii kutoka Dubai,US,UK na tunaingiza mabilioni ya $$$$$.
 
Back
Top Bottom