Nathubutu kusema kuwa chuo hakina serikali ya wanafunzi, kwani uchaguzi ulifanyika mwaka huu, lakini ikatokea mizengwe, uchaguzi ule ukafutwa, hivyo ikateuliwa serikali ya muda mpaka uchaguzi mwingine utakapofanyika, hiyo serikali ya muda hatujui inafanya nini kwani hali inazidi kuwa mbaya na hatuoni wanachofanya.
Mbona unaongea sana walikunyima fomu za ugombea nini?
We waonesha ni moja wa vijana wanakulaga kwa mama mjeshi pale mzambarauni,soma dogo wacha siasa.
Aisee, umenikumbusha sana kwa mama mjeshi, siku nyingi sijamuibukia, ngoja leo ntaelekea kumcheki! hapa sio siasa Dogo, ila ukweli lazma tuuzungumze, hostel tunazoishi "value for money" haipo kabisa, na serikali ya wanafunzi ambao ndio watetezi wetu wakuu haipo, kwani waliopo ni wale walioteuliwa kwa muda, na hawatusaidii. Then sijawahi hata kuomba nafasi yoyote ya uongozi hata Monitor darasani sikuwahi kuomba.
Siasa zinamaliza Elimu ya Tanzania!
Ninavyofahamu mimi mojawapo ya vigezo vya mwanafunzi kufanya vizuri katika masomo yake inachangiwa pamoja na mazingira anayoishi na ya kujifunzia. Hali hii ni tofauti sana katika chuo cha Mipango hasa kwa wanafunzi wanaishi "Furaha Hostel" kwani mazingira ya eneo hilo ni mabovu, hosteli hizo vyoo vyake havina milango, havina taa, kolido zake ikifika usiku ukiwa unapita ni kama upo shimoni kwani hakuna taa hata moja, milango yenye vitasa inahesabika na wafanya usafi ni kama watu wanaojifunza kazi yao kwani ukiambiwa kuwa pamesafishwa huwezi amini na ni kawaida kukuta madimbwi ya maji chooni wakati mfanya usafi kamaliza kazi yake, mbaya zaidi ada kwa ajili ya Accomodation imepanda kutoka 250,000/- kwa mwaka jana mpaka kufikia 350,000/-
Wana JF hebu nisaidieni gharama ya accomodation inayolipwa inaendana na huduma tunayopata? hapa "Value for Money" ipo kweli?