itagata
JF-Expert Member
- Sep 4, 2011
- 209
- 71
Ninavyofahamu mimi mojawapo ya vigezo vya mwanafunzi kufanya vizuri katika masomo yake inachangiwa pamoja na mazingira anayoishi na ya kujifunzia. Hali hii ni tofauti sana katika chuo cha Mipango hasa kwa wanafunzi wanaishi "Furaha Hostel" kwani mazingira ya eneo hilo ni mabovu, hosteli hizo vyoo vyake havina milango, havina taa, kolido zake ikifika usiku ukiwa unapita ni kama upo shimoni kwani hakuna taa hata moja, milango yenye vitasa inahesabika na wafanya usafi ni kama watu wanaojifunza kazi yao kwani ukiambiwa kuwa pamesafishwa huwezi amini na ni kawaida kukuta madimbwi ya maji chooni wakati mfanya usafi kamaliza kazi yake, mbaya zaidi ada kwa ajili ya Accomodation imepanda kutoka 250,000/- kwa mwaka jana mpaka kufikia 350,000/-
Wana JF hebu nisaidieni gharama ya accomodation inayolipwa inaendana na huduma tunayopata? hapa "Value for Money" ipo kweli?
Wana JF hebu nisaidieni gharama ya accomodation inayolipwa inaendana na huduma tunayopata? hapa "Value for Money" ipo kweli?