Ndugu jamaa na marafiki kama na nyie limewakuta hebu tuambiane nini tatizo maana kila nikienda kupima maralia kwenye hizo HOSPITALI naambiwa sina maralia wakati nikijiangalia ninaumwa kweli.
Naamua kwenda maabara au hospitali binafsi, huko napatiwa tiba kisha narudi nikiwa na amani.
Jana usiku nilimpeleka mke wangu zahanati akiwa hoi na dalili zote za maralia lakini cha kushangaza naambiwa hana maralia, sikutaka kusubiri nikaamua kumpeleka maabara huko akakutwa na maralia, nashukuru kwa sasa anaendelea vizuri mseto unamsaidia.
Si rahisi kutoa hukumu sahihi kati ya taasisi mbili husika.
Hakuna dalili zenye hati miliki ya malaria. Tuna shida ya maambukizi mengine yenye dalili kama malari.
Mfano: Maambukizi ya Virusi na Maambukizi ya bakteria.
Tunajua virusi kulingana na aina , ukipata dawa ya kupunguza maumivu utapata nafuu. Hivyo, lolote laweza kuwa kweli kwa wahusika wote. Hakuna haja ya kuhukumu kwa ujumla.
Moja ya kitu ambacho tunashindwa kukielewa au tukipuuza tu ni kuwa:
1: Jukumu la kuutambua ugonjwa kwa mgonjwa hutegemea ushirikiano kati ya mgonjwa na mtoa huduma wake.
Hii huusisha uchukuaji wa historia/kutoa taarifa sahihi, ukaguzi wa mwili/kutoa ruhusa ya ukaguzi , kujua matarajio ya mgonjwa/wagonjwa huja na malengo yao, kupata tathmini ya nini kinaweza kuwa tatizo, kufanya vipimo na kupata majibu.
Maamzi ya yanayofuata ni kufahamu ugonjwa.
Baada ya kufahamu haya, kinachobaki ni kupewa majibu na kuelezwa aina ya tiba na matarajio hasi au chanya kutokana na ugonjwa na tiba husika.
Kuna magonjwa hufahamika kupitia historia tu, kuna magonjwa huitaji historia na ukaguzi. Kuna wakati utahitaji kipimo kuthibisha au kukanusha yale yaliyoko mikononi mwa mtoa huduma.
2: Hakuna mtoa huduma au mgonjwa atajisifu kuweza kutoa suluhisho la kiafya la mtu bila mahusiano mema kati ya watajwa hapo juu. Yote tunayotofautiana ni ubinadamu tu. Vivyo hivyo kwa watoa huduma ndani ya taasisi husika, ushirikiano na uwajibikaji wa kila mmoja kwa mujibu wa miongozo ni kitu muhimu sana ili kuleta ufanisi chanya.
Kuna wagonjwa wanajua magonjwa yao hasa ya kudumu pamoja na dawa na madhira yake kuzidi hata madaktari.