Hospitali ya Taifa Muhimbili yawezesha uanzishwaji wa Kliniki ya Himofilia na Selimundu Kigoma RRH

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Dkt. Jesca Leba ameishukuru Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kuwezesha upatikanaji wa Kliniki ya Himofilia na Selimundu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma - Maweni.

ff298404-054a-4b2c-b7e9-5769bce07a62.jpg


Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba - MNH, Dkt. John Rwegasha

Dkt. Jesca ambaye alimuwakilisha Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya, Prof. Pascal Rugajo katika uzinduzi rasmi wa Kliniki hiyo amesema uwepo wake katika Kanda ya Magharibi utasaidia wagonjwa kupata huduma karibu badala ya kuzifuata mbali.
818d04e3-2e15-4adc-b5e4-16456f58d4cf.jpg

48c3d83b-5119-4f1c-8ed7-4f828d3cd32a.jpg

Upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Maweni, Dkt. Stanley Binagi amesema MNH kupitia mradi wa kuongeza kasi ya upatikanaji huduma kwa wagonjwa wenye changamoto ya magonjwa ya damu imewezesha ukarabati wa jengo, upatikanaji wa vipimo, vifaa vya mazoezi na dawa kwa wagonjwa wa Himofilia.

Dkt. Binagi amesema "Kabla ya uzinduzi huu yalitangulia mafunzo kwa watoa huduma yaliyotolewa na wataalamu wa MNH kuhusu na namna ya kuwatambua na kuwahudumia wagonjwa wa Himofilia kwa wataamu wa maweni na hospitali za jirani, jambo ambalo litawasaidia kumudu uendeshaji wa kliniki hii."

Upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. John Rwegasha ambaye alimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji amesema Muhimbili itaendelea kutekeleza jukumu la kuzijengea uwezo hospitali za rufaa na mikoa ili kuhakikisha kuduma za kibingwa zinafika karibu na Wananchi.


Dkt. Stanley Binagi, Mganga Mfawidhi Kigoma RRH

Mganga Mkuu - Mkoa wa Kigoma, Dkt. Jesca Leba
 
Back
Top Bottom