Hospitali ya mkoa wa Njombe kukosa mortuary, ni aibu kwa mkoa hata taifa!

accused

JF-Expert Member
Aug 7, 2015
2,496
2,743
Mh. Sara Dumba (R.I.P) anazikwa Leo jijini Dar es salaam huku mwili wake ukitokea Njombe. Kilichonishangaza ni kua mh alifia Njombe mjini lakini mwili wake ukahidhiwa hospital teule ya Ilembula.

Hapa ndio ikanibid kufuatilia kulikoni. Jibu nlilopata ni kua hospitali ya mkoa wa Njombe (Kibena) haina uwezo wa kuhifadhi maiti. Kutoka Njombe hadi Ilembula ni zaidi ya kilomita 60.

Swali likanijia, hivi mkuu wa wilaya alishindwa kuhakikisha mafriji yanapatikana ktk hospitali ile kubwa ilopewa hadhi ya Regional hospital?

Vipi kuhusu mkuu wa mkoa na wizara ya afya? Mkoa hauna Pesa za kuhakikisha mortuary inafanya kazi vizuri? Hii ni aibu na maut zitawaumbua watawala.
 
Wananchi wakifa nao miili yao inahifadhiwa Ilembula?

Hiyo hatari makao makuu ya mkoa haina hospitali inayoweza kuhifadhi maiti.
 
Mambo mengine mnashangaza kuandika humu jf. Mikoa mingapi ya zamani inasuasua katika huduma mbali mbali za kiafya sembuse Njombe iliyopatikana juzi. Jiulizeni kwa upana zaidi kwa nini huduma ziko duni kwa miaka mingi licha ya ukweli kuwa nchi ina rasilimali nyingi kupindukia. Wizi na ufisadi serikalini.
 
Sijasema mortuary haipo, hiyo ipo lakini friji hakuna. Sasa kua na mortuary halafu no friji hyo ni sawa na kusema una gari elhal gari yako haina injini.

Naamini kabisa msafara ulopeleka mwili Ilembula kutoka Njombe na kuurejesha Njombe kuuaga ulikua na gari si chini ya 10 tena land cruiser, hyo gharama ya msafara tu ingesaidia bugdet ya kafriji japo kamoja.

Watawala wetu na planning officers tulionao ktk nchi hii ni bure kabisa.
Ummy Mwalimu anakomaa na machangudoa mjini badala ya kujidili na mambo ya msingi kama haya.
 
Mh. Sara Dumba (R.I.P) anazikwa Leo jijini Dar es salaam huku mwili wake ukitokea Njombe.
Kilichonishangaza ni kua mh alifia Njombe mjini lakini mwili wake ukahidhiwa hospital teule ya Ilembula.

Hapa ndio ikanibid kufuatilia kulikoni. Jibu nlilopata ni kua hospitali ya mkoa wa Njombe
(Kibena) haina uwezo wa kuhifadhi
maiti. Kutoka Njombe hadi Ilembula ni zaidi ya kilomita 60.

Swali likanijia, hivi mkuu wa wilaya alishindwa kuhakikisha mafriji yanapatikana ktk hospitali ile kubwa ilopewa hadhi ya Regional hospital?

Vipi kuhusu mkuu wa mkoa na wizara ya afya? Mkoa hauna Pesa za kuhakikisha mortuary inafanya kazi vizuri? Hii ni aibu na maut zitawaumbua watawala.

Njombe ni mkoa mpya
 
1954 said:
Njombe ni mkoa mpya

Kwahyo haupaswi kua na mortuary mkuu? Kumbuka ilikua wilaya tena ilobeba mji mkubwa wa kibiashara (Makambako). Cha ajabu pale makambako nshawahi ona mortuary tena nzuri tu. Anyway, sibishi ila ni tatzo so wakuu wa mkoa husika walione hili
 
Tutasutana sana humu jf lakini ukweli usemwe mchawi namba moja kwa maendeleo ya watz ni ccm maana wao wanaagalia zaidi kushika madaraka kuliko maendeleo ya watz ndo maana chama cha ni tajiri kuzidi serikali
 
ccm ndio wa kulaumiwa, wanajali uhai ili wakutumie baada ya hapo kimya, nawashauri wabunge wa ccm wakati mwingine toeni hata ahadi za mafriji ya KIJANI kwenye hizi motuary.
 
Kiufupi Mkoa wa Njombe Serekali ipo Chini kiuwezo kuliko watu binafsi. Huduma za Serikali hazieleweki! Watu wanaenda Hospital za Misheni kama Ilembula(KKT)(Wanging'ombe). Ikeru(St.Joseph Roman, Njombe) na Ikonda( Roman, Makete).Kama unataka Ufe ukijiona nenda Hospital za Serekali hapa Mkoa wa Njombe. Hospital za Serekali Njombe zinaitwa dispensali, MTU anaenda Km 120 kufata Huduma katika hospital za Mishen, hakuna jinsi ndo hivyo!. Mama Sarah Dumba(R.I.p) alikua Mkuu wa wilaya ya Njombe lakini anahudumu mpaka Makambako, kwenye sherehe hadi usafi utamuona Makambako, hapa Makambako wanamuita Mkuu wa Wilaya ya Makambako, lakini Serekali wanamuita Mkuu wa wilaya ya Njombe!. Basi tabu tupu!.
 
Mkuu upo sahihi sana, yaani utadhani Ikonda ndio hospitali ya mkoa.

Back
Top Bottom