#COVID19 Hospitali ya Bugando yakumbwa na upungufu wa mitungi ya Oksijeni kwa Wagonjwa wa Kupumua

hospitali marehemu mama yangu alilazwa walikuwa wanatumia VENTILATOR za umeme!sio cylinder!...
Mkuu ukiona mtu anafanya joke na UVIKO-19 ujue haujampitia au haujapitia familia yake. Ebu aende ICU akaone wagonjwa wenye UVIKO-19 wanapumuaje, alafu aje hapa aseme ni mafua tu. Hii kitu isikie tu mkuu kwa mbali. Usiombe ikutokee au itokee wazizi wako alafu uambiwe yuko kwenye ventilator.
 
Wewe jamaa ni mjinga sana. Kabla hujaandika jaribu kufikiria kidogo na sio kuandika kwa ushabiki tu. Serikali ina hela imetoa wapi? Hiyo ni hela yetu wananchi na ni lazima ituhudumie kwanza kabla ya kwenda kujenga masanamu yasiyo na maana yoyote. Wananchi wanakufa kwa kukosa oxygen na wana hela zao wamekabidhi watu kuzitunza na kutumia kwa ajili yao lakini wao wanakwenda kujenga sanamu. Sanamu yenyewe ya mtu aliyeacha historia mbaya katika jamii. Ujenzi wa sanamu ni matumizi mabaya ya hela ya wananchi. Amka!!!!!
 
Kitaeleweka TU,
Kikubwa imani yako, ukiwa na hofu utakufaa mapema.

Shughuri ziendelee,
Kama tulisavaivu kipindi inaanza, na tutasavaivu pia hata kipindi hiki.

Tusitiane Hofu,
Nna imani Mungu atatutia Nguvu.

Inshallah
Kweli kabisa... Tusitishane
 
Tunajenga kwanza sanamu ya aliegundua vitunguu swaumu na malimau kama dawa ya Corona,mitungi ni mambo ya baadae sana.
 
Hata mashehe gerezani waliugua na kupona kwa kutumia azuma. Dawa inayotibu kisonono.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Hivi serikali inasubilia nini ku impose strict measures ikiwemo lazima ya barakoa,marufuku ya mikusanyiko isiyo ya lazima na kwenye mastendi kuzuia milundikano,lazima ya maji tiririka kama kipindi kile unaingia?

Kutumia tuu soft language ya kwamba watu wachukue tahadhari haisaidii na hata shule kwa sasa zipigwe ban kabla Hali ya India haijatufika..

Ikiwezekana lockdown ifanyike kwenye mkoa huo
 
Kukumbushana bila bakola watu hawaelewi
 
We mtu wa ajabu hiyo ripoti inasema kuchukua tahadhari na kujiandaa kuwa na mitungi ya oxygen.
Ulichoandika ni kana kwamba wagonjwa ni wengi mpaka oxygen imekosekana.Watu Kama wewe ni hovyo kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…