Kamakabuzi
JF-Expert Member
- Dec 3, 2007
- 2,861
- 1,302
Huo ndio usanii wa Tanzania na takukuru yake.Chenge ambaye wakati wa ununuzi huo alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) anatuhumiwa kuwa kiungo muhimu katika ununuzi wa rada kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya BAE Systems. .
Asisitiza hana kesi ya rada
Kuhusu kuhusika kwa Chenge katika kashfa ya rada baada ya Mahakama Kuu Uingereza kuamuru BAE Systems kurejesha sehemu ya fedha kwa Tanzania kutokana na kubaini upotevu wa nyaraka muhimu za manunuzi halali, Dk Hoseah, alisema, mbunge huyo hahusiki na kwamba hakuna ushahidi wowote wa kumtia hatiani.
Nashangaa kuona Watanzania wakishikilia kuwa Chenge ashtakiwe kwa kitu ambacho hakina ushahidi, lakini wanasahau kuwaeleza Waingereza kuwa ndio wahusika, alifafanua Dk Hoseah,
Kuhusu Kagoda
Akizungumzia kashfa nyingine inayotikisa Kampuni ya Kagoda Agricultural Limited inayodaiwa kuchota Sh 40 bilioni kutoka Akaunti ya Madeni Nje (EPA) katika Benki Kuu Tanzania (BoT), alisema taasisi yake imeanzisha upya uchunguzi, licha ya kamati ya Rais Kikwete, kuwabana wahusika wakarudisha kitita hicho.
Dk Hoseah alisema kwa kutambua hilo, ndiyo maana amewaomba Watanzania wote wenye ushahidi wauwasilishe ofisini kwake ili kuwezesha kuendelea kwa mchakato huo wa kuwafikisha mahakamani wahusika wote. Mkuuu huyo wa Takukuru, alisema kwa sasa kumbukumbu katika jalada la usajili wa kampuni hiyo kwa Msajili wa Makampuni (Brela), zinaonyesha wamiliki wake wote wawili ni marehemu.
Mwananchi
Yaani chenge alikuwa kiungo muhimu kati ya tanzania na BAE kwenye ununuzi wa rada; na imeshabainika kuwa ununuzi ule uligubikwa na rushwa, halafu hicho kiungo kiwe hakiusiki? Inashangaza na inatia mashaka.
Kama hana kesi ya kujibu juu ya suala zima la rada, kwanini sasa mnamshitaki. Mimi nadhani mnamshtaki si wa kuwa na mali bali ni kwa kuwa mali ni nyingi na mna wasiwasi na namna alivyozipata, na mojawapo ya njia hizo ni rushwa katika rada.
Isitoshe chenge hakujuliana leo kuwa ana mali nyingi, mlimjua tangu aliposema kuwa hizo dola 1.2m ni vijisenti - mbona hamkuchukua hatua wakati huo?.
Hosea tunakushangaa sana - ulishakataa kumshitaki chenge kwa masuala hayo tangu zamani, leo umesukumwa na nini?. Kuna sababu mbili
Ya kwanza ni kuwa serikali imeona inanyimwa hela za rada kwa kuwa inatuhumiwa kuwalinda mafisadi wa rada, sasa inaona ijitutumue. Wakishalipwa, yanaishia hapo.
Pili ni suala zima la kujivua gamba. Wameona chenge hataki kujizuru toka uongozi wa ccm hivyo wameona wamuundie kesi.
Kuhusu suala la kagoda
Hosea anasema watuhumiwa walibanwa wakarusha kitita, bado anataka ushahidi. Ushahidi gani zaidi ya huo?
Eti wenye ushahidi waulete na wakati huohuo eti wahusika wameshakufa!
Walirudisha fedha wakiwa hai hamkuwakamata, wamekufa ndipo mnataka ushahidi!!!!!