Kweli kazi nzuri sana kwa miji ya kisasa
Kasoro ndogo tu ni kwamba Sio rafiki kwa walemavu wavuka njia.
Fuatilia Kipindi alichorusha Zembwela Jpili iliyopita sehem za kuvukia hasa kwa walemavu ndio utapata jibu.
Technically hiyo barabara italeta ajali sana hususani magari kupigana pasi.
Upo sahihi kabisa mkuu, kwa mfano mtu anatokea Sinza kwa Remy na anaenda K'Koo au let say Posta, itabidi apande bus mpaka Shekilango ili aweze kuconnect na haya mabus ya kwenye kwa haraka, hii inamaanisha kwamba uchumi wa watanzania inabidi ukue kidogo ili waweze kuafford hizi changes otherwise mtu inabidi atembee tu from Sinza to Shekilango ili apande bus la kwenda kwa haraka, kwa kweli ni changamoto. Buguruni-Kawe/Masaki inaweza kuwepo mpaka pale tu mpango wa barabara ya Kawawa itakapokamilika, lakini hata ikikamilika kumbuka yenyewe inaanzia magomeni Mapipa tu mana yake ni kwamba lazima mtu from Buguruni afanye mchakato wa kupanda bus jingine mpaka Mapipa. Yaani kazi kweli kweli. Kwa ufupi biashara ya coster na hiace bado itaendelea kuwepo baadhi ya sehemu. Kwa mfano route kama K'Koo-Tabata, Magomeni-Sinza kupitia Tandale, Mwananyamala Posta, Mwenge-Posta n.k
Hapo si ndo shekilango!
Ni kweli, inabidi vipato viongezeke ili kumudu gharama za kusafiri jijini. Barabara ya kawawa ikikamilika, mtu anayetoka buguruni kwenda kawe/masaki atapanda Mara tatu hadi kufika mwisho wa safari. Mwenge kwenda kimara atabadili mara mbili, mwenge-sinza kwenda k.koo atabadili mara tatu...nahisi haya vipato inabidi viongezeke...
Are you serious? Kwa hiyo kutakuwa na mabasi yanauounganisha njia za Dart? Lets say mtu anatoka sinza-kariakoo, anakuwa na junctions tatu..sinza-sheki, sheki-fire(dart)then fire-kariakoo...huyu ananunua ticket ticket moja tu? Then itapinguza kidogo mzigo wa nauli kuongezeka. Japo nina wasiwasi mabasi ya dart nje ya njia zake yatakuwa machache sana..anyway, tusubiri tuone...!unakata tiketi moja tu mahali unapoanzia safari mpaka mwisho wake.....pia unaweza kukata tiketi ya siku/wiki/mwezi/mwaka kulingana na mahitaji yako....kwa mfano uko buguruni unaenda masaki unakata tiketi ya buguruni masaki single/return ambayo utatumia kwenye mabasi yote yatakayihusika na connection zako....sehemu ambazo hizo barabara za dart hazifiki wataweka mabasi yao ndio yatakuwa yanaleta watu hadi barabara kubwa za dart....ila nauli itakuwa juu kidogo sio 400/= kwa route.......kizuri gharama.
are you serious? Kwa hiyo kutakuwa na mabasi yanauounganisha njia za dart? Lets say mtu anatoka sinza-kariakoo, anakuwa na junctions tatu..sinza-sheki, sheki-fire(dart)then fire-kariakoo...huyu ananunua ticket ticket moja tu? Then itapinguza kidogo mzigo wa nauli kuongezeka. Japo nina wasiwasi mabasi ya dart nje ya njia zake yatakuwa machache sana..anyway, tusubiri tuone...!
asante serikali ya ccm kwa kuboresha miundo mbinu iliyobora
thats how it works...unaona kile kituo cha shekilango rd ni kwa ajili ya feeder buses from shekilango road...ukipita magomeni moroko hotel kipo ile njia inayotoka kwa mtogole kwa ajili ya feeder buses from kwa mtogole....ukija kinondoni nyuma ya puma petrol station kipo kwa ajili ya feeder buses kutoka m'nyamala..pale magomeni butiama hotel kipo kwa ajili ya feeder buses kutoka kigogo hivyo ndivyo itakavyokuwa na feeder buses ni kubwa kama yale ya mbagala moja washalifanyia majaribio watu wakafikiri ndio mabasi yao.
fire-kariakoo-kamata dart main inapita kwahio yale makubwa yatafika huko,connection ndio hizo kama unatokea sinza unakuja shekilango....mwenge/kawe unakujaj hadi moroko...mwananyamala unakuja hadi nyuma ya puma pale mwanamboka etc
Kazi nzuri, ila naona kasoro kwenye bus stops walizoziweka, naona ziko nyingi na karibu sana, mfano kutoka Kimara mpaka Fire kuna vituo vingi sana, na sehemu kubwa wamechukua vitu vile vile vya zamani. Sasa hapo maana ya mabasi ya mwendo kasi naona haitakuwepo sana.
Si kwamba hayo mabasi yatakwenda kwa kasi hapana, lengo ni kwamba yatakua hayasimami kwenye foleni kama magari mengine na unaweza panga safari yako toka kimara hadi fire, utakua unajua kua utafika hapo firw mda gani
Ni kweli, inabidi vipato viongezeke ili kumudu gharama za kusafiri jijini. Barabara ya kawawa ikikamilika, mtu anayetoka buguruni kwenda kawe/masaki atapanda Mara tatu hadi kufika mwisho wa safari. Mwenge kwenda kimara atabadili mara mbili, mwenge-sinza kwenda k.koo atabadili mara tatu...nahisi haya vipato inabidi viongezeke...
Wamepunguza sana upana wa barabara kama kiasi kwamba tutapigana pasi sana na tukijitahidi kukwepana tutakuwa tunazitandika zile nguzo za taa barabarani na si dhani kama zitasalimika zile. Boda boda wajiandae kwa kiama zaidi hasa inapotokea wanakatiza katikati ya magari kwani nafasi haitoshi hivyo wataishia mivunguni mwa magari kwa haraka zao maana wao wanataka kupita sehemu yoyote na wakati wowote. Hata hizo barabara za katikati za mabasi ni finyu sana kama dereva ni mtu wa kupepesa macho pembeni atajikuta ameparamia pavement blocks na kuhamia upande wa barabara za raia ambako nako ni kufinyu. Solution ni kuamua kuwa barabara hizi zitumike na vigari vidogo tu mwisho size ya coaster na canter. Milori na mibasi iishie nje ya mji kwani kwa ukubwa wao moja tu linatosha barabara yote na usiombe liwe na trailer ndio balaa! Na likiharibika barabarani ndio shida kubwa!
Ukiacha ufinyu wa barabara! Shida nyingine ni pale watakaposhuka kwenye mabasi na kutaka kuvuka ili waingie pembeni mwa barabara! Magari katika barabara za kawaida yatalazimika kusimama mara kwa mara karibia kila kituo! Hapo ndo watatengeneza foleni za kufa mtu! Magari yatakuwa hayatembei kabisa!