Sielewi hii habari ya NSSF kabisa mpaka nikielezwa kama hii ni investment nzuri kwa hela za members wake! Mtu hawezi kupata compliments kwa kutumia hela za watu kutafuta sifa! Pension funds duniani kote (isipokuwa kwa nchi chache za Africa) huwa zinawajibika kwa wachangiaji wake, na sio kwa serikali i.e. kuzitumia kutekeleza ilani au order za serikali! Pity!
Hao nssf mara wemekopesha kiwira!, hao mara wamejenga soko la machinga, hao wanataka daraja la kigamboni, hao hao, magodown ya manji, haohao wamejenga nyumba zote za serikali dodoma (Area C nk), hao hao wamejenga mabweni ya UDSM mabibo, hao hao wamejenga majengo kadhaa dodoma university, nk! Hivi hii yote inareflect vipi kwenye kipato cha pensioners/members wake! Nadhani kuna haja ya kuzifanye hizi pension funds tanzania zifanye kazi kama life insurance companies ili pension iwe predetermined kama kwenye life insurance policy! Hii habari ya kuchangia hela (20% ya gross wage) bila kujua utapata nini ukistaafu (defined contribution, not defined benefit!) ni ya ajabu kabisa! KUna haja ya kufuta sheria ya pension ili watu wapeleke hela zao kwenye bima. Leo hii wastaafu wangekuwa wanajinafasi sana na pension zao kama tungekuwa na mfumo tofauti!
I hate this system and will never give a credit for anything to anyone wallowing in the pool of money - someone not seriously accountable to anyone and not being being objectively benchmarked to anyone/anything! These funds are just vehicles for theft and politics!
jibu: hii sio investment nzuri kwa member wake
NSSF investment facts
48% govt bonds (hapa ndio utaona majengo kama udom, polisi, PCCB na miradi mingineyo ya serikali)
18% properties( hapa utakutana na vitu kama ubungo plaza, quality ambayo ukusanyaji wake wa rent ni tata na majengo mengi)
govt bonds zinajulikana duniani kote kama ni safe kwa hiyo interest yake ni ndogo sana..... na kama interest ni ndogo pia returns zake ni ndogo pia, na kwa ajili return ni ndogo kwa hiyo pengo la pension linajengeka ndani ya nssf (kwa lugha ya kigeni "pension black hole"), na mjenzi wa hili pengo si mwingine bali ni dr dau...
kama dr dau ame invest nusu ya nssf kwenye govt bonds hii ni dhairi kwamba nssf haiko diversified, serikali ya TZ ikikumbwa na misukosuko na ku default on payments kampuni ya kwanza ku bust itakuwa NSSF
wataalamu wanasema america lives on china credit card, china wameivest savings zao nyingi kwenye american bonds, lakini american bonds ni safest bonds in the world, pamoja na mtikisiko wa uchumi america haja default bonds zao, ukae ukijua TZ sio marekani wao wata default tuuu......
kwa kifupi juu ya NSSF, bonds na serikali (udom, polisi na mengineyo ni mikakati ya serikali, NSSF ni credit provider na watu wanaolipia interest ya hiyo credit ni walipa kodi wa TZ)
mambo yakifanywa na america kwa kupitia mauzo ya bonds zao kwa china huwezi kusema china ndio wamefanya unasema marekani
na mambo yakifanya na TZ kwa kupitia mauzo ya bonds zao kwa NSSF, crdb, nmb huwezi kusema NSSF ndio wamefanya unasema serikali ndio imefanya.....
wakati umefika NSSF kukopesha wanachama wake ambao wanahela zao pale na hizo hela zitumike kama security