Kujenga nyumba kwa ajiri ya jamii ni vyema sana na ninatoa suport kubwa kwa NSSF. Na pia kama wengine walivyosema MIFUKO yote ya hifadhi za jamii yaani PPF, PSPF , NHIF, CWT LAPF, yote inatakiwa kutoa mifano ya kuigwa kwa manufaa ya jamii. Kwani kwa mfano Chama Cha Walimu kinakusanya pesa nyingi sana, lakini hakijawahi kuwekeza kwenye nyumba za walimu wakati ndiyo wanaotoa hizo pesa!!! Hivi kingeamua hata kujenga nyumba Mbili kila Wilaya kwa mwaka kingeshindwa??? .Viongozi walioko huko wamelala na kujinufaisha wenyewe.
No comment
Kuhusu gharama halisi ya project ni muhimu sana kuuliza kwani ufisadi mkubwa hufanyika huko, Hao Auditors unaosema '' Most of them they are good as nothing'' Most auditors niliokwisha kutana nao wakishapewa fupa tu, huandika report nzuri ya kumsifu mwajiri wao kwa wakati huo ambaye huwa ni Mkurugenzi wa hizo kampuni au mashirika. Kwanza Auditor ni wewe MD ndiyo unawapa kazi, na wakikuharibia next year huwapi kazi!!! What do you expect.!!!
Sasa kama hatumwamini auditor sijui tumwamini nani? What about kamati ya bunge ya mashirika ya uma?
Umeomba akupe mfano wa matumizi mabaya ya pesa za project !!! Ina maana wewe upo Tz hii au huwa unafunga masikio pindi anayetuhumiwa anapokuwa kipenzi chako??!! Project ya kununua Magodown pale ubungo toka NSSF na Manji kwa Bil. 3 na kuyakarabati kwa pesa ya NSSF Bil. 9 na kuyauza kwa NSSF kwa Bil. 40 siyo matumizi mabaya hayo ya pesa za project??????!!!
Kuhusu magodown nenda kajiandae vizuri kisha uje na data then tujadili kwa sababu maelezo yako hayana ukweli hata kidogo..lakini kwa kukufafanulia tu kuwa NSSF ni shirika makini na liko chini ya watu makini hayo unayoyasema hayakufanyika, hayajafanyika na hayawezi kufanyika kwa sababu Kwa mujibu wa Kanuni za Fedha [Financial Regulations] na Sera ya Uwekezaji [Investment Policy] ya NSSF, maamuzi kuhusu uwekezaji huanzia kwenye Kamati ya Uwekezaji ya Menejimenti [Management Investment Committee]. Kamati hii hufanya uchambuzi wa miradi yote inayowekezwa na Shirika na iwapo itaridhika kuwa miradi hiyo ina faida kwa Shirika, Kamati huwasilisha mapendekezo yake kwenye Kamati ya Bodi ya Wadhamini inayoshughulikia masuala ya Fedha na Uwekezaji. Kamati ya Bodi nayo hufanya uchambuzi na kujadili hoja zinazowasilishwa na Menejimenti. Kamati ya Bodi ikiridhika na hoja hizo, huwasilisha mapendekezo kwenye Bodi ya Wadhamini ya NSSF [NSSF Board of Trustees] kwa maamuzi ya mwisho. Sasa unamaana hawa wote na hii mechanism yote kwako haina maana au vipi
Kwanza hebu lete sources zako z kisha tujue mwelekeo uko wapi
Tusiwe biased wakati tunataka kutoa ukweli ili tusaidie taifa letu. Hata kama mtu ni kipenzi chako, akiharibu mwambie ukweli, na akifanya vizuri mpe haki yake.
Bias itoke wapi wakati kazi iko open inaonekana? Na kama unataka kupekuwa utendaji wa Mashrika ya Umma usiishie NSSF. How about TIB? ATC?
usisahu kutaja sisahau kuandika MAZURI ya NSSF kama yapo. Lakini sisi tunayajua yafuatayo:
-Dodoma University where NSSF inajenga NUSU ya Chuo [20,000 students]
-Mabibo Hostels Chuo Kikuu DSM [5,000 students]
-Nyumba za Jeshi
-Nyumba za Polisi
-Daraja la Kigamboni (anytime)
Picha nilizoziweka hapo juu zinaonyesha fika kuwa askari wetu wanaishi katika sub human conditions. Inwezekana hili hulijui kama hao wengine wanaishi nje ya nchi miaka mingi
ohh how can i forget kuwa
-Ujenzi wa Jengo la Bunge lenye hadhi
-ujenzi wa Balozi zetu mbalimbali ukianzia Kenya.
Hapa kwenye nyumba za balozi NSSF imesaidia sio tu kuokoa mamilioni ya dola ambayo serikali inalipa kama kodi bali pia NSSF wameiondolea serikali fedheha ya kukodi nyumba na kuadhiriwa na landlords kama watachelewa kulipa.
Contrary na alivyosema jamaa hapo juuu usidhani NSSF inafanya miradi hiyo hapo juu ili KUJIPENDEKEZA serikalini. La hasha! Miradi YOTE hiyo inaendeshwa kwa misingi ya kibiashara na NSSF inapata a much higher return than the alternative investment of the SAME tenure
-in 2001 wakati Dau anajiunga NSSF, Contribution zilikuwa 39 billion. Leo ni over 200 billion
-growth in Investments
-NSSF inatoa mafao 7 kati ya mafao 9 yaliyomo kwenye ILO Convention 102 ya 1952.
NSSF TANZANIA inatoa mafao mengi zaidi kuliko taasisi YOYOTE ya pensheni kusini mwa Sahara INCLUDING South Africa. No wonder Kenya, Uganda, The Gambia, Sierra Leone etc WANAPIGANA VIKUMBO kuja kujifunza NSSF
-Staff Welfare: 2001 minimum wage 52,000. Now over its 400,000
Kwa kumalizia tuu ni kuwa wiki iliyopita kwenye
SABA SABA (NSSF) ilikuwa second overall winners in all categories
sasa tabu ya nini ?