Hongera Zitto Kabwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera Zitto Kabwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mamanalia, Feb 11, 2011.

 1. m

  mamanalia JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 671
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Natoa pongezi zangu nyingi kwa zitto kabwe (mb) ambaye muda wote amekuwa a good gentleman with showing patriotism in the parliament.

  Ni mbunge mmoja tu wa upinzani ambaye toka niangalie bunge naona anatueleza ukweli bungeni. mchango wake wa jana kuhusu hotuba ya rais wetu ambaye kwa ukweli ameonyesha kuwa among the two weakest presidents in TZ ulikuwa very constructive.

  Mie namwomba pia akayazungumze haya bungeni:

  Lazima Rais azungumzuie kuongeza mapato and hence uchumi kwa kufikiria short term measures kama vile kufanya kila mtanzania anayeingiza kipato alipe kodi. mfano. Naamini wenye nyumba wote wanaozipangisha hapa nchini hawalipi kodi, hivi tunapoteza shilingi ngapi kila mwezi ambazo hawa wafanyabiashara za nyumba za kupangisha hawazilipii kodi.

  Zitto kawaambie kuwa Watanzania wengi hasa wa mjini wanaishi informal life na wanamiliki fedha nyingi ambazo hawazilipii kodi na ndio maana hata gharama za maisha zikiongezeka hawaandamani sababu wanaweza ku afford. Hii inapelekea wengi waingisho vijijini kuwa wana suffer everyday.

  Zitto mie pia nimekuwa nchini malaysia na nchi mbalimbali za asia, afrika kusini, europe n.k. Nilichojifunza ambacho ningependa pia uwaeleze hao serikali ingawa huwa hawana masikio; serikali yoyote brilliant na iliyoendelea lazima ijihusishe kwenye public businesses kama nyumba za kupanga na kuuza, usafiri wa daladala (commuting), reli, nishati (including petroleum), bandari and all types of public businesses ambazo hizi ndizo huwa zinakuwa daily income za serikali.
  Imagine ni pesa ngapi wamiliki wa madaladala wanaingiza kila siku, wamiliki wa manyumba n.k.

  Kaka zitto tusaidie sie ambao hatujaenda mjengoni kufikisha mawazo yetu huko.

  Wish u the best.
  Note wanaJF. Mie sio ccm wala chadema. I m a humble Tanzanian.
   
 2. kisu

  kisu JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 802
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Sasa wanaolipia leseni za daladala kila mwaka ni za kazi gani kama nayo si kodi? Mkuu, serikali inakusanya pesa nyingi sana (Nadhani si chini ya Trilion 10 kwa mwaka, kama ilivyo kwenye bajeti). Lakini, Serikali mbofumbofu na matumizi mbofumbofu, ndio sababu kuu wananchi kusota!! Chukua Chako Mapema!!!!!
   
 3. m

  makongorosi Member

  #3
  Feb 11, 2011
  Joined: Apr 24, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ogo cha mfano wa magari ya daladala, nchi zilizoendelea unazozizungumzia wewe ni tofauti na tanzania katika miundo mbinu mfano barabara, Tanzania wamiliki wa hivyo vidaladala wanafanya kazi ngumu sana unawea kuona wanaingiza sana lakini kiukweli na magari yanaharibika sana na vipuri vyake ni gharama hivyo uendeshaji wa vidaladala hata magari makubwa kwa tz in mgumu japo kwa nje utaona wanaingiza pesa sana, hapo hapo kuna mapolisi kila kona kuwachomoa madereva hata kama hawana makosa, kitu ambacho kwa nzhi zilizoendelea hakuna upumbafu kama huo. Kuna wafanyabiashara wakubwa ambao wanasamehewa kodi lakini siyo kuwakaba wamachinga kuwadai kodi eti ndiyo watajenga uchumi wa Tanzania. tuanzie kwa wafanyabiashara wakubwa kuwakaba tujenge mazinginra na miuondo mbinu mizuri ndiyo hapo tuje tutazame wafanyabiashara wa wadogo hapo tutaipata Tanzania tunayoi dream.
   
 4. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  mnasahau kuwa serikali ilimiliki uda, kamata, mabasi ya reli lakini mapato yale yakaishia mfukoni mwa wachache? hakuna cha malaysia au china hapa. ufisadi kwanza utokomezwe mengine yatajipa yenyewe. kuna watu hapa wakienda nje mara moja wanakuja na kufikirika chungu mbovu. situation yetu haina mbadala wa kujifunza nje. hapa kuna serikali mbili inayokaa ikulu na akina rostamu na lowasa. tukishakuwa na aserikali moja ndo hapo hizo alinacha za malaysia tutaweza kujipanga nazo. otherwise usipoteze muda wa watu hapa kutueleza safari zako uchwara za nje.
   
 5. L

  LAT JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu... public business ilishashindikana toka enzi za Nyerere... kwani UDA si ndio unachozungumnzia kama commuting .., TRA.., ATC.., vipo wapi....? public business zote zimeliwa na wajanja..... its because of greedy leaders..., kinachotakiwa sasa hivi ni Private Public Partnership
   
 6. birungi

  birungi JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hakuna kinachoshindikana chini ya jua, tuangalie waliofanya hivyo walijipanga vipi na wanakabiliana nalo vipi.
  nasi tunaweza ni mfumo kuangaliwa na kupangwa upya.
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,481
  Trophy Points: 280
  Mamanalia, asante kwa hili, hata mimi naungana nawe kumpungeza Mhe. Zitto yuko very organized na content bila kuhamanika na siasa za vyama bali kugongelea misumari ya moto hotuba ya JK huku ikiandamana na vithibitisho na mifano hai ya success stories.

  Zitto ni miongoni mwa wabunge wachache wenye kuonyesha maana ya kwenda shule, wengi wamekwenda shule lakini huishia kuropoka na kupiga makele kwa majigambo ya superiority complex za elimu zao!.

  Exposure imemsaidia sana Zitto ku drive home his nail tu utumbo wa vipaumbele vya mkulu na kuitumia exposure hiyo kujiuliza kama mwanzo Tanzania tulikuwa masikini kama the tiger countries ambao wao hawana resources kama tulizonazo sisi wala hawana ardhi kubwa kama yetu
  kwanini wao wameweza na kwa nini sisi tumeshindwa?. Hivi kuna Mtanzania yoyote aliyesafiri mataifa mbalimbali zaidi ya Vasco?. Akiwa safarini huwa anafanya nini?, au zile pay TV za room zinamkeep bize hivyo mchana hana la kujifunza?. Tangu ameingia ameleta mageuzi gani ya ukweli ukiondoa UDOM?. Kama ni lami mababara yalikuwepo, nothing new!.

  Angalau Mkapa alimleta Prof. Hernando De Sotto na matokeo yake ni formalization ya indigineous property, MKURABITA na leseni za makazi, JK ameleta funzo gani toka atokako zaidi ya kutembeza bakuli?.

  Zitto amethibitisha ni kichwa, na naamini bado kuna vichwa vingi mule akiwemo JJ.Mnyika, ila hata Tundu Lissu ni kichwa ila bado amehamanika na pride ya ushindi na superiority complex ya 'the learned brothers', inayompelekea kuwa na papara za miongozo ya Spika, akitulia he is good!.

  Nliwahi kuwapa Chadema ushauri fulani kuhusu Zitto, nilichoambulia ni matusi. Zitto ni jiwe walilolikataa waashi, limefanywa kuwa jiwe kuu la pembeni (POAC). Aliposhauri genereta za Dowans zinunuliwe au zitaifishwe, alibezwa sana na kuonekana kama mwendawazimu fulani. Waliopinga walipinga kisiasa zaidi kuliko kihalisia wakazitosa genereta mpya za kutoa megawati 100 kwa capacity charge ya Shilingi Milioni 152 kwa siku, halafu serikali hiyo hiyo ikakubali kuilipia mitambo obsolate ya IPTL shilingi milioni 300 kwa siku huku ikitoa megawati 60 tuu na inakunwa dizeli ya ajabu na uchafuzi wa mazingira on top of it!. Nani ni mwendawazimu hapa?.

  Naamini Zitto has very bright future ahead of him, amesemwa sana amejinyamazia na kumwaga nondo.

  Mhe. Zitto punguza hasira na JF, rejea jamvini, kuvumilia cricisim ni strength na running away from problem ni weakness, I don't believe you can be that weak!, kama ni execuse kuwa uko busy na Ph.D yako, tutakuelewa na tuko pamoja.

  Pasco
   
 8. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #8
  Feb 11, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Mamanalia nakubaliana nawe,ila nadhani usilinganishe developed nations,na developing ones. Tatizo hapa ni ufisadi na uongozi mbovu wa juu. Pia,naomba urejee vizuri maktaba ujiridhishe kuwa Income Tax Act (ITA) 2004,imeweka wazi vyanzo vya raia ambavyo havitalipitia kodi! Ukitaja pango yani residential houses sorely for residential purposes shall not pay tax on rent,unless owned by non-resident person or for commercial. Kwa iyo pango kwa wakazi wa dar haitalipiwa kodi. Nadhani apo tupo pamoja. Vinginevyo naungana nawe kumkubali zitto,na si huyu tu wapo hata Peter serukamba,Lissu na wengine ila tatizo lipo hapo juu kwenye utawala wa mwisho!
   
 9. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #9
  Feb 11, 2011
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  kwa kweli zitto is grown up in the head in terms of politics
   
 10. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #10
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  well, it can be done , if others did why not we?
   
 11. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #11
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Tunashukru sana kwa taarifa,lakini si wote wako TZ wengine wapo nje ya nchi, je waweza kutuelezea walau kwa kifupi ni yapi aliyoyaongea ili nasi tuelewe?
  Thanks
   
 12. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #12
  Feb 11, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  Nliwahi kuwapa Chadema ushauri fulani kuhusu Zitto, nilichoambulia ni matusi. Zitto ni jiwe walilolikataa waashi, limefanywa kuwa jiwe kuu la pembeni (POAC). Aliposhauri genereta za Dowans zinunuliwe au zitaifishwe, alibezwa sana na kuonekana kama mwendawazimu fulani. Waliopinga walipinga kisiasa zaidi kuliko kihalisia wakazitosa genereta mpya za kutoa megawati 100 kwa capacity charge ya Shilingi Milioni 152 kwa siku, halafu serikali hiyo hiyo ikakubali kuilipia mitambo obsolate ya IPTL shilingi milioni 300 kwa siku huku ikitoa megawati 60 tuu na inakunwa dizeli ya ajabu na uchafuzi wa mazingira on top of it!. Nani ni mwendawazimu hapa?.

  Naamini Zitto has very bright future ahead of him, amesemwa sana amejinyamazia na kumwaga nondo.


  wana jf tuache ushabiki wa kinafiki kila mara zitto anap[otuhumiwa huwa ushahidi unatolewa Said kubenea aliwahi toa hadi mawasiliano kati ya ziitto na Rostam Aziz, pia zitto na zola, pia zitto kupinga uamuzi wawabunge wa chadema kwa kutokufika bungeni, acheni unafiki na ushabiki wa kijinga tuanmgalie maslahi ya nchi huyo zitto pekeyake hana uwezo wa kuinusuru nchi bali ni juhudi zetu soote pamoja na mshikamano katika kuupinga ufisadi.
   
 13. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #13
  Feb 11, 2011
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Kaambiwa kigoma itakuwa dubai hana jipya!
   
 14. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #14
  Feb 11, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kuna tofauti kubwa sana kati ya mali ya umma na mali binafsi. Hakuna popote pale duniani ambapo mali ya umma imelindwa kwa dhati na wananchi bila ya kuwepo udhibiti wa kueleweka. Mali binafsi inajulukana na mwenye mali ana uchungu nayo hivyo atajua mwenyewe namna ya kuidhibiti. Cha msingi hapa ni kuwepo na mikakati ya udhibiti wa mali za umma na mengine yataenda sawa.

  Walter Rodney katika kitabu chake-How Europe underdeveloped Africa ameandika kuwa "serikali yoyote inayotegemea kodi ni mufilisi". Kodi ni nyongeza tu katika matumizi ya serikali. Serikali inatakiwa kuwa na vyanzo vya uzalishaji kama ilivyosemwa hapo juu-majengo, njia za usafirishaji, viwanda, n.k. Mapato yatokanayo na hivyo vyanzo ambayo yamedhibitiwa yakichanganywa na kodi hakutakuwa na haja ya kumtegemea mfadhili wala kuwepo na upungufu wowote
   
 15. semango

  semango JF-Expert Member

  #15
  Feb 11, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  mkuu umenena.mtoa mada ananipa wasiwasi kua nae ni fisadi mkubwa.yani bado anawazo mwananchi wa kawaida abanwe zaidi!!!inanisikitisha.me wazo langu ni kua kwanza hiki kiasi kinachopatikana kitumike vizuri kabla hata ya kusaka zaidi.imani yangu ni kua kama hakuna discipline ktk matumizi na ufisadi usipokoma then hata tukipata vyanzo vya kukusanya trilion 10 kwa siku 1 bado haitatosha
   
 16. W

  WildCard JF-Expert Member

  #16
  Feb 11, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Zitto alikuwa amejikita kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi yetu (7%!) na umasikini wa watu wetu ambao unazidi kuongezeka. Zitto ni mchumi kwa hiyo anajua kunyambulisha tarakimu hizi za kiuchumi na inaleta raha kumsikiliza kama alivyo kaka yake Kakobe na masuala ya Biblia. Hatoi majibu ya matatizo tuliomo na anajua sana kuchagua maneno ya kutumia ili asiwaudhi CCM na hasa JK wake.
  Aligusia pia huduma za jamii kama elimu, afya jinsi zinavyozidi kuwa za kibaguzi na kitabaka kwa wenye nacho na wasio nacho. Hakusema tufanye nini kama Taifa.
   
 17. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #17
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  hapo ndio kwenye tatizo zaidi.Hao ndio viongozi wetu tuliowapa madaraka lakini wanapokosoa vitu hawaatoai suluhisho kama njia mbadala, je kama hiambii serikali njia mbadala itabadilikaje? wao ndio wasimamizi na washauri wa hiyo serikali sio kulaumu tu
   
 18. m

  mamanalia JF-Expert Member

  #18
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 671
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mkuu hizi excuse za kodi ndio moja ya excuse nyingi zinazotuumiza tz. lazima ziondolewe ili watu wengi walipe kodi hapa tz sio kuwaumiza public servants na wafanya biashara wachache wasiojua kukwepa kodi.
   
 19. m

  mamanalia JF-Expert Member

  #19
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 671
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mkuu kupambana na ufisadi ni basic task ya rais wa nchi. so kama rais hataki kufanya hivyo na bado mmemchagua tufanye nini. Lazima tufikirie njia zingine ambazo zitaongezea kipato nchi. Nssf n the likes lazima wawekeze kwenye NHC na nishati kama umeme na huku tukikusanya kodi kwa mwananchi yeyote anayeingiza kipato kikubwa kama vile wenye nyumba.

  hata ukibisha huo ndo msingi wa maendeleo ya taifa lolote. Try to Expand your horizon.
   
 20. malkiory

  malkiory JF-Expert Member

  #20
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 272
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zitto anatumiwa na CCM kuimaliza Chadema. Kimsing yeye ndiyo chanzo cha migogoro ndani ya Chadema. Ni mbinafsi na mpenda madaraka.
   
Loading...