Hongera Waziri Ummy Mwalimu kwa mkakati mpya wa kupambana na COVID19

Mudawote

JF-Expert Member
Jul 10, 2013
7,394
2,000
Great Thinkers, ujumbe unaofuata unaonesha jinsi wizara ya afya ilivyojipanga kukabiliana na COVID19, kikao alichofanya na chama cha Madakitari (chini ya rais wao Dr Osati) kinatoa matumaini mapya kwa watanzania.

Mrejesho wa kikao cha wanataaluma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Habari za leo

Jana tarehe 27 Aprili, 2020; vyama vya kitaaluma vya afya nchini kikiwemo MAT tulikutana na timu ya Wizara ya Afya kujadiliana kuhusu mwenendo wa wa COVID-19 nchini. Kikao hiki ni matokeo ya mkutano wa vyama vyote wa tarehe 26 Aprili, 2020 kilichofanyika kupitia "zoom ". Tulijadili yafuatayo.

1. Upatikanaji wa PPEs Wizara

Mheshimiwa. Waziri Ummy Ally Mwalimu alisema tayari wameagiza mzigo wa PPEs unaotosheleza matumizi ya mwezi mzima; mzigo huo unategemewa kufika wakati wowote wiki hii. Pia wizara imepata fedha kiasi cha shilingi za kitanzania 9.6Billioni walioielekeza MSD kwa ajili ya kuagiza mzigo mwingine wa PPEs.

2. Wagonjwa kukataliwa kwenye hospitali mbalimbali

CMO na RMOs wameagizwa kushughulikia swala hili mara moja. Hii itaambatana na kuangalia upya mwongozo wa utumiaji wa PPEs bila wafanyakazi kuambukizwa. Sambamba na hilo watumishi wamehimizwa kufuata mwongozo wa IPC ili kuepuka maambukizi na hivyo wasiwakatae wagonjwa wanaopewa rufaa au kuja kwenye vituo vyao.

Kikao pia kiliridhia kwamba mafunzo ya IPC lazima yaendelee kwenye kila kituo cha kutolea huduma za afya. Pamoja na hayo tulikubaliana kuwa isolation centers ziongezeke hata kwenye hospitali za binafsi (private hospitals); kwa kuanzia hospitali hizi kupitia kwa Association of Private Health Facilities in Tanzania (APHFTA) wamekubaliana kutenga isolation za level 3 (level1, 2 and 3) katika kila wilaya ya mkoa wa Dar es Salaam na baadae mikoani, kwa ajili ya kuwaweka wagonjwa.

3. Ucheleweshwaji wa majibu ya COVID-19

Wizara imekubali kuongeza vituo vitatu kati ya tisa zenye uwezo wa kupima COVID-19. Kuanzia Jumanne ya wiki ijayo ya tarehe tarehe 5 May, 2020; maabara ya NIMR Dodoma itaanza kutoa majibu, ikifuatiwa na Mwanza na Mbeya. Changamoto imekuwa ni uwepo wa wataalam wanane tu wa maabara wanaoweza kuchakata majibu ya COVID-19. Kwa hiyo Mafunzo kwa wataalam wengine yameanza na watasambazwa kwenye vituo husika.

4. Mazishi ya waliofariki

Ikitokea mgonjwa amefariki kwenye hospitali, ndugu inabidi wahusishwe iwezekanavyo chini ya uangalizi wa wataalam wa afya kutoka manispaa husika kuhusu mazishi na eneo la kuzikia. Mganga mkuu wa wilaya (DMO) husika ataarifiwe kwa msaada zaidi ikiwa ni pamoja na magari na utaratibu wa mazishi bila kupoteza muda zaidi.

5. Contact tracing

Kwa upande wa Dar es Salaam ambapo tayari kuna maambukizi mengi kwenye jamii ni changamoto kuendelea na kuwatafuata "contacts" na pia ni vigumu kuwa weka wote ‘’isolation’’. Wizara walishauri kwa hatua tuliyo nayo sasa kwa mkoa wa Dar es Salaam kama mtu anahisi kuwa na dalili za COVID-19 aende kwenye kituo husika kwa ajili ya kuchukuliwa vipimo, na kurudi nyumbani huku wakiendelea kuchukua tahadhari zote ikiwemo kuvaa Barakoa na kujitenga na wengine. Mikoa mwingine ambayo ugonjwa haujasambaa sana waendelee na utaratibu wa "contact tracing".

6. Kuweka wagonjwa wenye dalili ndogo ndogo kwenye isolations

Kuhusu hili tulijadiliana na hatukufikia muafaka. Mheshimiwa Waziri akaomba wanataaluma tujadiliane halafu tumshauri kwenye hili. Maswali yakiwa; Je ni sahihi kuwa weka wagonjwa wenye dalili ndogo ndogo kwenye isolation ambazo tayari zimejaa au tuwape ushauri halafu wajitenge nyumbani mpaka Ikitokea wana dalili za hatari?. Hii itabidi tuitolee maoni sisi kama wanataaluma

7. Upungufu wa Damu salama kipindi hiki

kumeonekana kuna upungufu mkubwa sana wa damu salama katika benki za damu hasa kwa Dar es Salaam. Wito umetolewa kwa hospitali zote kupunguza kufanya/kutoa huduma ya upasuaji usio wa dharura ili kupunguza matumizi ya damu.

8. Utafiti kwenye eneo la COVID-19

Taasisi ya taifa ya utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR) tayari inaendelea na tafiti tatu juu ya COVID-19 na pia imetoa mwongozo wa utafiti kwa wakati huu wa COVID-19. Utafiti pia unahusisha dawa za miti Shamba (tiba mbadala) ikiwa ni pamoja na kujifukiza.

9. Ufafanuzi ya juu ya kauli ya waziri kuwa hakuna watumishi walioambukizwa

Mheshimiwa Waziri alisema alichomaanisha ni kuwa hakuna mtumishi anayehudumia wagonjwa kwenye isolations aliyeambukizwa. Kwa sababu labda walipewa Mafunzo zaidi ya namna ya kujikinga. Alisema anajua kuwa kuna watumishi wameambukizwa wakiwa EMD/Mapokezi na OPDs (idara ya magonjwa ya nje). Kwahiyo ameomba Mafunzo zaidi yaelekezwa kwa watumishi wote.

NB: Tunaomba maoni yenu juu ya kipengela Namba 6 hapo juu.

Nawasilisha

Dr Elisha Osati, Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT).
 

Mudawote

JF-Expert Member
Jul 10, 2013
7,394
2,000
Tunataka kujua watu wangapi wamepimwa wangapi wanaugua, wangapi wako karantini na wangapi wamepoteza maisha.
Ndukidi hayo mambo ya kupanikishana tuachane nayo, tuweke mikakati ya mass testing ila hakuna mambo ya kutoa taarifa, kwa sababu hatuna briefing ya HIV au Kisukari so why iwe COVID19???? Kwanini tukopy kila kitu?

Je kuna umuhimu wa kutaja maambukizi ya malaria? Cancer??? Au kuna umuhimu wa kutaja vifo vya malaria??? Nadhani mikakati ya kujikinga ni bora zaidi. Tuungane kumpongeza Waziri Ummy kwa hatua aliyochukua
 

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
6,940
2,000
Ni ombi langu kuwa watumishi wa afya wote watumie mask za N95. Hats kama mask za Vitambaa zimeruhusiwa kwenye jamii kwa ujumla ukweli ni kwamba mhudumu wa afya kumpàtia mask za vitambaa ni sawa na kumpa rungu askari aliyeko mstari wa mbele kwenye mapambano badsla ya machine gun.

Rsis Magufuli aliposhauri watu wajitengenezee mask za vitambaa hakumaanisha kuwa amebariki madaktari na manesi wapewe mask hizo!! Kuna taarifa ya baadhi ya hospital kuwapa watumishi wao mask za vitambaa!! Huu utakuwa ni upotoshaji mkubwa sana wa kauli ya Rais.

Napendekeza Wizara itoe tamko rasmi la kuzuia wahudumu wa afya kupewa mask za vitambaa.

Rais alishauri mask za vitambaa kwa jamii kwa sababu hali halisi hairuhusu kila mtu kumudu mask rasm. Hata Marekani wameruhusu mask za vitambaa lakini si kwa watumishi wa afya walioko mstari wa mbele kwenye vita hii.
 

Ndukidi

JF-Expert Member
Jun 30, 2012
1,436
2,000
Ndukidi hayo mambo ya kupanikishana tuachane nayo, tuweke mikakati ya mass testing ila hakuna mambo ya kutoa taarifa, kwa sababu hatuna briefing ya HIV au Kisukari so why iwe COVID19???? Kwanini tukopy kila kitu? Je kuna umuhimu wa kutaja maambukizi ya malaria? Cancer??? Au kuna umuhimu wa kutaja vifo vya malaria??? Nadhani mikakati ya kujikinga ni bora zaidi. Tuungane kumpongeza Waziri Ummy kwa hatua aliyochukua
Kwa hiyo mnaogopa kutoa taarifa, yaani kutangaza mwenendo wa ugonjwa pia ni kitu cha kuogopa ? kuna nini sasa cha kuficha iwapohuu ni ugonjwa wa dunia nzima?, kumbuka hii ni pandemic, ni ugonjwa unaosambaa kwa kasi sio sawa na magonjwa mengine, hatua zinatakiwa kuchukuliwa haraka kutokana na mwenendo wa ugonjwa.Acheni kujidanganya na kudanganywa tunakufa kijinga.
 

cutelove

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
2,703
2,000
Tunaomba kujua mikakati ya kupambana na huu ugonjwa vijijini ambapo hawana elimu ya kutosha kuhusu dalili,maambukizi,na miundombinu ya huko,maana Tanzania ndo taifa litakuwa na wagonjwa wengi mpaka ndani ndani huko vijijini maana ni free movement from no where to known where

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom