Hongera Waziri Ummy Mwalimu kwa mkakati mpya wa kupambana na COVID19

Ukichanganya kilichozungumzwa hapo utaona bado kuna tatizo. Mengi ni kutibu na machache ni ya kujikinga. Na bado hatujaoneshwa mashine ngapi za usaidizi wa kupumua zinahitajika na zipo ngapi.

Utoaji taarifa sahihi pia halijazungumzwa
 
Niliongelea maambukizi ya corona.
je inasaidia nini kujua idadi ya wagonjwa wa COVID19? kama tu wanaoambukizwa HIV huwa hatupewi briefing iweje mtake hiyo COVID19? Je umesikia USA Drs wanalazimishwa kuandika COVID19 kama sababu ya kifo hata kama chanzo ni kisukari?
 
Kipengele no 5 ni dhahiri serikali imeshazidiwa na wagonjwa,kuwaacha watu wenye dalili za corona majumbani ni hatari,

Huwezi mwacha mgonjwa nyumbani umwambie aji isolate mwenyewe,huu ugonjwa wagonjwa wanatabia yakuzidiwa ghafla,hivi akizidiwa nyumbani atapataje tiba ya dharula?

Nashauri ni bora kama tatizo ni pesa basi simamisheni miradi mikubwa tupambane na corona,stiglers na reli ya mwendokasi vingesubiri.

Mh Magufuli wewe ni jembe hasa lakini kwenye corona serikali bado haijatoa uzito unaolingana na tatizo.

Leo tunawezajigamba kwamba hatuifungi dar lakini hali itakapokuwa mbaya hakika dar itajifunga yenyewe.

Mwanzo tuligoma kabisa kutofunga usafiri wa ndege kwa safari za kimataifa,nini hatma ya misimamo yetu leo?
 
Ukichanganya kilichozungumzwa hapo utaona bado kuna tatizo. Mengi ni kutibu na machache ni ya kujikinga. Na bado hatujaoneshwa mashine ngapi za usaidizi wa kupumua zinahitajika na zipo ngapi.

Utoaji taarifa sahihi pia halijazungumzwa
Taarifa sahihi za nini???? Kwenye kujikinga hapo ok
 
Shida inaanzia kwa yule.jamaa aliyekaa na vyombo vya ulinzi na usalama....
 
Hii mikakati yote ilitakiwa iwe mapema kabla ya ugonjwa kuenea kama ilivyo sasa

Sent using kidole gumba
 
Ndukidi hayo mambo ya kupanikishana tuachane nayo, tuweke mikakati ya mass testing ila hakuna mambo ya kutoa taarifa, kwa sababu hatuna briefing ya HIV au Kisukari so why iwe COVID19???? Kwanini tukopy kila kitu? Je kuna umuhimu wa kutaja maambukizi ya malaria? Cancer??? Au kuna umuhimu wa kutaja vifo vya malaria??? Nadhani mikakati ya kujikinga ni bora zaidi. Tuungane kumpongeza Waziri Ummy kwa hatua aliyochukua
Mkuu unajua maana ya pandemic disease? Huwezi ukaifananisha cancer na H I V kama pandemic wakati umeambiwa Corona ni pandemic na tunatakiwa tuukabili ugonjwa seriously na kwa kiwango cha fast kupunguza maambukizi na vifo kwa muda huo huo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
je inasaidia nini kujua idadi ya wagonjwa wa COVID19? kama tu wanaoambukizwa HIV huwa hatupewi briefing iweje mtake hiyo COVID19? Je umesikia USA Drs wanalazimishwa kuandika COVID19 kama sababu ya kifo hata kama chanzo ni kisukari?
Huna hoja, hata WHO sasa hivi wana tanga za idadi ya waathirika na vifo vya corona. Kwanini hawaamki kila siku na kutangaza takwimu za malaria na HIV?
 
Kwa hiyo mnaogopa kutoa taarifa, yaani kutangaza mwenendo wa ugonjwa pia ni kitu cha kuogopa ? kuna nini sasa cha kuficha iwapohuu ni ugonjwa wa dunia nzima?, kumbuka hii ni pandemic, ni ugonjwa unaosambaa kwa kasi sio sawa na magonjwa mengine, hatua zinatakiwa kuchukuliwa haraka kutokana na mwenendo wa ugonjwa.Acheni kujidanganya na kudanganywa tunakufa kijinga.
Omba msamaha faster, nakuona unavyohangaika, very soon naanika uchafu wako. Kama hatuna briefing ya maambukizi ya HIV basi si muhimu covid19
 
Great Thinkers, ujumbe unaofuata unaonesha jinsi wizara ya afya ilivyojipanga kukabiliana na COVID19, kikao alichofanya na chama cha Madakitari (chini ya rais wao Dr Osati) kinatoa matumaini mapya kwa watanzania.

Mrejesho wa kikao cha wanataaluma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Habari za leo

Jana tarehe 27 Aprili, 2020; vyama vya kitaaluma vya afya nchini kikiwemo MAT tulikutana na timu ya Wizara ya Afya kujadiliana kuhusu mwenendo wa wa COVID-19 nchini. Kikao hiki ni matokeo ya mkutano wa vyama vyote wa tarehe 26 Aprili, 2020 kilichofanyika kupitia "zoom ". Tulijadili yafuatayo.

1. Upatikanaji wa PPEs Wizara

Mheshimiwa. Waziri Ummy Ally Mwalimu alisema tayari wameagiza mzigo wa PPEs unaotosheleza matumizi ya mwezi mzima; mzigo huo unategemewa kufika wakati wowote wiki hii. Pia wizara imepata fedha kiasi cha shilingi za kitanzania 9.6Billioni walioielekeza MSD kwa ajili ya kuagiza mzigo mwingine wa PPEs.

2. Wagonjwa kukataliwa kwenye hospitali mbalimbali


CMO na RMOs wameagizwa kushughulikia swala hili mara moja. Hii itaambatana na kuangalia upya mwongozo wa utumiaji wa PPEs bila wafanyakazi kuambukizwa. Sambamba na hilo watumishi wamehimizwa kufuata mwongozo wa IPC ili kuepuka maambukizi na hivyo wasiwakatae wagonjwa wanaopewa rufaa au kuja kwenye vituo vyao.

Kikao pia kiliridhia kwamba mafunzo ya IPC lazima yaendelee kwenye kila kituo cha kutolea huduma za afya. Pamoja na hayo tulikubaliana kuwa isolation centers ziongezeke hata kwenye hospitali za binafsi (private hospitals); kwa kuanzia hospitali hizi kupitia kwa Association of Private Health Facilities in Tanzania (APHFTA) wamekubaliana kutenga isolation za level 3 (level1, 2 and 3) katika kila wilaya ya mkoa wa Dar es Salaam na baadae mikoani, kwa ajili ya kuwaweka wagonjwa.

3. Ucheleweshwaji wa majibu ya COVID-19

Wizara imekubali kuongeza vituo vitatu kati ya tisa zenye uwezo wa kupima COVID-19. Kuanzia Jumanne ya wiki ijayo ya tarehe tarehe 5 May, 2020; maabara ya NIMR Dodoma itaanza kutoa majibu, ikifuatiwa na Mwanza na Mbeya. Changamoto imekuwa ni uwepo wa wataalam wanane tu wa maabara wanaoweza kuchakata majibu ya COVID-19. Kwa hiyo Mafunzo kwa wataalam wengine yameanza na watasambazwa kwenye vituo husika.

4. Mazishi ya waliofariki

Ikitokea mgonjwa amefariki kwenye hospitali, ndugu inabidi wahusishwe iwezekanavyo chini ya uangalizi wa wataalam wa afya kutoka manispaa husika kuhusu mazishi na eneo la kuzikia. Mganga mkuu wa wilaya (DMO) husika ataarifiwe kwa msaada zaidi ikiwa ni pamoja na magari na utaratibu wa mazishi bila kupoteza muda zaidi.


5. Contact tracing

Kwa upande wa Dar es Salaam ambapo tayari kuna maambukizi mengi kwenye jamii ni changamoto kuendelea na kuwatafuata "contacts" na pia ni vigumu kuwa weka wote ‘’isolation’’. Wizara walishauri kwa hatua tuliyo nayo sasa kwa mkoa wa Dar es Salaam kama mtu anahisi kuwa na dalili za COVID-19 aende kwenye kituo husika kwa ajili ya kuchukuliwa vipimo, na kurudi nyumbani huku wakiendelea kuchukua tahadhari zote ikiwemo kuvaa Barakoa na kujitenga na wengine. Mikoa mwingine ambayo ugonjwa haujasambaa sana waendelee na utaratibu wa "contact tracing".


6. Kuweka wagonjwa wenye dalili ndogo ndogo kwenye isolations

Kuhusu hili tulijadiliana na hatukufikia muafaka. Mheshimiwa Waziri akaomba wanataaluma tujadiliane halafu tumshauri kwenye hili. Maswali yakiwa; Je ni sahihi kuwa weka wagonjwa wenye dalili ndogo ndogo kwenye isolation ambazo tayari zimejaa au tuwape ushauri halafu wajitenge nyumbani mpaka Ikitokea wana dalili za hatari?. Hii itabidi tuitolee maoni sisi kama wanataaluma

7. Upungufu wa Damu salama kipindi hiki

kumeonekana kuna upungufu mkubwa sana wa damu salama katika benki za damu hasa kwa Dar es Salaam. Wito umetolewa kwa hospitali zote kupunguza kufanya/kutoa huduma ya upasuaji usio wa dharura ili kupunguza matumizi ya damu.


8. Utafiti kwenye eneo la COVID-19

Taasisi ya taifa ya utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR) tayari inaendelea na tafiti tatu juu ya COVID-19 na pia imetoa mwongozo wa utafiti kwa wakati huu wa COVID-19. Utafiti pia unahusisha dawa za miti Shamba (tiba mbadala) ikiwa ni pamoja na kujifukiza.


9. Ufafanuzi ya juu ya kauli ya waziri kuwa hakuna watumishi walioambukizwa


Mheshimiwa Waziri alisema alichomaanisha ni kuwa hakuna mtumishi anayehudumia wagonjwa kwenye isolations aliyeambukizwa. Kwa sababu labda walipewa Mafunzo zaidi ya namna ya kujikinga. Alisema anajua kuwa kuna watumishi wameambukizwa wakiwa EMD/Mapokezi na OPDs (idara ya magonjwa ya nje). Kwahiyo ameomba Mafunzo zaidi yaelekezwa kwa watumishi wote.


NB: Tunaomba maoni yenu juu ya kipengela Namba 6 hapo juu.


Nawasilisha

Dr Elisha Osati, Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT).
Dr ulimboka alikuwepo mtu
 
Huna hoja, hata WHO sasa hivi wana tanga za idadi ya waathirika na vifo vya corona. Kwanini hawaamki kila siku na kutangaza takwimu za malaria na HIV?
Sky Eclat usipende kukariri, ni upumbavu kutangaza maambukizi ya COVID19 wakati kuna magonjwa mengine mengi huwa hatutangazi.
 
Dr Elisha Osati nikuulize: Je una habari kuwa kuna wahudumu wa afya wanaopewa mask za vitambaa? Je ni sahihi kufanya hivyo? Je waliotoa mask za vitambaa je wamekiuka utaratibu? Je watachukuliwa hatua zozote? Vinginevyo mtakuwa mnatia doa ushauri mzuri wa Rais wetu.
 
Huna hoja, hata WHO sasa hivi wana tanga za idadi ya waathirika na vifo vya corona. Kwanini hawaamki kila siku na kutangaza takwimu za malaria na HIV?
WHO siyo baba yetu wala mama yetu tufuate kila wanachofanya,sisi ni nchi huru inayojitegemea bi dada Sky Eclat
 
Back
Top Bottom