Ila ni mwanzo mzuri wa kuwaweka watu sawa pia kuwa wamoja kama issue ndogo ndogo zinatatuliwa kwa uharakaOSBP ni convenience ya usafiri tu, haiondoi yaliyo kwenye mioyo ya watz na wakny.
OSBP ni convenience ya usafiri tu, haiondoi yaliyo kwenye mioyo ya watz na wakny.
Ni muda tangu nitumie mpaka wa Namanga, kawaida nimezoea JNIA moja kwa moja. Leo nimepita hapo Namanga na kushangaa jinsi mambo yamebadilika, wanacho kitu wanaita One Stop Border Post (OSBP), kwamba wahudumu/afisa wa uhamiaji pande zote mbili wanapatikana sehemu moja, inategemea unatokea wapi.
Yaani kama unatokea Kenya, unavuka mpaka na kwenda moja kwa moja uhamaji na utawakuta afisa wa Kenya ndani ya jemgo la uhamiaji Tanzania, hivyo shughuli zako unazifanyia sehemu moja, vile vile kama unatokea Tanzania, unavuka na kuingia Kenya ambapo unawakuta afisa wa Tanzania ndani ya ofisi za Wakenya, wote wanakumalizia shughuli zako papo hapo, sio kama ilivyokua usumbufu balaa, mifoleni Kenya halafu uvuke ukapange foleni zingine Tanzania.
Huu ni ushirikiano mzuri sana kama kweli tunamaanisha, ujenzi ulianza enzi za Kikwete na mzee Kibaki, naomba huu ushiriakiano udumishwe maana ni nafuu kwa sisi tunaofanya biashara zetu pande zote mbili.
Tuache kutia vifaranga viberiti na kukamata ng'ombe na kuwapiga minada, nina uhakika kuna jinsi ya kurekebisha wakati kuna matatizo yoyote, sio kuchukua hatua za chuki na mihemko.
Yaani uliingia county yetu ya Kajiado na hukuona haja ya kunifahimisha? Mkuu kwani wewe ni mheshimiwa wa sampuli gani?
Yaani ikitokeaga nchi hazina uhusiano mzuri wafanyabiashara ndio huugulia maumivu zaidi!Huu ni ushirikiano mzuri sana kama kweli tunamaanisha, ujenzi ulianza enzi za Kikwete na mzee Kibaki, naomba huu ushiriakiano udumishwe maana ni nafuu kwa sisi tunaofanya biashara zetu pande zote mbili.
Mikiki mikiki eeh. Haina noma japo Kajiado watu huja kushangaa shangaa na meno yao tu. Sasa hivi nyama haziliki labda tu kwa macho. Kiangazi jombaa labda Mwezi wa kumi na mbili ndo mvua imeanza kunyesha.Te te te!! Hebu waza, kutoka Nairobi nasafiri kwa gari binafsi inayochezea kwenye alama ya 120km/h halafu iniache Namanga na kugeuza, kuanzia hapo mikimbio ya kujaribu kupigiwa mihuri fasta na kutafuta usafiri wa haraka hadi Arusha, hatimaye taxi hadi KIA, yaani mchakamchaka hakuna nafasi ya kuja kushangaa shangaa hapo Kajiado.
Japo nitakuja tule nyama.
Unakimbia Kenya kwani bado kuna vurugu? hahahahahaah nakutania MK254
Hehehe Hamna, ni shughuli tu za kusaka mkwanja tu, unajua hawa wanasiasa wanataka tupige kura kila siku, siasa haziishi hawafahamu tuna majukumu mengine. Wakithubutu kuagiza tupige kura tena nikiwa nje ya nchi nitaawachia wajipigie wenyewe.
Hapa MK254 unatuangusha kama Great Thinker wa JamiiForums. Suala la vifaranga waliosafirishwa bila kufuta utaratibu, viwango vya chanjo/afya/magonjwa/ kuhamisha mifugo na kuku ili kuepusha magonjwa kwa binadamu na mifugo ni suala nyeti na halina mzaha.By MK254, Tuache kutia vifaranga viberiti .........