Hongera uhamiaji Kenya na Tanzania kwa OSBP

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
31,516
47,751
Ni muda tangu nitumie mpaka wa Namanga, kawaida nimezoea JNIA moja kwa moja. Leo nimepita hapo Namanga na kushangaa jinsi mambo yamebadilika, wanacho kitu wanaita One Stop Border Post (OSBP), kwamba wahudumu/afisa wa uhamiaji pande zote mbili wanapatikana sehemu moja, inategemea unatokea wapi.

Yaani kama unatokea Kenya, unavuka mpaka na kwenda moja kwa moja uhamaji na utawakuta afisa wa Kenya ndani ya jemgo la uhamiaji Tanzania, hivyo shughuli zako unazifanyia sehemu moja, vile vile kama unatokea Tanzania, unavuka na kuingia Kenya ambapo unawakuta afisa wa Tanzania ndani ya ofisi za Wakenya, wote wanakumalizia shughuli zako papo hapo, sio kama ilivyokua usumbufu balaa, mifoleni Kenya halafu uvuke ukapange foleni zingine Tanzania.

Huu ni ushirikiano mzuri sana kama kweli tunamaanisha, ujenzi ulianza enzi za Kikwete na mzee Kibaki, naomba huu ushiriakiano udumishwe maana ni nafuu kwa sisi tunaofanya biashara zetu pande zote mbili.
Tuache kutia vifaranga viberiti na kukamata ng'ombe na kuwapiga minada, nina uhakika kuna jinsi ya kurekebisha wakati kuna matatizo yoyote, sio kuchukua hatua za chuki na mihemko.
 
Hili ni jambo zuri sana kwani sisi ni ndugu. Wakoloni ndiyo waliokuja kuweka mipaka na kututenganisha.
 
Yaani uliingia county yetu ya Kajiado na hukuona haja ya kunifahimisha? Mkuu kwani wewe ni mheshimiwa wa sampuli gani? Hiyo OSBP ilikuwa kilio kwa wanabishara wadogo wadogo wa hapo Manga kama miaka miwili hivi iliyopita. Ilikuja na bomoa bomoa ya kiaina, upanuzi wa barabara, majengo mapya, hama hama na sheria za ajabu ajabu n.k. Ilichukua vichwa vigumu muda mrefu sana kabla ya wao kuielewa vyema.
 
Ni muda tangu nitumie mpaka wa Namanga, kawaida nimezoea JNIA moja kwa moja. Leo nimepita hapo Namanga na kushangaa jinsi mambo yamebadilika, wanacho kitu wanaita One Stop Border Post (OSBP), kwamba wahudumu/afisa wa uhamiaji pande zote mbili wanapatikana sehemu moja, inategemea unatokea wapi.

Yaani kama unatokea Kenya, unavuka mpaka na kwenda moja kwa moja uhamaji na utawakuta afisa wa Kenya ndani ya jemgo la uhamiaji Tanzania, hivyo shughuli zako unazifanyia sehemu moja, vile vile kama unatokea Tanzania, unavuka na kuingia Kenya ambapo unawakuta afisa wa Tanzania ndani ya ofisi za Wakenya, wote wanakumalizia shughuli zako papo hapo, sio kama ilivyokua usumbufu balaa, mifoleni Kenya halafu uvuke ukapange foleni zingine Tanzania.

Huu ni ushirikiano mzuri sana kama kweli tunamaanisha, ujenzi ulianza enzi za Kikwete na mzee Kibaki, naomba huu ushiriakiano udumishwe maana ni nafuu kwa sisi tunaofanya biashara zetu pande zote mbili.
Tuache kutia vifaranga viberiti na kukamata ng'ombe na kuwapiga minada, nina uhakika kuna jinsi ya kurekebisha wakati kuna matatizo yoyote, sio kuchukua hatua za chuki na mihemko.

Well Said MK254.
 
Yaani uliingia county yetu ya Kajiado na hukuona haja ya kunifahimisha? Mkuu kwani wewe ni mheshimiwa wa sampuli gani?

Te te te!! Hebu waza, kutoka Nairobi nasafiri kwa gari binafsi inayochezea kwenye alama ya 120km/h halafu iniache Namanga na kugeuza, kuanzia hapo mikimbio ya kujaribu kupigiwa mihuri fasta na kutafuta usafiri wa haraka hadi Arusha, hatimaye taxi hadi KIA, yaani mchakamchaka hakuna nafasi ya kuja kushangaa shangaa hapo Kajiado.

Japo nitakuja tule nyama.
 
Huu ni ushirikiano mzuri sana kama kweli tunamaanisha, ujenzi ulianza enzi za Kikwete na mzee Kibaki, naomba huu ushiriakiano udumishwe maana ni nafuu kwa sisi tunaofanya biashara zetu pande zote mbili.
Yaani ikitokeaga nchi hazina uhusiano mzuri wafanyabiashara ndio huugulia maumivu zaidi!

Hongera JMT na Kenya!
 
Osbd ipo kila mikoa ya mpakani holili kule ipo na kesho Rais Magufuli na Museveni watazindua Osbd ya mtukula boarder ya Tanzania and Uganda leo anazindua Kagera Airport juzi liliwekwa jiwe la msingi mkoa wa Geita Airport.
 
Te te te!! Hebu waza, kutoka Nairobi nasafiri kwa gari binafsi inayochezea kwenye alama ya 120km/h halafu iniache Namanga na kugeuza, kuanzia hapo mikimbio ya kujaribu kupigiwa mihuri fasta na kutafuta usafiri wa haraka hadi Arusha, hatimaye taxi hadi KIA, yaani mchakamchaka hakuna nafasi ya kuja kushangaa shangaa hapo Kajiado.

Japo nitakuja tule nyama.
Mikiki mikiki eeh. Haina noma japo Kajiado watu huja kushangaa shangaa na meno yao tu. Sasa hivi nyama haziliki labda tu kwa macho. Kiangazi jombaa labda Mwezi wa kumi na mbili ndo mvua imeanza kunyesha.
 
Hii ni hatua Nzuri sana, Kama hili limewezekana la Ngombe na vifaranga pia linawezekana, Viva east africa community.
 
Namanga walichelewa Mtukula, na Busia walilifanya mapema kabisa . wenzetu wanataka East Africa federation lakini Watanzania hawataki kwa sababu ya Roho ya Korosho ( Roho mbaya)
 
Unakimbia Kenya kwani bado kuna vurugu? hahahahahaah nakutania MK254

Hehehe Hamna, ni shughuli tu za kusaka mkwanja tu, unajua hawa wanasiasa wanataka tupige kura kila siku, siasa haziishi hawafahamu tuna majukumu mengine. Wakithubutu kuagiza tupige kura tena nikiwa nje ya nchi nitaawachia wajipigie wenyewe.
 
hahahahahahaahahaha

MK254,
By MK254, Tuache kutia vifaranga viberiti .........
Hapa MK254 unatuangusha kama Great Thinker wa JamiiForums. Suala la vifaranga waliosafirishwa bila kufuta utaratibu, viwango vya chanjo/afya/magonjwa/ kuhamisha mifugo na kuku ili kuepusha magonjwa kwa binadamu na mifugo ni suala nyeti na halina mzaha.
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom