MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 31,757
- 48,407
Ni muda tangu nitumie mpaka wa Namanga, kawaida nimezoea JNIA moja kwa moja. Leo nimepita hapo Namanga na kushangaa jinsi mambo yamebadilika, wanacho kitu wanaita One Stop Border Post (OSBP), kwamba wahudumu/afisa wa uhamiaji pande zote mbili wanapatikana sehemu moja, inategemea unatokea wapi.
Yaani kama unatokea Kenya, unavuka mpaka na kwenda moja kwa moja uhamaji na utawakuta afisa wa Kenya ndani ya jemgo la uhamiaji Tanzania, hivyo shughuli zako unazifanyia sehemu moja, vile vile kama unatokea Tanzania, unavuka na kuingia Kenya ambapo unawakuta afisa wa Tanzania ndani ya ofisi za Wakenya, wote wanakumalizia shughuli zako papo hapo, sio kama ilivyokua usumbufu balaa, mifoleni Kenya halafu uvuke ukapange foleni zingine Tanzania.
Huu ni ushirikiano mzuri sana kama kweli tunamaanisha, ujenzi ulianza enzi za Kikwete na mzee Kibaki, naomba huu ushiriakiano udumishwe maana ni nafuu kwa sisi tunaofanya biashara zetu pande zote mbili.
Tuache kutia vifaranga viberiti na kukamata ng'ombe na kuwapiga minada, nina uhakika kuna jinsi ya kurekebisha wakati kuna matatizo yoyote, sio kuchukua hatua za chuki na mihemko.