Bantugbro
JF-Expert Member
- Feb 22, 2009
- 4,473
- 4,253
Katika hali ya kushangaza na kusikitisha, vyombo vyetu vya habari hasa television vimeshindwa kuwaonyesha watanzania mechi ya mpira wa miguu kati ya timu yetu ya Taifa (Taifa Stars) iliyokuwa ikicheza dhidi ya Moroco.
Wakati vituo vya binafsi vikiendelea kurusha vipindi vyao vya kawaida, Television ya Taifa (TBC) wao walijikita uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kurusha matangazo ya moja kwa moja juu ya ujio wa raisi wa China.
Hivi kweli watanzania tumefika mahali pa kuwathamini wageni kuliko timu yetu ya Taifa? Naamini watanzania walioko Tarime, Tandahimba, Kakonko, Pemba, Namanyele ama Tunduru wangetamani kuishuhudia timu yao ya Taifa kuliko raisi wa China asiye na maslahi yoyote na maisha yao.
Ni dhahiri kuwa viongozi wetu wa sasa wameishiwa kabisa na uzalendo, na ndio maana wanaendelea kufanya mambo ya kijinga huku wananchi wakiwakodolea macho bila kuchukua hatua.
Tuwe na shukrani jamani, umeshasahau hata huo uwanja wa mpira wamejenga kwa ufundi na pesa yao (baada ya Mkapa kutembeza bakuli:A S shade🙂...Huyu ataondoka na hatarudi kwa mda mrefu, wakati mechi zinachezwa kila wiki...Tuache kulalamika kwa kila jambo.