Hongera sana Stars! Jana mmecheza mpira mzuri sana. Morroco walitaka kupambana lakini hatimaye walikubali kushindwa na wakabaki wanakaba kwa macho! kwa tuliokuwa uwanjani tunajua almanusra ziwe tano jana! Ilikuwa siku nzuri sana kwa Tanzania na Mungu aendelee kutubariki hivi hivi! Kwa hakika tunao uwezo wa kuongeoza hili kundi. Hata Ivory Coast tukijipanga vizuri na kuwapa motisha wa kutosha vijana na kuwatuliza kisaikolojia, lazima tutawafunga hapa kwetu huo mwezi wa sita. Morroco kwao wala hawatatusumbua kihivyo kama ambavyo tulihofia. kwa sisi tuliocheza mpira ni wachezaji very average sana. Tukitulia, hasa kwenye midfield, na hivi wanatujua tulivyo wabaya kwenye counter attacks, lazima tutawafunga kwao! na hapo ndo kiama kitakapowashukia Ivory Coast watakapotua hapa! Mungu Ibariki Tanzania tena na tena!!!