Hongera sana kwa Waziri Mkuu wa India kwa kudumisha na kujivunia utamaduni wa India katika mavazi

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,663
18,037
1653441859704.png

Kwa kweli huyu waziri mkuu wa India anafurahisha sana!! Anajivunia uvaaji wa kihindi kwa kujiamini kabisa!! Waarabu pia nawapongeza sana na wanigeria!! Anaitangaza nchi yake sawasawa!! Ana msimamo, ndio maana hawezi kuyumbishwa propaganda za nchi za magharibi!!
 
Kuna kipindi hapa Tanzania Ilikazaniwa sana suala kuwa na vazi la kitaifa, sijui mkakati huo uliishia wapi? Wala hatujawahi kuwa na mapatano vazi letu la Taifa ni lipi!! Vazi ambalo ukilivaa kila anayekuona anakuwa ameiona Tanzania! Anakutambua kuwa wewe ni mtanzania kwa jinsi ulivyovaa!!
 
Ata sijui umeandika nini hapa kwani mama samia amewahi kwenda kichwa wazi huko anakoenda nje? Ni jambo la kawaida sana kwenye kivazi wala sioni haja kuleta hii thread, mimi nadhan ungetaka kujua kwanini India inaunga mkono ujio wa Biden.
 
Ata sijui umeandika nini hapa kwani mama samia amewahi kwenda kichwa wazi huko anakoenda nje? ni jambo la kawaida sana kwenye kivazi wala sioni haja kuleta hii thread, mimi nadhan ungetaka kujua kwanini India inaunga mkono ujio wa Biden
Ninazungumzia vazi la kitaifa!! Mama Samia havaagi vazi la kitaifa!! Vazi lake ni la kidini!! Popote utakapomwona utajua kuwa yeye ni dini gani lakini hapa tunazungumzia vazi la kitaifa linalomtambulisha mtu kuwa ni mtanzania! Hadi sasa mtanzania huko nchi za nje huwezi kumtambua kwa vazi lake kuwa ni mtanzania!
 
Kwamba wakristo hawafungi ushungi?
 
Ninazungumzia vazi la kitaifa!! Mama Samia havaagi vazi la kitaifa!! Vazi lake ni la kidini!! Popote utakapomwona utajua kuwa yeye ni dini gani lakini hapa tunazungumzia vazi la kitaifa linalomtambulisha mtu kuwa ni mtanzania! Hadi sasa mtanzania huko nchi za nje huwezi kumtambua kwa vazi lake kuwa ni mtanzania!
Lete vazi la India lilotajwa kwenye katiba yao kwamba hili litakuwa ndio vazi la kitaifa
 
Back
Top Bottom