Francis fares Maro

JF-Expert Member
Jun 20, 2021
1,089
2,000
Kwanza nipende kukuombe Kwa Mwenyezi Mungu akupatie Umri mrefu wenye mafanikio na hitaji la Moyo wako.

Hakika Wanawake ni Nguzo kuu kwenye kila Hatua kwenye Dunia hii!!.

Mama Samia napenda kukupongeza Kwa hatua kadhaa na jinsi unavyofanya nchi yetu inaenda Kwa kasi sasa.

Mama Samia tukiangalia miezi michache iliyopita Nchi yetu ilipita kwenye kiza kizoto baada ya kuondokewa na Rais aliyekuwa Madarakani lakini Kwa Nguvu za Mungu na Utashi wako hakika tumevuka salama sana.

Mama Samia naona sasa huku mtaani baadhi ya shughuli Kati ya Nyingi zilizokua zimefungwa na kufa sasa zimeanza kurudi Kwa Kasi sana, Uchumi Unaanza kuja taratibu.

Mama Samia sasa kwenye vituo vyetu vya Afya kuna madaktari na wahudumu hata kama sio wengi wa kutosha lakini tunafarijika Kwa juhudi hizi.

Mama Samia Elimu yetu ina suasua sana hapa najua utatufanyia marekebisho makubwa ijapokua tumeona kwenye Elimu ya juu siyo haba umefanya kiasi hongera.

Mama Samia Maendeleo bila nishati ya umeme,Gas ni danganya toto!!. Hapa napenda kukupongeza zaidi sasa umeme tunapata (kuunganishiwa) Kwa bei Ndogo nadhani Tokea timepata Uhuru haijawahi kufikia hivi!!..Upande wa Gas sasa tunaenda kuonganishiwa majumbani kwetu hakika hii ni hatua nzuri sana.

Mama Samia watumishi wa Umma umetufanyia Jambo la msingi sana najua sio kikubwa lakini Kwa hiki kidogo tunamshukuru sana,Ubarikiwe.

Mama Samia ili tuishi na kufarahia mema ya nchi yetu usalama wetu na Mali zetu ni kitu kikubwa sana!!..Kwa hapa napenda kuwapongeza wakuu wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama pamoja na wewe mwenye kama Amiri jeshi mkuu,nchi ipo salama sana

Mama Samia, Bunge letu linafanya Kazi kubwa sana,tunaona sasa wanaweza kusikiliza kero za wananchi na kutatua hata kama sio Kwa 100% lakini tunamshukuru sana.

Kwa Leo naomba niishie hapa.
 

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
9,033
2,000
Kwanza nipende kukuombe Kwa Mwenyezi Mungu akupatie Umri mrefu wenye mafanikio na hitaji la Moyo wako!!

Hakika Wanawake ni Nguzo kuu kwenye kila Hatua kwenye Dunia hii!!....
Mama Samia mbona unawatesa akina Mbowe bila sababu ya msingi? Hujui kwamba wana haki ya kuhoji na kudai katiba mpya?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom